Msaada: Najiandaa kwenda kutambulishwa ukweni kwenye familia ambayo baba na mkwe ni wakorofi

mimi20

Member
Jan 16, 2021
14
24
Nina week nimebakiza niende kujitambulisha ukweni kwenye familia ambayo kwa jinsi binti alivyonieleza baba na mama mkwe ni wakorofi Sana.

Ameniambia pia nijiandae kujibu maswali kwani unaweza kuulizwa maswali ya maudhi yakakutoa kwenye reli au ya kawaida kwani familia yake anailewa jinsi ilivyo na mdomo mdomo soo naombeni ushauri jinsi ya kudeal na hali hii na nijiandaaje siku hiyo?
 
Nahisi hata huyo Binti utakaemchumbia kuna kipindi mkigombana nae atakuwa na vijitabia kama hivyo vya ukorofi wa Wazazi wake.

Nakushauri nenda tu kama huyo Binti mmependana. Maana ndoa ni ya watu wawili, japo wazee wetu siku za nyuma walikuwa wanaangalia na tabia za familia husika kisha wanajua kuwa hamtafika mbali - Ndoa kuvunjika.
 
Mtoto wa kike hufuata tabia za mama yake na mtoto wa kiume hufuata tabia za baba yake,ikitokea mkapishana kauli na mwenza wako wanatakiwa kuwaweka chini wazazi sasa kama wazazi vibati vimelegea jua mtihani huo, hapo chukua hatua mapeeeeeema
 
Ili ufaidi ndoa inabidi utengeneze mazingira aina yeyote ile ile baba na mama mkwe wakuogope kama simba,kinyume na hapo tegemea família yako kuongozwa kwa sheria za baba mkwe!
 
Nina week nimebakiza niende kujitambulisha ukweni kwenye familia ambayo kwa jinsi binti alivyonieleza baba na mama mkwe ni wakorofi Sana.

Ameniambia pia nijiandae kujibu maswali kwani unaweza kuulizwa maswali ya maudhi yakakutoa kwenye reli au ya kawaida kwani familia yake anailewa jinsi ilivyomdomo mdomo soo naombeni ushauri jinsi ya kudeal na hali hii na nijiandaaje siku hiyo?
MUNGU akutangulie
 
Mrejesho leta ulienda.
Ukioa familia wakorofi tegemea kuzaa watoto wakorofi
 
Mrejesho leta ulienda.
Ukioa familia wakorofi tegemea kuzaa watoto wakorofi.Familia wakorofi sio za kuingia nao mkataba
 
Mrejesho leta ulienda.
Ukioa familia wakorofi tegemea kuzaa watoto wakorofi.Familia wakorofi sio za kuingia nao mkataba
 
Back
Top Bottom