Msaada naomba kujua duka la Spanish tiles hapa DSM

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,016
32,451
Salaam wadau wa ujenzi,
Naomba kufahamu maduka ya Spanish tiles kwa hapa Dsm.
Of course najua lililopo Victoria,
Lakini ngependa kujua zaidi ili niwwze kufanya ulinganifu wa Bei,na aina tofauti tofauti ili niweze kuchagua.
Pia kama Kuna mtu anafahamu zaidi kuhusu aina nyingine na ubora za tiles zaidi ya Spanish tiles.
Nawashukuruni nyote.
 
CTM wana show rooms mbili moja round about ya Kawe na nyingine ipo Jet ka unaelekea Airport

Screenshot_20220320_100340_com.android.chrome.jpg
 
1. Dar Ceramica pale karibu na Clouds kwenye daraja la Jkt..

2. Inara ceramics hapo Makumbusho

Dar Ceramika wapo K'koo pia wana branches mbili...

CTM pale roundabout mkono wa kulia uelekeo wa Mbezi Beach au maeneo ya Airport...

Pia nishawahi ona Taha ile ya K'koo nayo inauza mzigo wa Spain...

Hata hivyo Indian tiles nazo ni nzuri tu
 
Asante sana
 
Taha ceramic wapo posta ya zamani roundbaout ya kwenda nkurumah na Africana baada ya mataa kuelekea baharini

Espaniola ceramica wapo mwenge ITV junction kuna ghorofa jipya rangi ya kijivu lina madirisha ya vioo pia wapo mikocheni warioba mkabala na shule ya DIS

Spanish tiles hawa wanaongoza kwa bei kubwa ya kutisha wapo victoria.

Swahili ceramics wako Changombe kona ya mbozi road kuna ghorofa liko kama showroom ya tiles na mabomba

Dar ceramica wapo mikocheni mlalakuwa kabla ya JKT makao makuu pia wapo mikocheni warioba kwenye fremu za wapemba. Na eneo la warioba tuu kuna wauzaji wa tiles kama wanne.

Mbezi beach Africana kabla ya Benki ya BOA wanajiita SSL wapo pia Mikocheni Heineken kabla ya shule ya Feza primary.

Jipange mzee Spanish square metre moja inaanzia 55 elfu kuendelea
 
Asante sana Mkuu,Mungu akubariki saana.
Umemaliza Kila kitu.
 
Naskia pwani kama sijakosea kuna kiwanda cha tiles kinaitwa tywford. Naomba mwenye contacts zao anisaidie. Hizi spanish zitanitoa roho kwa kweli
Hizi ni mpauko Ila wanajitajidi kiasi kuliko goodone na goodwill!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom