Msaada namna ya kufikisha malalamiko JWTZ

Katika maisha lazima kuwe na PROFIT and LOSS account

Hili jambo lako liweke katika LOSS account mkuu otherwise ukilazimisha sana utapewa kesi nyingine nzito zaidi
 
Labda utake kusamehe...

Ukienda polisi anaitwa Na atakuja...

Jeshi la Sasa limestaarabika sio kama lazamani...tushaona kesi nyingi tu wanalipishwa ..acha woga!

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
nenda kambini kalianzishe mkuu, uje utupe mrejesho.
Haujamshauri sawa sawa.

Kambi la jeshi hupokea malalamiko madogo madogo ya kiutawala na ya kimadai pamoja na usuluhishi, mfano ndoa, madeni nk nk.

Mambo mengine ya kufungua kesi na mashitaka ni polisi na mahakamani tu.

Jeshi wanaruhusiwa kukamata mtuhumiwa na kumpeleka polisi, lakini hawaruhusiwi kumuweka ndani raia na kumfungulia mashitaka kwenye lockup zao.

Hivyo kwa muktadha huu, hiyo ni traffic case ambayo inafahamika pa kuanzia na pa kuipeleka.

Kosa la barabarani litendwapo na mtu yeyote bila kujali kada yake, sheria hufuata mkondo.

Sema nini, udhaifu na ubabe uliotokea kwenye tukio, umeharibu ushahidi.

Msaada atakaoupata akienda kuripoti polisi pamwe kambini ni mdogo ama wa kupotezeana wakati tu, kutokana na udhaifu wa vielelezo vya kuanzia.
 
Kwa haya Mataifa fukara wa akili ambayo raia wake wamekubaliana na utawala usio wa kisheria na usio na demokrasia huwezi kupata haki yako hapo.Kuna gharama kubwa sana huwa inalipwa kimya kinya kila siku na wananchi kwa kukubali kuwa na Taifa kama hili.
Umenena vema mkuu. Binafsi kwa tukio kama hili nisingemuacha aende hivihivi. Zingepigwa vizuri sana tu as long as kalianzisha yeye. Unadandia gari unasogea dirishani kwake pale unasema naye akueleze kama alichokifanya kipo sawa. Uoga unaumiza wengi na kupoteza haki za wengi sana. Hii haina tofauti na matumizi mabaya ya vyeo. Yaani kisa wewe fulani basi ndo ufanye unachojisikia na kuvunja taratibu zilizowekwa. Mkuu kwa upande wangu, zingepigwa.
 
Kwa Mataifa ambayo hayazingatii utawala wa sheria wala haki za binadamu kama Tanzania angechukua bastola yake kutoka kwenye gari yake kisha anakupiga risasi moja ya paji la uso kisha unakufa hapohapo halafu hakuna kesi wala nini na hata kukiwa na kesi hutatendewa haki.
 
Mkuu binadamu ni kiumbe mzuri sana na pia ni mbaya sana, jinsi wanyama wanavyowindana ndivyo ambavyo hata baadhi ya binadamu huwindana hivyohivyo kwa maslahi binafsi.

Itoshe kusema, ingenitokea zingepigwa vizuri sana. Unapotoka kwako, yeyote unayekutana naye ni rafiki yako pia yeyote unayekutana naye ni adui yako.
 
ungemrushia hata jiwe angesimama tu. Akileta za kuleta mnazichapa tu. ukiona anakuzid unamtia hata kitofa cha kichwa. Usawa huu hamna kumuogopa mtu mzee.
Umenichekesha sana we jamaa, sema kuna siku mzee mmoja mwnajeshi(mkorofi sana) alikuwa barabaran mara ghafla gari ikatokea nyuma ikaikwaruza gari yake ubavuni, ile anahangaika kusimama yule mwenye gari iliyokwaruza gari ya yule dingi, dingi ashashuka chap kumfuata kwa kibabe hatari akashangaa anashuka mdada mrembo alafu kavaa full combat na nyota moja began(luten usu). Manina yule dingi alikuwa SSGT, aling'ata meno kwa hasira akaishia kutoa jambo afande kibao sema yule binti alikuwa mstaarabu sana alimuomba msamaha yakaisha.
 
Vipo vitu vingine lazima upoteze wewe hata kama una haki. Kama umepona potezea tu mkuu,usije ukapewa maumivu mengine huko mbele
 
Wanaboa sana hawa jamaaa. Kuna siku nipo mbele yao na ki gari changu pale mataa ya Chako ni chako sasa taa zikawa zimewaka yani hiyo mihoni wanayonipigia mbele kuna magari pembeni magari sijui walitaka nifanyaje wapo kibaooo kwenye karandinga lao nikasema si ndo ntabinywa hapa mimi leo jamani bahati taa zikawaka nikahama na upande lol.
 
siku nyingine na ww ukimkuta mjeda kasimama kizembe road mplekee boda boda mvunje miguu alfu sepa
 
Back
Top Bottom