Msaada: Nawezaje kupunguza deni ninalodaiwa TRA kutokana na biashara (Sio yangu) iliyofunguliwa na TIN number yangu?

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
3,468
8,289
Habari zenu wadau! Kuna ushu moja hapa imetokea.

Kuna huyu jamaa yeye alitumia jina lake kuweza kuwasaidia wadogo zake na mchepuko wake kuwafungulia biashara kwa kutumia TIN namba yake.

Amekuja kushtuka hawa watu walikua wameacha kulipa makadirio ya kila term na kusababisha mrundikano mkubwa wa madeni na faini.

Dogo wa kwanza baada ya kufunguliwa biashara, biashara ikamshinda na kukimbilia kuajiriwa na huku akimficha bro yake. Bro alipo kuja kumuuliza kazini kwake amemuacha Nani alijibu atarudi ile biashara kaifunga kwa muda.

Akamuuliza tena TRA wanajua hiyo ishu akajibu ndio. Bro kwakua anamambo mengi na ratiba tight akaona poa isiwe ishu . Kumbe dogo hajafanya hayo tangu 2017.

Dogo wa pili huyu ni huyu yalipo kuja masuala ya kuolewa nae biashara ikafa hivo hivo nae hakufunga biashara TRA bado Deni linasoma. Huyu tangu 2020.

Kwa mchepuko huyu yeye ni mwanamke wake wa siku nyingi ni wale wanawake ambao ndoa inakukuta tayari upo nao yaani mnaiva Sana Ila sijui inatokea nn mnashindwa kuoana Ila mambo mengine Kama kusaidiana na kuwezeshana bado yanaendela bila kusahau kunyanduana.

Hivyo basi huyu mchepuko ...Basi huyu mwanamke nae alilimbikiza Kama Kama miezi sita hivi ile kwenye kwenda kufuatilia ndio akaambiwa na hayo maana aliulizwa biashara ni ya Nani akasema yeye ameajiriwa hivyo katumwa na boss .

Ndipo alipo ambiwa akamwite boss maana Kuna madeni mengine yanatakiwa kulipwa . Mwanamke kusikia hivyo akaenda kumuomba msamaha na msaada bro kwa kulimbikiza madeni baada ya kufikiwa maelewano bro akajipeleka tra ndipo kuambiwa utumbo wote uliopo.

Bro kakuta anadaiwa milioni 37 hapa kichwa kimewaka hajui aanzie wapi amalizie wapi Ila pale TRA aliambiwa alipe na hili deni bado linakua.

Sasa msaada anaomba Kama Kuna njia nyingine za kuweza kulifuta . Mchango wako ni wa msingi maana Kuna wahanga wengi wa hii ishu labda tunaweza pata msaada.
 
Kama ni mkoa wa Ilala au Kinondoni nicheki PM kwa kutumia hii hii handle unayotumia hapa JF na si vinginevyo
 
Fanya mpango uifunge biashara iyoofunga na TIN namba alafu kaa miezi miwiliufungue mpya
 
Aisee kuna mtu alitaka nikamsaidie kupata Tin na kitambulisho changu nikawaza hapa uu jinga
 
Back
Top Bottom