Habari. Naomba nikufunze kitu
1. Vizuri umetaja umri lakini haujata elimu na ujuzi wowote ulionao.
2. Uaminifu ni jambo muhimu lakini kwanza tafuta wadhamini wawili/watatu uwaombe wakudhamini pamoja na barua ya mtendaji wa kata unayotoka au unayokaa. Iwe ni mjini au kijijini. Kwahiyo hapa unapojitangaza ongeza kipengele kinachoainisha kuwa tayari unao wadhamini 3 na barua ya mtendaji wa kata.
3. Taja mji uliopo kwa sasa pia.
4. Na je umeshaoa au la
5. Dini yako pia itaje.
Mwisho, ambatanisha maneno... Niko tayari kufanya kazi kwa kujitolea kwa muda wa mwezi mmoja ili muajiri mtarajiwa aweze kutathmini uwezo wangu.
Haya kafanyie kazi haya kisha juma lijalo uje kuEdit Uzi wako.
Utapata kazi Chap. In shaa Allah
Nakutakia mafanikio kaka