Msaada namna ya kufikisha malalamiko JWTZ

G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,771
2,000
Habari za usiku wapendwa katika bwana.

Leo nimepatwa na ajali iliyosababishwa na dereva wa JW aliyekuwa akiendesha gari aina ya hiace ndogo ivi yenye namba 1834 maeneo ya Ofisi za jiji Mwanza.

Nikiwa natokea maeneo ya maji haouse nikiendesha ki TVS changu, nilipofika yalipomataa pale maeneo ya jiji ghafla gari hiyo ili ni overtake upande wangu wa kulia kisha ikakata kona ya ghafla ili kuelekea maeneo ya seketure.

Gari iliniparamia ubavuni na kupelekea kuanguka pembeni, Nikiwa pale chini dereva wa gari husika aliliondoa kwa kasi kiasi cha kusababisha kuendelea kunisukuma zaidi.

Kwavile sikuwa na mwendo mkali sikuumia sana zaidi ya kupata maumivu mguu wa kulia na hii imesababishwa na vile alivyonipush akitokea upande wangu wa kulia, pia pikipiki imepata hitirafu kidogo.

Dereva wa gari husika hakutamka chochote pia hakushuka ndani ya gari, aliendelea na safari yake.

Naomba kufahamu ni vipi nitatoa malalamiko yangu kuhusu hili tukio ili ndugu zetu hawa wawe na nidhamu wanapokuwa barabarani, niende polisi au niende kambini kwao maeneo ya Airport.
kwa kua kuingia kambini kwao ni ngumu maana watakuhoji na ukieleza shida zako wenzie wa getini watamlinda,nenda hapo pembeni ya mahakama pale bwalo la mgambo kuna viongozi wa kijeshi watakusaidia,ukienda traffic police wanaweza wakahisi usumbufu kumtafuta afisa wa Jeshi na wakakupotezea
 
jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
9,756

andamana kama wale vijana 800, yatafika.
 
Emiir

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
24,786
2,000
Ang'ang'anie afu aambiwe amejaribu 'kuteka' gari la jw? Ungekuta yupo ndani saivi..

Aripoti polisi tu, huyo dereva atawasilishwa hapo fasta. Jw hawatetei uhalifu

Hapo na kichapo angekipata, muda mwingine ni muhimu kuwa na namba za Police traffic kwa maeneo husika, ili kuweza kupata msaada wa haraka lakini ukikosa kuwa nazo andika maumivu. Lakini pia kama angekuwepo Traffic eneo hilo angeweza kupata msaada. Lakini pia awe na vitu vyote dereva anavyotakiwa kuwa navyo bila ya hivyo kibao kinamgeukia.
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,374
2,000
Daaah wajeda bwana kuna siku nilipita karibu na geti lao nikaona watu wanarushwa vichura chura. Walifanya? Hata kujua sikutaka nilipita kimya kimya kwa mwendo wa haraka maana wasinge kawia kugeuka na kuniita na mimi nikasomeshwe namba.
Kuna jamaa yangu wakati tuko chuo aliwahi kunichekesha sana. Wanajeshi wako safarini, wakakuta sehemu barabara ni mbovu haipitiki mvua ilikuwa imenyesha sana. Wakaamua kufanya opersheni pale pale, kulikuwa na mawe umbali kidogo ikabidi waanze kusomba mawe na kuyaweka barabarani kama hatua ya dharura. Wao wakaanza kufanya kazi hiyo halafu gari zingine zote zilizokuwa zinafika pale yakiwemo mabasi ya abiria, yaani ile basi linafika tu abiria wote mnashuka haraka sana na kunyoosha moja kwa moja kwenda kuchukua mawe. Wale kama akina makanyaga wanaopenda kuhoji hoji kila kitu na kujishauri shauri, walikuwa wanapata mkong'oto wa uhakika sana zikiwemo fimbo za mgongoni na baada ya hapo mtu anyoosha moja kwa moja kwenda kuchukua mawe bila kuongea au kuuliza maswali. Cheza na jeshi wewe!
 
Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,661
2,000
kwa kua kuingia kambini kwao ni ngumu maana watakuhoji na ukieleza shida zako wenzie wa getini watamlinda,nenda hapo pembeni ya mahakama pale bwalo la mgambo kuna viongozi wa kijeshi watakusaidia,ukienda traffic police wanaweza wakahisi usumbufu kumtafuta afisa wa Jeshi na wakakupotezea
Afisa wa jeshi ni kuanzia mwenye nyota 1 kwenda juu,sio kila mwanajeshi ni Afisa.
 
Janja weed

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
561
1,000
Pita Lugalo ama ngome Upanga tukana sana na jifanye umelewa watakuingiza ndani watakusaidia kukuchukua malalamiko yako very simple
 
kipusaah

JF-Expert Member
Oct 15, 2017
252
250
nenda polisi upew pf3 kwa ajli ya ushahidi utaongozana na traffic mpaka eneo la tukio kwa ajil ya kupima ili hatua zingine zichukuliwe na ukienda polisi lazima utasaidiwa kwa sabab polisi na jw haziivi2. Nenda kwa mshauri wa mgambo mkoa anakuwa office za mkuu wa mkoa pale ukiuliza utapelekwa moja kwa moja na ukatoe malalamiko yako kwake
3’Tafuta namba za mkuu wa kikosi husika naamini utqzipata ukiamua mpe taarifa yako ya malalamiko ni lazima atachkua hatua na utalipwa mm nimeshuhudia hili watu wakilpwa baada ya ktoa taarifa kwa ma CO wa vikosi wa uharibu kama wako
4.nenda kwa mkuu wa wilaya wa kambi hyo iliyo katika himaya yake mpe hizo no atachkua hatua nisikudanganye hakuna lalamiko kubwa na dogo ukilalamika lazima tuu lazima utasidiwa kwa sabab ww sio mtoto ila cha kwanza nenda polisi upewe pf3 utunze ushaid then anza kuhangaika Mungu akutangulie katika hili mm najua jambo la kuonewa linauma sana sana
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
7,672
2,000
Mkuu usiende kambini, wewe nenda ukatengeneze tu pikipiki yako uendelee na shughuli zako! Utakuja unishukuru siku moja!
 
Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
17,419
2,000
Huu usenge wanao hata hawa madereva wa magari ya serikali

Nadhan kuna Haja kubwa ya kuwaambia, Wawapo barabarani wafuate Sheria na taratibu zote za Usalama kama watu wengine.

Wapumbav hawa, hujiona kua barabara ni zao
 
Goodguy

Senior Member
Feb 11, 2018
113
250
Habari za mchana wapendwa katika bwana.

Nawashukuru nyote kwa msaada wa mawazo, yaliyopelekea kufanya maamuzi.

Lengo la kutaka kuripoti tatizo hili haikuwa kufidiwa pesa au kupata msaada, ila tu kuwakumbusha hawa ndugu zetu kuwa na uungwana wanapokuwa barabarani.

Ni jambo tu la kumshukuru Mungu niko hai na niko salama, vinginevyo saivi ningekuwa mlemavu au Mfu.

Nilimshirikisha mzee wangu na kuchanganya na mawazo yenu nikafikia uamuzi wa kuachana nalo ili jambo.

Mtu mmoja amenambia gari iyo japo haikuwa ambulance ila anahisi ilikuwa na mgonjwa aliyekuwa anawahishwa hospitali ya seketure.

Asanteni sana, na nimepata mwanga sasa namna nzuri ya kudeal na changamoto kama hizi.
 
workshop

JF-Expert Member
Oct 16, 2020
266
500

Pole mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom