Msaada: Nahitaji sehemu nzuri ya kulala Masasi, Mtwara

Nategemea kwenda Masasi, Mtwara mwezi September 2021 kwa wiki moja. Hii itakuwa mara ya kwanza kufika maeneo hayo ya kusini.

Nitashukuru kwa mawazo ya members humu ni wapi maeneo mazuri ya kufikia (guest houses) ambayo ni salama na iko maeneo ya mjini, na yenye gharama za wastani.

Natanguliza shukrani kwa recommendations.

Gharama za wastani taja na bei kabsaa,ila Masasi na mtwara hawako pouwaaa sana kwenye ishu za Malazi/Gest....10000 ni gest za hivyooo na Kwetu sisi wataftaji ndo gharama za wastani,kunguni sasa dah!!!
 
Nilishataja bei, maximum 70,000 per night. Na nimepata suggestions mbalimbali. Ila hiyo mambo ya kunguni, umenitisha kidogo. Nisije wabeba kurudi nao. Hopefully Rock city hotel hawapo.
 
Narudi tena. Nahitaji ushauri wa usafiri kutoka Dar mpaka Masasi kwa anayejua. Nimeambiwa njia mojawapo ni kwenda na ndege mpaka Mtwara mjini na kisha kupanda basi kwenda Masasi (ambayo inachukua kama masaa 4 kutoka Mtwara mjini mpaka Masasi). ila pia nimeambiwa kuna mabasi yanayosafiri kutoka Dar direct mpaka Masasi. Ningependa usafiri wa basi ili kuokoa gharama kubwa za ndege, na pia kujua maeneo mbalimbali basi linapopita. Kwa anayefahamu usafiri wa mabasi, ni basi lipi zuri (luxury bus) linatoka Dar mpaka Masasi? Na wapi stendi yao?, na gharama zake zikoje? Na inachukua wastani wa saa ngapi kutoka Dar mpaka Masasi? Natanguliza shukrani tena kwa msaada. Asante
 
Kukusaidia tu mie nilishawahi kwenda masasi,Usafiri mzuri ni basi ni Maning nice ambalo nina ushahidi nalo nishalipandaga ila zipo kampuni nyingine nazo ni nzuri pia,Na safari ya uko masasi inachukua wastani wa masaa 9 mpaka 10 kwa basi zuri na basi ambalo sio zuri huchukua masaa 11 mpaka kufika pal,ni mji mzuri na gharama zake pia za kulala ni nafuu mie niliendaga kule nikamtafuta bodaboda akanipeleka kwenye lodge ya elfu 10 kiukweli nilienjoi sana mpaka kuondoka,lodge inageti,mlangoni kuna mlinzi na pia kuna parking kubwa na nzuri tu,jitahidi kuanza safari na yale mabasi ya asubuhi sana ili uweze kufika mapema,standi yao mie nilipandaga pale Mbagala ndani ya kituo cha mabasi,kwasasaivi nauli yake itakuwa kati ya 25 hadi 30.mie nilipandaga kwa 20 na kurudi ilikuwa 22 so kwa sasaivi diesel imepanda nahisi itakuwa imeongezeka pia,kila la kheri katika safari yako
 
Nashukuru sana kwa ushauri wako na maelezo muhimu ya kufanikisha lengo langu la kwenda Masasi. Mungu akubariki. Nitawacheki hao Maning Nice.
 
Narudi tena. Nahitaji ushauri wa usafiri kutoka Dar mpaka Masasi kwa anayejua. Nimeambiwa njia mojawapo ni kwenda na ndege mpaka Mtwara mjini na kisha kupanda basi kwenda Masasi (ambayo inachukua kama masaa 4 kutoka Mtwara mjini mpaka Masasi). ila pia nimeambiwa kuna mabasi yanayosafiri kutoka Dar direct mpaka Masasi. Ningependa usafiri wa basi ili kuokoa gharama kubwa za ndege, na pia kujua maeneo mbalimbali basi linapopita. Kwa anayefahamu usafiri wa mabasi, ni basi lipi zuri (luxury bus) linatoka Dar mpaka Masasi? Na wapi stendi yao?, na gharama zake zikoje? Na inachukua wastani wa saa ngapi kutoka Dar mpaka Masasi? Natanguliza shukrani tena kwa msaada. Asante
Kuna maning nice,baraka hii ina VIP,kuna warda,tashirf na nyingine nyingi..nauli 23 hadi 32 kwa vip..pia ni masaa 9 toka dsm to masasi.. barabara ni lami..kituo cha kula ni nagurukuru hapo utakutana na kila aina ya samaki wa bahari..usafiri wa mabasi upo kuanzia sa12 asbu mpka sa8 mchana...karibu kusini.

#MaendeleoHayanaChama
 
Habari ndugu zanguni. Kuna watu walinishangaa katikati ya mwezi June nilivyoomba ushauri wa hotel/guest houses za kufikia Masasi nitakaposafiri mwezi wa September. Ingawa walishangaa naanza maandalizi mapema, lakini pia walinipa ushirikiano na taarifa nzuri tu za mahali pa kufikia na namna ya kupata usafiri wa basi kutoka Dar-Masasi. Nawashukuru wote. September hiyo inaingia. Kwa waliokuwa wanaona September iko mbali, sasa hii hapa inafika. Siku zinaenda kwa speed ya 5G. Nitasafiri ndani ya wiki mbili zijazo kuelekea Masasi. Asante wote kwa michango yenu na ushirikiano mlionipa. Sitakuwa mgeni sana nikifika Masasi ingawa itakuwa mara yangu ya kwanza kufika. Hii ni kutokana na ushauri mzuri nilioupata hapa JF kwa wadau mbalimbali. God bless you all!!
 
Usisahau kondom. Kule masasi xinaadimika Mara kwa Mara. Halafu utasikia Dem akikuambia anajiamini Yuko Safi mtembee hivyo hivyo bila viatu.
 
Mbona hujaleta feedback? BobUpanga
Nilijisahau kuleta feedback kwa kweli. Asante kwa kunikumbusha. Yes, niliweza kwenda Masasi for the first time. Nilifikia kwa ndugu ambao walinishauri nikae kwao. Ila nilitembelea baadhi ya lodges kuona situation. Zile za TZS 10,000 mpaka 15,000 kwa kweli hazikuwa poa, ila siyo mbaya kama huwezi ongeza pesa kidogo kwenda zenye gharama zaidi. Nilipanda Baraka VIP kwenda na kurudi. Ilikuwa Shs 35,000 nadhani each way. Nilipandia Temeke. Sijaona u VIP wa hilo basi, zaidi ya ukubwa wa viti kwenye VIP cabin ambayo iko mbele. Mlango wa kutenganisha VIP na Economy ulikuwa unapiga kelele non-stop, ukichanganya na muziki wa Injili kwenye video ambayo quality ya nyimbo haikuwa nzuri. Ilikuwa makelele zaidi badala ya kiburudisho.

Sehemu nzuri ya starehe ilikuwa Kibo Bar and restaurant, na ilikuwa imechangamka sana siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Kulikuwa na promotion ya beer Saturday, ambayo ilikuwa safi. Pia niliweza kwenda nadhani inaitwa Iwawa night club. Siku hiyo ilikuwa inazinduliwa tena chini ya new management. Walimwalika TID kutoka Dar kuja kutumbuiza. Na pia kulikuwa na vijana wawili local artists walikuwa wanaperform siku hiyo. Hawakuwepo watu wengi siku hiyo hapo Iwawa, na sijaenda tena hapo. Nilikuwa naishia Kibo tu, kwani ndiyo niliona sehemu imechangamka. Usafiri mkuu boda boda. Halafu main street nimeona ni maduka mengi ya magodoro na mitumba ile ya mnada. Siku moja ilikuwa mechi ya simba na yanga nikiwa huko. Simba ilifungwa nadhani bao moja kama sikosei. Mji ulipooza nikajua wengi wa masasi ni wapenzi wa simba. Nilikaa wiki moja na nusu na kurudi Dar

Next trip napanga kwenda Kigoma! Nayo itakuwa mara ya kwanza
 
Back
Top Bottom