MSAADA:Nahisi nimetapeliwa TV mpya

MSAADA:Nahisi nimetapeliwa TV mpya

Hvi hamuwezi kutumia lugha nzuri, kinachokufurahisha hapo nini, roho za kichawi sana hizi, unashadadia nini wakati mwenzako kapata tatizo, mngekuwa vijijini watu wa aina hii ni wangekuwa wachawi tu
Sawa
 
Kuna mtu humu aliweka tangazo anauza smart tv niaamchek akaniambia samsung 43 inches smart TV mpya na box lake eti 630,000 nilishtuka sana.
Nikajua huu ni utapeli na eti unalipia 10% then ukiletewa utamalizia
Nikajiuliza hizo tv anazitoa wapi maana hata zinakotengenezwa haziuzwi bei hyo.
Ogopa vitu cheap
 
Ebay kipindi imeanza watu wamepiga hela mpka $1,000,000 sababu ya biashara ya online lakini Tanzania 325,000 tu mtu anaiba...pole sana mkuu ila watanzania wengi ni wajinga wao wanamlaumu na kumsema vibaya mtu kisa amekosea atajifunzaje kama hajakosea?

Asante sana, wachache wanaelewa.
 
Pole mkuu...hiyo pesa haitamsaidia chochote zaidi ya kumzidishia dhiki..lakini FIGHT FOR WHAT IS YOURS UNTIL THE END..!!
 
UHabari zenu wadau, nilikuwa nahitaji TV nikawa naperuzi mitandaoni kutafuta wauzaji na nikapata hawa wanajiita Electronic Dealers wanauza TV kwa bei nafuu toka Zanzibar na pia wanasafirisha kuja dar na mikoani,nikapata TV kwa 320,000. Jamaa nikaongea naye akasema nitume hela yeye anitumie mzigo,nikamwambia natuma nusu kwanza kiasi cha 200,000 halafu nikipokea mzigo nakamilisha hela. Bahati mbaya siku hiyohiyo kabla sijapokea mzigo nikapata tatizo la ghafla(msiba) na kutakiwa kusafiri haraka nikamwambia tuahirishe zoezi kwanza maana nina tatizo akasema haiwezekani ila nikimaliza mambo yangu nikamilishe hela anitumie.Baada ya siku mbili tatu nikarudi mjini na nikaongea naye akasema poa nimtumie kiasi kilichobaki na anitumie TV kwenye boti ya Azam ya asubuhi mapema kesho yake. Nikatuma hela kiasi kilichobaki 125,000 na ya kutolea ila kuanzia hiyo kesho yake akawa hapokei simu na muda mwingi ipo busy na baadaye ikawa haipatikani kabisa hadi leo hii. Imepita week nzima sasa.

Hela yote imekamilika(nilituma 325,000 jumla) na ushahidi wa msg upo. Sasa katika uchunguzi wangu nikakutana na matangazo kama yaleyale ya mwanzo ya TV yamefanana kila kitu kuanzia jina la kampuni, uandishi wa tangazo,location(ZNZ) na hadi bei za TV ila namba ndio tofauti. Nimepiga jana usiku aliyepokea akasema nipige leo asubuhi akiwa ofisini,leo wanasema haifahamu hiyo namba nyingine.

Hapa chini ni link la tangazo lake la awali ambalo nilinunua hiyo TV na namba ipo 0715606457,
Samsung 32 Inches Led HD Tv Zanzibar Central/South 86869875
na hii nyingine ni link ya tangazo jipya kwa namba nyingine Samsung Led 32 Inches Flat Screen Zanzibar Central/So883087
Naomba anayewafahamu hawa watu anisaidie namna ya kuwapata ili niweze kupata TV au kiasi changu cha fedha 325,000.

Nitaweka screenshot ya msg tulizokuwa tunawasiliana.

UPDATE:
Jamaa leo amepatikana kwenye simu anasema alikuwa safarini. Ameniblock, nikitumia simu nyingine anakata.
Nenda hospitali haraka, inaonekana una matatizo ya kichwa maana umeibiwa kizembe sana mkuu.

Nadhan una malaria kali
 
Back
Top Bottom