Msaada Mwanangu ananifirisi...

Msaada Mwanangu ananifirisi...

Mtoto kama huyo ungekuwa mtaalam wa IT unamfungulia computer lab, anaweza akaja kuwa wa maana sana baadaye.
Daah wazungu wametushinda mengi.
Akili za kiafrica hapa zinawaza dogo kudundwa tu. Sijui nani wakuja kutuokoa.
Afrika mtoto akiwa mtundu anaonekana hafai.
Msaidie dogo huyo.
 
Namcharaza kwa kosa gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
anzisha sasa kosa ili umchape, mfano:
Baba: " hakuna kudownload tena youtube sawa?"
Mtoto: " Sitaki, mimi nataka hiyoooo"
Baba: " Nitakucharaza bakora wewe husikii?"
Mtoto: " Sitaki"
hapo sasa unaweza kuanza kutumia bakora kujulisha kwa vitendo kuwa ni marufuku kudownload
 
Mtafutie michezo inayoendana na umri wake mfano simu ya plastick ya watoto.
Kumridhisha mtoto kwa kumpa kila kitu anacholilia haiwezekani. Akilia akiona haisaidii atanyamaza tu.
Mtoto wa umri huo usimpe kabisa smart fone. Hata macho yake hayako tayari kumudu smart fone (eye strain)
 
Yaa
Huyu dogo zamani kipindi ana miaka2 nilikuwa namwekea video za cartoon za kudownload zile ndefu ....kwa sasa ana miaka 3.2 ndugu nilimfundisha kuangalia video YouTube Leo najuta....
Hataki za kudowload anataka kuangalia mwenyewe YouTube tena anachagua anayotaka...
Nadhani unaelewa mchakato wa bando...ukimkataza kilio chake ci mchexo yaniiii...
Naomba ushauri nimfanye nn...
Pesa ngumu siwexi kuweka bajeti ya bando daily kwa ajili yake majukumu mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani wewe unaogopa kilio cha mtoto anayelilia bando?unapiga ngwara moja anatulia halafu unampa utaratibu mzima.
 
Mtoto kama huyo ungekuwa mtaalam wa IT unamfungulia computer lab, anaweza akaja kuwa wa maana sana baadaye.
Daah wazungu wametushinda mengi.
Akili za kiafrica hapa zinawaza dogo kudundwa tu. Sijui nani wakuja kutuokoa.
Afrika mtoto akiwa mtundu anaonekana hafai.
Msaidie dogo huyo.
Hata hao wazungu hawawapi watoto wao wadogo simu wastream youtube wanawapa vitu vianvyoendana na umri wao.Marehemu Steve Jobs na kuwa CEO wa apple lakini hakuwa anaruhusu watoto wake kutumia vitu kama iphone au ipod katika umri wao halikuwa haruhusu kabisa.
Sasa sisi kwa ulimbukeni kisa mtu ana ela unakuta kitoto cha miaka 7 kakinunulia smartphone halafu anajisifu mwanaye ana akili sana anaweza tumia smartphone kuja kushtuka kitoto kinatazama ngono kina tabia za ajabu ajabu.
Hata hizo cartoon zinabidi ziendani na umri wa mtoto kuna cartoon hazifai kutazamwa na watoto watu wakiona mikatuni/animation wanahisi ni kwa ajili ya watoto kumbe nyingine zimetengezwa kwa ajili ya watu kuanzia miaka 16
 
Akitoka kwenye cartoon ataanza kutazama x tena kama ni wa kiume atakutana na za mashoga basi kwisha khabar yake yakhee make ndo hivo KAUTIA GUU NCHUZI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio tabia za akina mama baadhi yao, mimi niko na mtoto wangu sasa hivi miaka minne alikua na tabia kama za mtoto wako.. Mbona kaacha!? Eti lazima apewe smartphone nilikua nikimpa ya toch haitaki. Ikafika kipindi nikamwambia kuanzia sasa hakuna ruhusa ya kugusa sim.. Alitii amri na kuniogopa hadi leo nikiwekewa kitu hata kama anakipenda kiasi gani.. Akiambiwa "cha baba yako" anakiangalia kama hakitaki maana sikumdekeza nilimcharaza bakora sasa hivi kawa mtii kwa baba lakini sio kwa mama.. Anamtii mama yake nikiwepo ila nilimwambia nikiondoka mama yake anapata tabu sana maana wanawadekeza sana.
Eti siku hiyo namkunja mtoto mama yake anaingilia nikakwambia ukithubutu kuja na wewe nakutandika mbona kaacha?

**Mpemba halisi**
 
Huyu dogo zamani kipindi ana miaka2 nilikuwa namwekea video za cartoon za kudownload zile ndefu ....kwa sasa ana miaka 3.2 ndugu nilimfundisha kuangalia video YouTube Leo najuta....
Hataki za kudowload anataka kuangalia mwenyewe YouTube tena anachagua anayotaka...
Nadhani unaelewa mchakato wa bando...ukimkataza kilio chake ci mchexo yaniiii...
Naomba ushauri nimfanye nn...
Pesa ngumu siwexi kuweka bajeti ya bando daily kwa ajili yake majukumu mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto wa miaka mitatu anakuumiza kichwa akifika 16 je?
 
Mtoto wa miaka mitatu anakupelekesha, je akifikisha miaka 15?
 
Back
Top Bottom