Msaada: Namna nzuri na ya 'tofauti' ya kutengeneza karanga za mayai

HumbleBoy98

JF-Expert Member
Aug 30, 2020
386
392
Habari zenu wakuu?

Natumai mko POA.

Najua Jf imejaa watu wa Kila Aina wenye uzoefu katika mambo mbalimbali na vichwa vyenye madini ya kutosha!

Hivyo basi wakuu nilikuwa naomba wataalamu wa mapishi mnisaidie namna nzuri na ya tofauti ya kuandaa karanga za mayai. Ninaposema namna ya tofauti namaanisha namna ya uandaaji ambayo ni tofauti na ile iliyozoeleka na wengi ambayo hutumia mchanganyiko wa unga wa ngano, mayai, sukari na chumvi basi Kisha kukaangwa.

Ninachohitaji kujua ni Kama Kuna vitu naweza ongeza ili kufanya karanga hizi ziwe na ladha nzuri zaidi na tofauti kidogo na ile iliyozoeleka na wengi, ni viungo gani vya kuongezea, mbinu za uandaaji n.k.

Nilijaribu kutafuta nyuzi zilizoelezea hii mada humu lakini njia zilizoelezewa na wadau ndo zile zile zilizozoeleka na Mimi nataka nitengeneze kitofauti na ziwe na ladha nzuri zaidi.

Nisaidieni waungwana Maana nakusudia kufanya biashara.

Wataalamu akina farkhina msaada unahitajika hapa tafadhali.

Asanteni nawasilisha
 
Back
Top Bottom