Msaada: Mke wangu anajisaidia choo chenye harufu kali

Msaada: Mke wangu anajisaidia choo chenye harufu kali

Dawa yake ni hii:-
  • Akiamka asubuhi, mpatie supu ya samaki sato mzima yenye mchemsho wa ndizi.​
  • Saa nne asubuhi mpatie matunda mchanganyiko sahani moja iliyojaa​
  • Saa sita mchana mpatie supu ya nusu kuku wa kienyeji, kwa pembeni kukiwa na mboga za majani​
  • Saa saba mpatie glasi mbili za juisi freshi ya matunda mchanganyiko isiyokuwa na embe.​
  • Saa tisa mchana, mpatie kilo moja ya kitimoto rosti na bia nne​
  • Akimaliza kula akapumzike angalau masaa sita​
  • Usiku ale matunda mchanganyiko na mboga za majani​
  • Ale hivi kwa muda wa miezi 2, tatizo litakuwa limeisha​
 
Pole mkuu
Harufu kali ya kinyesi husababishwa na
1. Inawezekana ana minyoo mikali inasababisha kutoa puu kali.
2. Uwepo wa bacteria kwenye colon yake.
3. Inawezekana aina ya vyakula.

Ushauri
1. Nenda hospital apime minyoo. Pia mnaweza kuanza kutumia dawa za minyoo huwa ni kila baada ya miezi mitatu unarudia dozi.

2. Badilini aina ya vyakula. Atumie matunda ma maji mengi.

Kama choo kinanuka sana kuna dalili ya magonjwa.

Pole mkuu.
 
Kwani kamtaja jina?

Kama ndoa ndo kuvumilia hadi hizi kero ambazo zinaweza kuepukika basi ni bora kubakia mseja.
Jina kutaja sio shida. Angalia alivyoandika hio title utaona tu sio mstaarabu..

Mambo kama hayo wanandoa si wanaongea tu na kutibiana, ikishindikana unaandika uzi kwa ile style ya "...Rafiki yangu amenambia ana shida ....(ndo unajaza shida yako).." hio inaonesha utu kdg
 
Kuolewa au kudate na mwanaume wa aina yako ni bora nibaki single niungane na wale wa kataa ndoa kina Mzee wa kupambania
Mbona kawaida tu, yaani bora mtu anayetafuta ufumbuzi kuliko anayekaa na kuumia tu.
Kuna kijana alimuacha mchumba wake kisa kila walipokuwa wanazagamulana dushe lilikuwa linachubuliwa, akawa anahisi mwenzake anakasoro ya kwenye K. Akampiga chini. Alivyoongea na watu wakamwambia binti hana kasoro ila hanyoi vuzi kwenye mashavu. Kumrudia akawa ameshachelewa
 
Kichwa cha habari hapo juu chajieleza wazi kabisa. Nilienda kuoa mke wangu kijijini kwetu Kafyofyo Kyela kisha tukaja hapa mjini Dar ninapo ishi...
Kuna mambo mawili kama uko hapa kupata mawazo na sio utani:

Je anapata choo kila siku?

Kama jibu ni ndiyo basi ndiyo alivyo na tengeneza choo vizuri ili kisirudishe harufu ndani. Nakumbuka kuna fundi aliweka vyombo vibaya hadi sinki la jikoni likawa linatoa harufu. Mara nyingi harufu yako binafsi huisikii sana muulize na yeye kama choo kinanuka wewe ikienda

Pili kama hapati choo kila siku inabidi uanze kwa kiongeza fiber nenda kwenye super market nunua unga wa mbegu za flax seed (mbegu za kitani), mananasi, matunda hasa yenye maganda na maji ya kutosha.

 
Kula matunda! Mboga za majani,epuka vyakula vyenye viungo vingi pia usisahau maji mengi.
 
Back
Top Bottom