Msaada: Mwanangu amekuwa addicted na catoon (katuni)

kuchangumu

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
724
Reaction score
290
Salama wakuu!

Mimi nina mtoto wa miaka 5 mtoto huyu anapenda sana katuni anaweza kuangalia katuni asubuhi mpaka jioni bila kuchoka

Na ikitokea ukizima Tv ni kilio mtindo mmoja mpaka uwashe

Kuhusu shule anasoma chekechea na huwa nikimpaga home work natumia nguvu za ziada sababu ya katuni

Je kuangalia katuni kwa masaa mengi kunaweza kumwadhiri?

Au katuni zinaweza kumjengea uwezo zaidi?

Naombeni kueleweshwa wanajamvi natarajia majibu mazuri kutoka kwenu
 
Natumai ulimaanisha kumuathiri.

Jibu ni ndio, anaweza kuathirika kisaikolojia na hata kimwili kwani anaweza kuiga mambo yanayofanywa na vikatuni akajiumiza au kuumiza wenzake.

Kila kitu kina limit zake. Anza kumbadilishia utaratibu, awe na wakati maalum wa kutazama katuni, nzuri zaidi ni zile zenye kufundisha. Awe na muda wa kusoma, hii unaanza kumzowesha kwa wewe kumsomea vitabu vyenye hadithi za kitoto zenye mafunzo, kumbuka, siyo kumhadithia, kumsomea. Awe na wakati wa kucheza, awe na wakati wa kupumzika.

Nakushauri google "child rearing" utapata kujifunza mengi, kuna kila aina ya mafunzo kuhusu kulea mtoto vyema.

Kama ana bibi, shangazi au ahli zake wako shamba (kijijini) mpeleke akakae nao kwa muda wa miezi miwili au mitatu atabadilika.
 
Asante sana sana nashukuru kwa msaada wako nitatekeleza
 
Salama wakuu!

Mimi nina mtoto wa miaka 5 mtoto huyu anapenda sana katuni anaweza kuangalia katuni asubuhi mpaka jioni bila kuchoka

Na ikitokea ukizima Tv ni kilio mtindo mmoja mpaka uwashe

Kuhusu shule anasoma chekechea na huwa nikimpaga home work natumia nguvu za ziada sababu ya katuni

Je kuangalia katuni kwa masaa mengi kunaweza kumwadhiri?

Au katuni zinaweza kumjengea uwezo zaidi?

Naombeni kueleweshwa wanajamvi natarajia majibu mazuri kutoka kwenu

asiangalie sana muda mwingine mwache acheze game kwa computer.
 
Ni tatizo kubwa sana kwa sababu akili yake itakua imeconcentrate sana kwenye katuni. kwa time zote ndani ya kichwa chake anakua anafikiria katuni tu, mwisho akili yake itakua haifanyi kazi kwenye masomo na ataanza kukwambia masomo magumu bado yuko mdogo. Mkataze au weka television chumbani au ifiche rimote
 
Salama wakuu!

Mimi nina mtoto wa miaka 5 mtoto huyu anapenda sana katuni anaweza kuangalia katuni asubuhi mpaka jioni bila kuchoka

Na ikitokea ukizima Tv ni kilio mtindo mmoja mpaka uwashe

Kuhusu shule anasoma chekechea na huwa nikimpaga home work natumia nguvu za ziada sababu ya katuni

Je kuangalia katuni kwa masaa mengi kunaweza kumwadhiri?

Au katuni zinaweza kumjengea uwezo zaidi?

Naombeni kueleweshwa wanajamvi natarajia majibu mazuri kutoka kwenu
While parenting is a joy, it's also hard work which is whyI'm sharing these effective and loving parenting techniques
There are six main parenting Tips, and your child fall underParenting Tip no 5&6:
Loving Parenting Tip #5- Structure
In order to feel safe and to learn boundaries, children need a regular scheduleof meals, naps, bedtimes, and other activities. Try posting a schedule whereyour children can view it as well as making clear the family rules and whatconsequences will take place should they break those rules.

Loving Parenting Tip #6- Consistency
Family Rules need to be clear and consistent. Both parents must enforce thesame rules and it must be done all the time.

For more information-bofya hapa http://www.tutorfi.com/Discipline&ParentingTechniques/lovingparenting
 
AAAAAAAAAAAAAAAAaaaaaaaaaaaaaa
zote ni Imani tupu kuangalia Katuni kuna faida kubwa hasa kwa kukuza kipaji chake
Katuni peke yake ni Tamthilia inayojitosheleza kwani huwa zina Fasihi na Tafsiri nyingi tu
Huyp mtoto anaweza kuwa mchoraji mahiri na akawa bingwa fasihi choraji
Katuni moa t inaweza kuwa na maana ya tafsiri aidi ya 100
 
sawa lakini asiangalie sana abakize na muda wa homework!
 
Dahh hahahaaa umenikumbusha mimi kama miaka miwili iliyopita nilinunua katuni fulani ya katoto keusi sijui ndo Kirikou or something, ya kiswahili yani ile dvd ilikua haipumui inachezwa kuanzia asubuhi mpaka jioni, hamna kuangalia mpira hamna habari hamna chochote na mkitoa ni kilio cha ajabu mpaka muweke. Mbona nilihamisha tv nikadai iko kwa fundi, kama miez miwili hivi hadi akasahau. Iliporudi na ile dvd niliivunja kwa jinsi nilivyokua na hasira. Baada ya hapo ni strict timetable baas. Thenx God ulikua upepo tu ukapita, kumbe tuko wengi? Pole mkuu....
 
sawa lakini asiangalie sana abakize na muda wa homework!
Salama wakuu!
Mimi nina mtoto wa miaka 5 mtoto huyu anapenda sana katuni anaweza kuangalia katuni asubuhi mpaka jioni bila kuchoka

Du miaka 5 unampa Home work
Hata chekechea hawawapi hivyo ngoja afike STD IV au V
mpe katuni za aina nyingi mfano za Lugha ya Kiingereza Boomerang, CT Catoon mbona zinamafunzo mengi na atakuwa mwepesi wa lugha kuliko Comedian za akina Joti
 
Salama wakuu!

Mimi nina mtoto wa miaka 5 mtoto huyu anapenda sana katuni anaweza kuangalia katuni asubuhi mpaka jioni bila kuchoka

Na ikitokea ukizima Tv ni kilio mtindo mmoja mpaka uwashe

Kuhusu shule anasoma chekechea na huwa nikimpaga home work natumia nguvu za ziada sababu ya katuni

Je kuangalia katuni kwa masaa mengi kunaweza kumwadhiri?

Au katuni zinaweza kumjengea uwezo zaidi?

Naombeni kueleweshwa wanajamvi natarajia majibu mazuri kutoka kwenu

Pole sana mkuu. Huyo mtoto wako ni photocopy ya mtoto wangu. Yeye ana miaka 4, anasoma chekechea. Tabia zake ni photocopy ya hizo za mtoto wako. Na bahati mbaya hata TANESCO wakikata umeme, yeye haelewi--ni kilio tu akitaka TV iwashwe aendelee kutazama katuni. Kama ni kuathirika kwa katuni, basi huyu wa kwangu ndiye atakayeathirika zaidi. Tatizo ni kwamba hata umeme ukikatika bado ni shida--dada hawezi kumdhibiti kwani ni mtundu sana. Akikaa kwenye katuni siku nzima inakuwa ni nafuu kwa upande wa kumdhibiti lakini nadhani katuni hizi zitamharibu. Msaada tafadhali wadau. Watoto kama hawa dawa yao ya kuacha ulevi wa katuni ni ipi. Let us share the experience among one another.
 
Natumai ulimaanisha kumuathiri.

Jibu ni ndio, anaweza kuathirika kisaikolojia na hata kimwili kwani anaweza kuiga mambo yanayofanywa na vikatuni akajiumiza au kuumiza wenzake.

Kila kitu kina limit zake. Anza kumbadilishia utaratibu, awe na wakati maalum wa kutazama katuni, nzuri zaidi ni zile zenye kufundisha. Awe na muda wa kusoma, hii unaanza kumzowesha kwa wewe kumsomea vitabu vyenye hadithi za kitoto zenye mafunzo, kumbuka, siyo kumhadithia, kumsomea. Awe na wakati wa kucheza, awe na wakati wa kupumzika.

Nakushauri google "child rearing" utapata kujifunza mengi, kuna kila aina ya mafunzo kuhusu kulea mtoto vyema.

Kama ana bibi, shangazi au ahli zake wako shamba (kijijini) mpeleke akakae nao kwa muda wa miezi miwili au mitatu atabadilika.
Darsa zuri sana hili, litanufaisha wengi.
 
Du miaka 5 unampa Home work
Hata chekechea hawawapi hivyo ngoja afike STD IV au V
mpe katuni za aina nyingi mfano za Lugha ya Kiingereza Boomerang, CT Catoon mbona zinamafunzo mengi na atakuwa mwepesi wa lugha kuliko Comedian za akina Joti

Mkuu, hata hawa wa chekechea nao wana homework zao. Kwa mfano, mwalimu anaweza kugandamizia herufi, halafu akija nyumbani namuelekeza namna ya kugandamizia zile herufi ili kutengeneza herufi halisi au picha. Au wanaweza kupewa homework ya kuandika 1 mpaka 10 au a mpaka u, akija nyumbani unamsaidia kuandika hizo namba. Umeona eeh?
 
Ni tatizo kubwa sana kwa sababu akili yake itakua imeconcentrate sana kwenye katuni. kwa time zote ndani ya kichwa chake anakua anafikiria katuni tu, mwisho akili yake itakua haifanyi kazi kwenye masomo na ataanza kukwambia masomo magumu bado yuko mdogo. Mkataze au weka television chumbani au ifiche rimote

Asante sana mkuu. Ushauri huu nitaufanyia kazi--maana na mwanangu naye amekuwa addicted na katuni.
 
Katuni si kitu kibaya kwa mtoto na tena zinasaidia sana kwa ukuaji wa akili na iq za mtoto. Kinachotakiwa awe na ratiba ya kila kitu afanyacho na kama anapenda katuni wewe kama mzazi shiriki kumchagulia katuni gani aangalie kwani kuna aina nyingine za katuni ni za adults(mfano wa kwangu huwa namkataza kuangalia American Dad kwani ina maudhui ya kikubwa). Mi nina mtoto wa 6yrs na yupo std 1. Nimemuwekea ratiba ya kwenda shule,akirudi analala,akiamka ni kufanya homework zake,akimaliza homework anaenda kucheza na watoto jirani,akimaliza kucheza huwa ni mida ya saa 12 au 1 jioni anatakiwa awe nyumbani jirani na dada lakini bila kuwasha tv. Ikifika mida ya saa 2 kama wakubwa hatujarudi,niliwaruhusu wawashe tv ili waangalie habari. Saa 3:30 kama nimerudi nitawajulia hali na kukagua homework zake la kama sijarudi ni kulala watoto wote pamoja na dada wa kazi. Ni ratiba nzuri kwa huyu wa kwangu kwani toka yupo chekechea hajashika nafasi nje ya tano bora kwenye mitihani ya mid term na annual. Lakini zingatia pia ratiba zitategemea na style ya kuishi ya familia yako.
 
Dahh hahahaaa umenikumbusha mimi kama miaka miwili iliyopita nilinunua katuni fulani ya katoto keusi sijui ndo Kirikou or something, ya kiswahili yani ile dvd ilikua haipumui inachezwa kuanzia asubuhi mpaka jioni, hamna kuangalia mpira hamna habari hamna chochote na mkitoa ni kilio cha ajabu mpaka muweke. Mbona nilihamisha tv nikadai iko kwa fundi, kama miez miwili hivi hadi akasahau. Iliporudi na ile dvd niliivunja kwa jinsi nilivyokua na hasira. Baada ya hapo ni strict timetable baas. Thenx God ulikua upepo tu ukapita, kumbe tuko wengi? Pole mkuu....

Du, kumbe tuko wengi. Ndio. Ile ya kiswahili inaitwa Kirkou. Mtoto wangu hiyo Kirku hana habari nayo tena--ameishaitazama sana. Sasa hivi amehamia kwa nyingine ya kiingereza nasikia wanaiita Ben Ten. Hapo huwezi kumtoa hata ufanye nini. Siku hizi hata kabla ya kwenda shule huweka sharti kwamba aangalie kidogo wakati dada anamuanda kwenda shule, vinginevyo kwenda shule inakuwa mbinde kweli kweli. Na akitoka shule breki ya kwanza ni kwenye Tv. Hakuna cha kuangalia taarifa ya habari wala habari yoyote--ni Ben Ten mtindo mmoja! Wazazi kazi tunayo!
 
Natumai ulimaanisha kumuathiri.

Jibu ni ndio, anaweza kuathirika kisaikolojia na hata kimwili kwani anaweza kuiga mambo yanayofanywa na vikatuni akajiumiza au kuumiza wenzake.

Kila kitu kina limit zake. Anza kumbadilishia utaratibu, awe na wakati maalum wa kutazama katuni, nzuri zaidi ni zile zenye kufundisha. Awe na muda wa kusoma, hii unaanza kumzowesha kwa wewe kumsomea vitabu vyenye hadithi za kitoto zenye mafunzo, kumbuka, siyo kumhadithia, kumsomea. Awe na wakati wa kucheza, awe na wakati wa kupumzika.

Nakushauri google "child rearing" utapata kujifunza mengi, kuna kila aina ya mafunzo kuhusu kulea mtoto vyema.

Kama ana bibi, shangazi au ahli zake wako shamba (kijijini) mpeleke akakae nao kwa muda wa miezi miwili au mitatu atabadilika.
Mimi mwanangu hupendelea kumnunulia katuni ya DORA THE EXPLORER hii inafundisha mambo mengi na huwa inamshirikisha yeye mtoto kujibu maswali na mambo mengi ,katuni kama tom and jerry mi sidhani kama inafundisha....na kuhusu kwamba anangalia katuni sana sio nzuri ...too much is bad
 
Yeah! Dora The Explorer! A very educative cartoon for a child.
Mimi mwanangu hupendelea kumnunulia katuni ya DORA THE EXPLORER hii inafundisha mambo mengi na huwa inamshirikisha yeye mtoto kujibu maswali na mambo mengi ,katuni kama tom and jerry mi sidhani kama inafundisha....na kuhusu kwamba anangalia katuni sana sio nzuri ...too much is bad
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom