MSAADA:Nahisi nimetapeliwa TV mpya

MSAADA:Nahisi nimetapeliwa TV mpya

Deleted_account

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2008
Posts
3,385
Reaction score
3,702
UHabari zenu wadau, nilikuwa nahitaji TV nikawa naperuzi mitandaoni kutafuta wauzaji na nikapata hawa wanajiita Electronic Dealers wanauza TV kwa bei nafuu toka Zanzibar na pia wanasafirisha kuja dar na mikoani,nikapata TV kwa 320,000. Jamaa nikaongea naye akasema nitume hela yeye anitumie mzigo,nikamwambia natuma nusu kwanza kiasi cha 200,000 halafu nikipokea mzigo nakamilisha hela. Bahati mbaya siku hiyohiyo kabla sijapokea mzigo nikapata tatizo la ghafla(msiba) na kutakiwa kusafiri haraka nikamwambia tuahirishe zoezi kwanza maana nina tatizo akasema haiwezekani ila nikimaliza mambo yangu nikamilishe hela anitumie.Baada ya siku mbili tatu nikarudi mjini na nikaongea naye akasema poa nimtumie kiasi kilichobaki na anitumie TV kwenye boti ya Azam ya asubuhi mapema kesho yake. Nikatuma hela kiasi kilichobaki 125,000 na ya kutolea ila kuanzia hiyo kesho yake akawa hapokei simu na muda mwingi ipo busy na baadaye ikawa haipatikani kabisa hadi leo hii. Imepita week nzima sasa.

Hela yote imekamilika(nilituma 325,000 jumla) na ushahidi wa msg upo. Sasa katika uchunguzi wangu nikakutana na matangazo kama yaleyale ya mwanzo ya TV yamefanana kila kitu kuanzia jina la kampuni, uandishi wa tangazo,location(ZNZ) na hadi bei za TV ila namba ndio tofauti. Nimepiga jana usiku aliyepokea akasema nipige leo asubuhi akiwa ofisini,leo wanasema haifahamu hiyo namba nyingine.

Hapa chini ni link la tangazo lake la awali ambalo nilinunua hiyo TV na namba ipo 0715606457,
Samsung 32 Inches Led HD Tv Zanzibar Central/South 86869875
na hii nyingine ni link ya tangazo jipya kwa namba nyingine Samsung Led 32 Inches Flat Screen Zanzibar Central/So883087
Naomba anayewafahamu hawa watu anisaidie namna ya kuwapata ili niweze kupata TV au kiasi changu cha fedha 325,000.

Nitaweka screenshot ya msg tulizokuwa tunawasiliana.

UPDATE:
Jamaa leo amepatikana kwenye simu anasema alikuwa safarini. Ameniblock, nikitumia simu nyingine anakata.
 
We tulia tu. Ushapigwa.
Kila siku mnaimbiwa hapa usilipe hela kabla ya kupokea mzigo.
Sasa thread zimejaa hapa kila siku, na bado UNATAPELIWA ??
Zanzibar pana umbal gan,si ungeenda kuchukua mwenyewe???

Yani huwa najiulizaga inakuaje utapeli WA ain moja unafanikiwa kwa watu wengi na japo tahadhar ishatolewa.

NIMEGUNDUA MABOYA BADO MPO....

pole kwa lugha yangu km nimeekuudh.
 
Pole sana, ripoti polisi kwanza watamtafuta kwa cyber hiyo kitu usiombe ikutokee
 
Ukome...
wajinga ndio waliwao...
koma tena sana...
Hujifunzi tu kutoka kwa wengine????
 
Kila siku tunapiga kelele uku usinunue kitu bila ya kuhakikisha mzigo uko mikononi mwako.
Mtaendelea kutapeliwa mpaka mkome
 
pole sana ndugu yang ila fatilia kwanza kafungue kesi polisi then ukimkamata akulipe na gharama zako za kumtafta ila ntakupa msaada wa kuhakikisha unampata uyo mtu
 
Jaribu kupeleka haya maelezo polisi wanaweza kujusaidia zaidi kuliko wana JF watakuingezea machungu tu pole sana, au tafuta mtu unae mfahamu aliepo znzbr afike ofisini kwao hapo.
 
Pole sana Mkuu, mbona tena nimekuona kule kwenye post ya kuuziana TV unaagiza kutoka huko huko zenji,imekaaje hapo mkuu
 
Jaribu kupeleka haya maelezo polisi wanaweza kujusaidia zaidi kuliko wana JF watakuingezea machungu tu pole sana, au tafuta mtu unae mfahamu aliepo znzbr afike ofisini kwao hapo.
Mkuu huku sijawahi kusikia jina la hiyo kampuni nipo mtendeni mtaa unaongoza kwa maduka ya electronics huku, na hata maduka yaliyoko ng'ambo mengi nayajua, kwa mchina, magomeni mlandege sijawah kusikia hilo duka..
Inawezekana huyo hata hayuko huku zanzibar na hana hata duka, aneamua tu kutumia hiyo identity ili kuwavuta watu, pole mkuu nadhani ungelipeleka huli kituo cha polisi ili kulifuatilia kuliko kuja huku pengine hata hayupo zanzibar
 
Pole sana Mkuu, mbona tena nimekuona kule kwenye post ya kuuziana TV unaagiza kutoka huko huko zenji,imekaaje hapo mkuu
Ameagiza kwangu mi sinaga hizo mkuu hata ukitaka nikuletee ndo ulipe mzigo mi sina tatizo maana ndo kazi yangu sina ubabaishaji
 
Habari zenu wadau, nilikuwa nahitaji TV nikawa naperuzi mitandaoni kutafuta wauzaji na nikapata hawa wanajiita Electronic Dealers wanauza TV kwa bei nafuu toka Zanzibar na pia wanasafirisha kuja dar na mikoani,nikapata TV kwa 320,000. Jamaa nikaongea naye akasema nitume hela yeye anitumie mzigo,nikamwambia natuma nusu kwanza kiasi cha 200,000 halafu nikipokea mzigo nakamilisha hela. Bahati mbaya siku hiyohiyo kabla sijapokea mzigo nikapata tatizo la ghafla(msiba) na kutakiwa kusafiri haraka nikamwambia tuahirishe zoezi kwanza maana nina tatizo akasema haiwezekani ila nikimaliza mambo yangu nikamilishe hela anitumie.Baada ya siku mbili tatu nikarudi mjini na nikaongea naye akasema poa nimtumie kiasi kilichobaki na anitumie TV kwenye boti ya Azam ya asubuhi mapema kesho yake. Nikatuma hela kiasi kilichobaki 125,000 na ya kutolea ila kuanzia hiyo kesho yake akawa hapokei simu na muda mwingi ipo busy na baadaye ikawa haipatikani kabisa hadi leo hii. Imepita week nzima sasa.

Hela yote imekamilika(nilituma 325,000 jumla) na ushahidi wa msg upo. Sasa katika uchunguzi wangu nikakutana na matangazo kama yaleyale ya mwanzo ya TV yamefanana kila kitu kuanzia jina la kampuni, uandishi wa tangazo,location(ZNZ) na hadi bei za TV ila namba ndio tofauti. Nimepiga jana usiku aliyepokea akasema nipige leo asubuhi akiwa ofisini,leo wanasema haifahamu hiyo namba nyingine.

Hapa chini ni link la tangazo lake la awali ambalo nilinunua hiyo TV na namba ipo 0715606457,
Samsung 32 Inches Led HD Tv Zanzibar Central/South 86869875
na hii nyingine ni link ya tangazo jipya kwa namba nyingine Samsung Led 32 Inches Flat Screen Zanzibar Central/So883087
Naomba anayewafahamu hawa watu anisaidie namna ya kuwapata ili niweze kupata TV au kiasi changu cha fedha 325,000.

Nitaweka screenshot ya msg tulizokuwa tunawasiliana.
Pole sana. Ila wahenga walisema always "cheap is expensive". Kilichokuponza ni tamaa iliyokuzuia kutazama vyema! Ulikuwa unawasiliana na mtu au kampuni! Pole sana. TV mtumba zipo nyingi tu, nauli ya boti Zanzibar ni Tshs 20,000/= ukichukua hiyo X 2 unapata go and return. Au ungeweza tafuta ndugu ama tuma mtu. Ai salama sana kufanya malipo kwa njia ya mitandao kwa mazingira ambayo huna uhakika nayo. Kwa kuwa una ushahidi, kafungue kesi ya utapeli, nenda kaombe watu wa mitandao per haps wataweza saidia kufuatilia and the like. Next time kuwa muangalifu zaidi.
 
Back
Top Bottom