Msaada: Mke wangu anajisaidia choo chenye harufu kali

Msaada: Mke wangu anajisaidia choo chenye harufu kali

Awe anapuu kila siku asubuhi, watu wengine wana ka tabia ka kujisaidia mpaka siku tano Hadi Saba zipite, mwambie apuu kila siku, hata Kama hajiskii, ajilazimishe ataona mabadiliko.

Kingine , mkuu Kwan mnashinda wote nyumbani mda wote masaa 24? Huwa anasubiria wewe urudi ndo anapuu au.si apuu ukiwa haupo?

Kingine pia mlango wa chooni kwako mtakuwa mmeacha gap kubwa sana, kwa chini na juu. Mlijenga vibaya tangu mwanzoni. Usimlaumu bure.
 
Basi Kuna dada nafahamiana nae wa kijijji hi hi ulichokitaja ananilalamikia kuona and iko linalomuhusu jf
Kumbe ni kweli na wewe ndo bwanake wa mujini?
Acha basi hizo pigo mazee
 
Mshauri mke wako anywe maji mengi ya kutosha,awe anakunywa na maziwa fresh pia kila siku Ili kuondoa Sumu mwilini.Pendelea kumpa vitu laini laini,na kumtoa outing unachokula wewe na yeye ale.
Hakikisha pia yoghurt zipo ndani
 
Kichwa cha habari hapo juu chajieleza wazi kabisa. Nilienda kuoa mke wangu kijijini kwetu Kafyofyo Kyela kisha tukaja hapa mjini Dar ninapo ishi.

Awali sikuwahi kuishi na mke wangu nyumba moja hadi alipokuja hapa kwangu Dar na ndipo nilipo gundua mengi sana.

Mke wangu akienda msalani kujisaidia haja kubwa hata aki flash bado harufu ile kali haiondoki kwa masaa. Nikajua akikaa hapa Dar akizoea aina hizi za vyakula hali ile itaondoka, lakini ndio inazidi na tumetumia dawa nyingi za tumbo lakini hamna unafuu.

Ombi langu. Je, kuna yeyote hapa ni mtaalam wa afya ya binadamu anaweza tusaidia au kutushauri tufanye nini au twende wapi?

Natanguliza sana shukran zenu na nasubiri msaada wenu

Asante.
inawezekana huko kwenu kafyofyo kuna minyoo sugu sana.
 
Mkuu shukuru sana mods wamekubadirishia Heading Otherwise watu Wangeliona Umekuja Kuwachekesha(kuwatania)

My opinion: Ni Vyema Ukamwambia kuhusu jambo Hilo kama hujamwambia Bado kusudi Muungane wewe na yeye kutafuta Ufumbuzi hili kusudi asione Kunyanyaswa na Kutengwa Mwambie(Mshirikishe) kwa Namna ya Upendo wala Usitumie ukali wala Lugha kali

Naimani atakuelewa na mtalimaliza tatizo kabisa.

Kila lakheri na pole sana mkuu.
 
Mabadiliko ya vyakula, utumiaji wa baadhi ya madawa, Maambukizi utumbo , matatizo kama IBS, IBD, Celiac D, kutokunywa maji ya kutosha, Wala kutokula matunda ,Kansa ya utumbo n.k.. ..

Hata Ivo Harufu mbaya ya kinyesi inayoambata ama na Chooo kua cheupe, au kupungua uzito, au choo kua na Damu , Kuchoka sana ,Homa zisizoisha ..hapo ndo wakati wakuanza kutilia shaka.


Kawaida alipaswa afanye vipimo hiv

1-Stool C&S
2-Feacal Occult blood Test
3-Endoscopy
4-Abdominal X Ray
5-Full Blood Picture


Sasa kutoka kwangu Mimi kabla ya hivo Vipimo waweza msaidia mkeo Kwa kufanya yafuatayo

Mnunulie hizi Dawa na atumie kama nilivyoandika ...

Tab.Ciprofloxacin 500mg every 12 hours for 10 days .

Tab. Metronidazole 400mg every 8 hours for 10 days .

Anywe Maji ya kutosha.
Ale vyakula vya nyuzi nyuzi Kwa wingi.
Ale matunda mfano papai, parachichi, embe .
Aachane na pombe
Kama Kuna madawa anayotumia aweke wazi .
 
MAJI , MAJI, MAJI, MAJI, MAJI, MAJI, MAJI, anywe mengi alafu ale matunda mhimu aende haja kwa wakati pindi anapohisi tu aende
 
Back
Top Bottom