MSAADA:Nahisi nimetapeliwa TV mpya

MSAADA:Nahisi nimetapeliwa TV mpya

Ebay kipindi imeanza watu wamepiga hela mpka $1,000,000 sababu ya biashara ya online lakini Tanzania 325,000 tu mtu anaiba...pole sana mkuu ila watanzania wengi ni wajinga wao wanamlaumu na kumsema vibaya mtu kisa amekosea atajifunzaje kama hajakosea?
 
Ebay kipindi imeanza watu wamepiga hela mpka $1,000,000 sababu ya biashara ya online lakini Tanzania 325,000 tu mtu anaiba...pole sana mkuu ila watanzania wengi ni wajinga wao wanamlaumu na kumsema vibaya mtu kisa amekosea atajifunzaje kama hajakosea?
Mkuu mi naamini huyu si mfamyabiashara, mfanyabiashara hawezi kuingia mitini kwa laki 3 hata siku moja, yule ni tapeli tu, tangazo kama lile mtu yeyote anaweza kuliweka
 
Pole kwa yaliyokutokea.

Na nyie mnaomcheka hamna adabu, utafikiri mnajua kila kitu duniani.

Ripoti polisi na utie namba yake na print za screenshot zako. Ili pia usizipoteze jitumie kwenye e-mail zikae huko hata ukiziitaji baadae zitakuwepo kukusaidia ushaidi.
 
Mimi sikulaumu nakupa pole mana muda mwingine unatapeliwa halafu ukija kujifikiria unajiona mjinga.
Tatizo watu tunapenda rahisi halafu tunasahau rahisi aghali.
Ni bora kufanya makabidhiano ana kwa ana nakupa pesa unanipa mzigo mana wabongo hatuna uaminifu kabisa.
Muda mwingine huwa naona bora kulipa aghali dukani kuliko kutapeliwa.
Ununuzi wa namna hiyo yako unahitaji umakini wa hali ya juu.
 
Mie sina tatzo nae.. Pic nishafuta, nmekereka kuniita tapeli tu wakat sikuwa na nia n biashara tuliipiga frwsh kabsa..

Yote kwa yote maisha yanaendelea baada ya mambo yote, wote wa hapa town kuna leo na kesho..

Aniwie radhi ambapo nimemkosea haikuwa dhumuni kumuanika ila kuonesha ni jins gani biashara ilitendeka..
Blessed Brother kwa Uungwana wako
Unajua Binaadam hatupo sawa.
 
UPDATE:
Jamaa leo amepatikana kwenye simu anasema alikuwa safarini. Ameniblock nikitumia simu nyingine anakata,namba yake ni 0715606457
 
Ukisikia Kupatwa kwa jua Mbalali- Mbeya ndiyo Kama hivi umeshampa Mpemba pesa ya kuolea mke wa 4 kirahisi kabisa
Pole sn mkuu.
 
Ameagiza kwangu mi sinaga hizo mkuu hata ukitaka nikuletee ndo ulipe mzigo mi sina tatizo maana ndo kazi yangu sina ubabaishaji
Sony flat screen, lcd HD, 50 inches ni bei gani ukiniletea hapa daslaam?
 
Habari zenu wadau, nilikuwa nahitaji TV nikawa naperuzi mitandaoni kutafuta wauzaji na nikapata hawa wanajiita Electronic Dealers wanauza TV kwa bei nafuu toka Zanzibar na pia wanasafirisha kuja dar na mikoani,nikapata TV kwa 320,000. Jamaa nikaongea naye akasema nitume hela yeye anitumie mzigo,nikamwambia natuma nusu kwanza kiasi cha 200,000 halafu nikipokea mzigo nakamilisha hela. Bahati mbaya siku hiyohiyo kabla sijapokea mzigo nikapata tatizo la ghafla(msiba) na kutakiwa kusafiri haraka nikamwambia tuahirishe zoezi kwanza maana nina tatizo akasema haiwezekani ila nikimaliza mambo yangu nikamilishe hela anitumie.Baada ya siku mbili tatu nikarudi mjini na nikaongea naye akasema poa nimtumie kiasi kilichobaki na anitumie TV kwenye boti ya Azam ya asubuhi mapema kesho yake. Nikatuma hela kiasi kilichobaki 125,000 na ya kutolea ila kuanzia hiyo kesho yake akawa hapokei simu na muda mwingi ipo busy na baadaye ikawa haipatikani kabisa hadi leo hii. Imepita week nzima sasa.

Hela yote imekamilika(nilituma 325,000 jumla) na ushahidi wa msg upo. Sasa katika uchunguzi wangu nikakutana na matangazo kama yaleyale ya mwanzo ya TV yamefanana kila kitu kuanzia jina la kampuni, uandishi wa tangazo,location(ZNZ) na hadi bei za TV ila namba ndio tofauti. Nimepiga jana usiku aliyepokea akasema nipige leo asubuhi akiwa ofisini,leo wanasema haifahamu hiyo namba nyingine.

Hapa chini ni link la tangazo lake la awali ambalo nilinunua hiyo TV na namba ipo 0715606457,
Samsung 32 Inches Led HD Tv Zanzibar Central/South 86869875
na hii nyingine ni link ya tangazo jipya kwa namba nyingine Samsung Led 32 Inches Flat Screen Zanzibar Central/So883087
Naomba anayewafahamu hawa watu anisaidie namna ya kuwapata ili niweze kupata TV au kiasi changu cha fedha 325,000.

Nitaweka screenshot ya msg tulizokuwa tunawasiliana.

UPDATE:
Jamaa leo amepatikana kwenye simu anasema alikuwa safarini. Naendelea kuwasiliana naye.
My take
Kutokana na mkasa wako iwe fundisho kutopenda MTEREMKO maana short cut is a wrong cut.
 
Unapo nunua kitu mtandaoni hutakiwi kulipa moja kwa moja.
Unatakiwa kulipa on delivery.
Ila pole sana.

Me mwenyewe na nunuaga na kuuza sana vitu huko kupatana.
But huwa nalipa na kulipwa wakati bidhaa nimeshaiona kwa macho na kuigusa na kuitest pia.

That is pay on delivery
 
Ukome...
wajinga ndio waliwao...
koma tena sana...
Hujifunzi tu kutoka kwa wengine????
Hvi hamuwezi kutumia lugha nzuri, kinachokufurahisha hapo nini, roho za kichawi sana hizi, unashadadia nini wakati mwenzako kapata tatizo, mngekuwa vijijini watu wa aina hii ni wangekuwa wachawi tu
 
Back
Top Bottom