TRA kuna vilaza pia hasa wanafunzi walioko kwenye mazoezi ya vitendo na wakongwe waliokwama kwenye ufanyaji kazi kimazoea na hawako tayari kubadilika..., kwa kawaida unatakiwa kujaza fomu ya kuomba TIN ya biashara au hiyo uliyonayo inabadilishwa kuwa ya biashara. Mchakato huo hufanyika kwenye kaunta yoyote ya ofisi za TRA.... Sio lazima uende kule ulikopatia TIN, Tumia ofisi za kikanda.
Rudi tena ofisi ya TRA kesho usingoje zege lipoe, omba kuonana uso kwa uso na Manager wa TRA kwenye kanda hiyo utafanikiwa tu. Uzoefu wangu kwenye ofisi zetu hizi ni kuwa wewe mwenye shida unatakiwa ujue unataka nini kwa asilimia mia, na uhakikishe unasimamia unachokitaka ukipate, mradi huvunji sheria.