Msaada: Naomba somo la coding

Msaada: Naomba somo la coding

Google Diggers

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2015
Posts
944
Reaction score
1,149
Naomba kujua coding, mimi ni beginner nianzie kitu gani. Nataka niweze kuingia kwenye website niweze kuedit code na kutengeneza scripts.

Kwa sasa naingia natumia ujanja ujanja kuedit, nimeaminiwa na ofisi na ofisi haijui kuna gharama hizo, inabidi nijiongeze. Kila mmoja wetu anajua ajira ni za kubembeleza naomba sapoti.
 
Coding siyo ya kispot spot. Jaribu kupitia kwa mtaalamu huyu.
 
Naomba kujua coding, mimi ni beginner nianzie kitu gani. Nataka niweze kuingia kwenye website niweze kuedit code na kutengeneza scripts.

Kwa sasa naingia natumia ujanja ujanja kuedit, nimeaminiwa na ofisi na ofisi haijui kuna gharama hizo, inabidi nijiongeze. Kila mmoja wetu anajua ajira ni za kubembeleza naomba sapoti.
Usijali mkuu kila kitu kinawezekana, Kwanza kabisa ningependa nijue mpaka sasa unajua nini ili nijue naanza kukusaidia wapil
 
Ndio naanza kuuliza
Cha Kwanza tafuta Eneo lako la kujidai....

Programming ni pana kwa maelezo yako unataka uwe Web developer

Kuna Aina tatu za Web developer...

1.Front End developer
-Hapa uta deal na muonekano wa nje wa website/app yako
(Angalau unapaswa kuwa na basic knowledge ya front end languages Kama HTML,CSS,na JavaScript)

-Html kwa ajiri ya kusuka muundo wa website yako
(HTML inazipa maelezo browsers ipi ni paragraph,ipi ni heading,ipi ni section n.k)

-Ni mark up language...Lugha nyepesi inayotumika kusuka muundo wa web pages

-Css ni Kama rangi inayotumika kupendezesha muonekano wa web pages zako baada ya HTML kumaliza kazi yake
(Jua jinsi ya kuitumia tu,Kuna framework nyingi zitakazo kusaidia, Popular zaidi ni Bootstrap)

-Framework ni nini?
Framework ni 'block of codes' au codes zilizoandikwa tayari kwa ajiri ya kufanya kitu fulani
(Kutengeneza navigation bar,footer, section n.k)
Framework zitarahisisha kazi yako...No need to reinvent the wheel

-Then JavaScript hii itafanya website yako kuwa Interactive
(Kuunda pop up modal...n.k,zinategemea setting za browsers kufanya kazi)

-Bootstrap huwa Ina contain pia bit of JavaScript

-So Kama unataka uwe front end developer,Soma Bootstrap tu...

2.Back End developer
-Hii uta deal na mfumo wa ndani wa website yako(Server side)

-Mara nyingi tunazitumia pale tunapotaka kuunda website ambayo ita store data au information za watumiaji wetu
(Mfano Ecommerce site, Forums n.k)

-Lugha utakazogusa ni Php, Python,ASP,Java n.k

-80% ya website nyingi duniani,zinatumia Php Kama backend language

-Kama kawaida utatumia framework kurahisisha kazi na kuepusha makosa ya kijinga yanayofanywa na novice Php developers

-Kuna frameworks nyingi za php,popular zaidi ni Lavarel
(Na recommend hii kwa sababu ya security na kuzuia tatizo la kuandika codes za hovyoo)
-Mfano wa big site inayotumia php ni Facebook

-Pia Kuna Python....pale unapotaka kuunda website smart zaidi ikiwa na framework yako ya Django
(Mfano wa web app zinazotumia Python Kama backend language ni Instagram, YouTube)

-Pia Kuna SQL,hii ni language inayotumika kuunda database na inasaidia na server side languages kupeleka data kwenye site yako
Ni simple Sana(Readable)

3.Full stack web developer
Huyu yupo vizuri pande zote

Unapiga job ofisini gani?...nichek pm kaka tugawane ugali huo
(X mas sio Mbali)
 
Back
Top Bottom