Msaada mwepesi na waharaka wa kubadili TIN namba isiyokuwa ya kibiashara kwenda ya kibiashara

King Sae

JF-Expert Member
Mar 22, 2018
2,795
5,264
Naona Staff wa TRA wa uku nilipo siwaelewi kabisa,wanafanya mambo yawe magumu...

Mwaka 2017 nikiwa Dar es salaam nilipata TIN namba lakini ilikuwa si kwa ajiri ya biashara (non business use),niliipata nkiwa ktk harakati za mafunzo ya udereva.

Kwa sasa nipo mkoa wa nyanda za juu uku ktk harakati za kutafuta maisha,nimeenda TRA wanibadilishie hii TIN namba yangu isome special kwa ajiri ya biashara....lakini nasikitika napewa story za kurudi tena dar Kwenye ofisi nilipopatia hii TIN namba Ili wafanye transfer isome mkoa niliopo sasa,na ndo zoezi la kubadili kwenda Kwenye matumizi ya kibiasha lifanyike...

Nikawaambia basi isiwe case,mnitengenezee TIN mpya wanasema haiwezekana kwasababu tayari una namba ya TIN.

Msaada kama kuna mtu anaufahamu kuhusu hili issue.
 
Hao wanatengeneza mazingira ya rushwa, Mimi nilibadili kutoka Iringa kuja Mkoa wa kikodi Ilala bila kwenda Iringa, nilijaza fomu pale Vingunguti ya kuhamisha Tin kutoka Iringa kuja Ilala baada ya wiki moja ikahamishwa taratibu za kubadili matumizi zikaendelea.
 
TRA kuna vilaza pia hasa wanafunzi walioko kwenye mazoezi ya vitendo na wakongwe waliokwama kwenye ufanyaji kazi kimazoea na hawako tayari kubadilika..., kwa kawaida unatakiwa kujaza fomu ya kuomba TIN ya biashara au hiyo uliyonayo inabadilishwa kuwa ya biashara. Mchakato huo hufanyika kwenye kaunta yoyote ya ofisi za TRA.... Sio lazima uende kule ulikopatia TIN, Tumia ofisi za kikanda.

Rudi tena ofisi ya TRA kesho usingoje zege lipoe, omba kuonana uso kwa uso na Manager wa TRA kwenye kanda hiyo utafanikiwa tu. Uzoefu wangu kwenye ofisi zetu hizi ni kuwa wewe mwenye shida unatakiwa ujue unataka nini kwa asilimia mia, na uhakikishe unasimamia unachokitaka ukipate, mradi huvunji sheria.
 
Andika barua ya kuomba kuihamisha hiyo tin namba kutoka ulikoipatia ije hapo ulipo/unapotaka kufanyia biashara Kisha meneja wa eneo Hilo atawasiliana na meneja wa kule ilipo tin namba yako na kuhamisha taarifa zako.

Nb
Usitoe rushwa huduma hiyo ni bure.
 
Mi nilihamisha from Temeke to Kinondoni Bure.

Just nenda Mahala unapotaka iamie, andika barua kwa Meneja.

Tena uzuri siku hizi ni form unajaza sio barua.
 
TRA kuna vilaza pia hasa wanafunzi walioko kwenye mazoezi ya vitendo na wakongwe waliokwama kwenye ufanyaji kazi kimazoea na hawako tayari kubadilika..., kwa kawaida unatakiwa kujaza fomu ya kuomba TIN ya biashara au hiyo uliyonayo inabadilishwa kuwa ya biashara. Mchakato huo hufanyika kwenye kaunta yoyote ya ofisi za TRA.... Sio lazima uende kule ulikopatia TIN, Tumia ofisi za kikanda.

Rudi tena ofisi ya TRA kesho usingoje zege lipoe, omba kuonana uso kwa uso na Manager wa TRA kwenye kanda hiyo utafanikiwa tu. Uzoefu wangu kwenye ofisi zetu hizi ni kuwa wewe mwenye shida unatakiwa ujue unataka nini kwa asilimia mia, na uhakikishe unasimamia unachokitaka ukipate, mradi huvunji sheria.
Daah shukran mkuu....hakika nmekuelewa vzur ntafanya hvyo
 
Andika barua ya kuomba kuihamisha hiyo tin namba kutoka ulikoipatia ije hapo ulipo/unapotaka kufanyia biashara Kisha meneja wa eneo Hilo atawasiliana na meneja wa kule ilipo tin namba yako na kuhamisha taarifa zako.

Nb
Usitoe rushwa huduma hiyo ni bure.
Shukran sanaa mkuu..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom