Msaada: Mke wangu amekuwa chizi baada ya kutumia PEP

pole, nadhani ni post-traumatic disorder,ni natural mechanism ya kudeal na lililomtokea…….

sijui treatment yake but I guess combination of medication pamoja na ushauri nasaha/therapy vinahitajika
 
Broo kwenye ule uzi wa Deception si ulisema hizi dawa muhimu kwa mtu affected mbona sasa hivi unasema yanashida tena ! !
Sasa mkuu unategemea dawa zisiwe na shida??? sasa kutumia TLE na upate side effects ambazo unaweza kuzivumilia na kusubiri Ngoma ipambe moto kipi bora???
 
Pole sana. PEP inafanyakazi. Hatapata virusi akiitumia vizuri. Hapo kwenye mambo ya ndani naona umekazia sana. Kwani huko ndani huwa mnafanya nini? Epuka kufanya mambo yasiyo ya kawaida uwapo ndani...
Umesababisha nimecheka mnoo mkuu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama wamempa TLE hiyo ni side effect ya efavirenz, wakimbadilishia dawa hiyo kadhia itaisha.
Pole sana mkuu
 
Yatapita Ndugu, vumilia na wasikilize Wataalamu, kila jambo na muda wake.
 
Ni kweli kuna baadhi ya watu hawapatani na Efavirenz na ndiyo sababu kuu ya mauzauza.

Una maana gani unapotaja dawa ya 1r? Tumia majina halisi au vifupisho watu waelewe.

Kama alikuwa anapewa TLE inatakiwa abadilishiwe apewe dawa gani? Duovir N? Mwongozo wa PEP unasemaje?
1r ni tenofovir, lamivudine, dolutegravir,,, inatolewa Kama PEP kwa zile setting zinazotumia TLD kama default first line regimen
 
Huyo amepata shock kutokana na hofu aliyonayo juu ya HIV.Unajua jinsi uwazavyo ikitokea ukapata tension or stress kidogo kiuhalisia lazima ufyetuke.Halafu huyo ni nurse lakini inaonyesha akili,upeo uelewa wake kuhusu huu ugonjwa jinsi ulivyokuwa.Pengine alikuwa anawanyanyapaa hata hao wagonjwa kwa mawazo tu,Sasa kuja kuwaza naye anaupata ndio amepata mshtuko.Atakaa sawa.Hata humu jukwaani utaona comments nyingi zitolewazo kuhusu waathirika ni za kinyanyapaa(ukisoma uzi za huu ugonjwa utathibitisha Hilo).Mtu mwenye mentality hiyo ikitokea kivyovyote apate ama ahisi Ana huu ugonjwa,nakuhakikishia lazima achizi.
Mkuu bila Shaka wewe ni miongoni mwa wenye jangwa wa ugonjwa hili ,coz umeshakimbilia unyanyapaa bila kujua hata huyo mhushika alikuwa anatekelezaje majukumu yake. Jambo la kawaida kupatwa na hili ugonjwa lkn sio kutupia mwenzio lawama ya unyanyapaa
 
Huyo amepata shock kutokana na hofu aliyonayo juu ya HIV.Unajua jinsi uwazavyo ikitokea ukapata tension or stress kidogo kiuhalisia lazima ufyetuke.Halafu huyo ni nurse lakini inaonyesha akili,upeo uelewa wake kuhusu huu ugonjwa jinsi ulivyokuwa.Pengine alikuwa anawanyanyapaa hata hao wagonjwa kwa mawazo tu,Sasa kuja kuwaza naye anaupata ndio amepata mshtuko.Atakaa sawa.Hata humu jukwaani utaona comments nyingi zitolewazo kuhusu waathirika ni za kinyanyapaa(ukisoma uzi za huu ugonjwa utathibitisha Hilo).Mtu mwenye mentality hiyo ikitokea kivyovyote apate ama ahisi Ana huu ugonjwa,nakuhakikishia lazima achizi.
Wacha madaktari wafanye kazi yao. Wewe piga magoti mlilie Mungu. Yeye ndiye pekee anayeponya.

Pole sana Mkuu.
Kwa hiyo saa hivi mke wako ni mwadhirika..
Pole sana mkubwa..
Kuna baadhi ya maswali yanapaswa yajibiwe kwa mikorongoko au unywerenywete bila kusahau yunguluku.
 
Daah Efavirenz hiyo inafanya kazi...itaisha wala usijali...pole sana lakini
 
Habari za asubuhi ndugu zanguni? leo siku ya pili sijalala ni purukushani mtindo mmoja.
Hipo hivi wife ni muhudumu wa afya sasa juzi kwa bahati mbaya akaji choma na sindano ya mtu alipata maambukizo ya virusi vya HIV.Ikabidi apewe dawa PEP kuzuia maambukiza kwake, alianza jioni kutumia hizi dawa' baada ya masaa 4 balaa likaanza nikapigiwa simu kuwa wife ameweuka anakimbia ovyo barabarani anaropoka kila kitu hadi siri zetu za ndani..ikabidi wamkamate wampeleke hospital wakamchoma valium , nilivyotoka job nikapitia hospital moja kwa moja mpka kwa daktari nimeongea bna daktari amesema hiyo ni kawaida kwa ARV hizo ni side effects zake akiamka atakuwa yupo poa.Baadae akaamka yaani ndio balaa likapamba moto fujo, matusi anaropoka vya ndani hadi aibu.
leo siku ya pili bado hali yake ipo hivyo hivyo hakuna mabadiliko yoyote...kibaya zaidi ana mtoto wa miezi 5
NB:kwao hakuna history ya magonjwa ya akili.
Naombeni msaada kwa ili maana nimechanganyikiwa hapa
@skyeclat Deception Suriya na wengineo
Mkuu vip Hali ya mkeo hadi sasa inaendeleaje
 
Pole sana mkuu. Wasiliana na walipomwazishia TLE kama wameanza kutoa TLD wampe hayo ni maudhi ya Efavirenz
 
Pole, inaelekea nawe umechanganyikiwa kiasi hata unashindwa kutueleza yuko hosipitali gani ili tuweze kujua kama anapatiwa huduma stahiki au la.
Unaposema anakimbia mitaani napata picha yupo zahanati za mitaani ambapo anafanyia kazi, mpeleke hosipitali JF siyo hosipitali sahihi kwa kwenye matatizo ya akili kwani nako kumelemewa wenye matatizo hayo.
Hakukosea kuandika hapa Gf...kupeana mawazo ni muhimu pia..afu hapa anajua wengi wao wako vizuri tofauti na kule facebook mnakolinganisha na hapa!
 
Kama mkuu Deception atakuja kutia neno lolote hapa basi naomba tushituane!

Ndio maana siku zote huwa nawaambia watu kwamba wasikimbilie kubisha pale wanaposikia jambo geni,bali wanatakiwa kuwa wanyenyekevu na wasikivu,kisha wahoji namkudadisi,hizi ndio taratibu nzuri zitakazofanya watu wapate maarifa ambayo pengine yatawasaidia sana katika maisha yao;

Sustiva kwa mfano,ambayo ndani yake kuna efavirenz,huwa inasababisha matatizo ya akili kwa watumiaji wengi sana,lakini watu wakipata matatizo ya akili basi inachukuliwa kama ni dalili au matokeo ya HIV,wanamsingizia bure HIV.

Huko Afrika kusini mateja wanatumia hizi ARVs kama street drugs kama ilivyo cocaine au heroin na wanapata ladha/effect kama ile wanayoipata watumiapo heroin au cocaine....sasa unganisha dots hapo;

Someni hizi link hapo chini;

madhara ya efavirenz;

watu wasije kusema hawajaambiwa.
 
Habari za asubuhi ndugu zanguni? leo siku ya pili sijalala ni purukushani mtindo mmoja.
Hipo hivi wife ni muhudumu wa afya sasa juzi kwa bahati mbaya akaji choma na sindano ya mtu alipata maambukizo ya virusi vya HIV.Ikabidi apewe dawa PEP kuzuia maambukiza kwake, alianza jioni kutumia hizi dawa' baada ya masaa 4 balaa likaanza nikapigiwa simu kuwa wife ameweuka anakimbia ovyo barabarani anaropoka kila kitu hadi siri zetu za ndani..ikabidi wamkamate wampeleke hospital wakamchoma valium , nilivyotoka job nikapitia hospital moja kwa moja mpka kwa daktari nimeongea bna daktari amesema hiyo ni kawaida kwa ARV hizo ni side effects zake akiamka atakuwa yupo poa.Baadae akaamka yaani ndio balaa likapamba moto fujo, matusi anaropoka vya ndani hadi aibu.
leo siku ya pili bado hali yake ipo hivyo hivyo hakuna mabadiliko yoyote...kibaya zaidi ana mtoto wa miezi 5
NB:kwao hakuna history ya magonjwa ya akili.
Naombeni msaada kwa ili maana nimechanganyikiwa hapa
@skyeclat Deception Suriya na wengineo
Daa pole sana ndugu huo ni moja ya mtihani
 
Ndio maana siku zote huwa nawaambia watu kwamba wasikimbilie kubisha pale wanaposikia jambo geni,bali wanatakiwa kuwa wanyenyekevu na wasikivu,kisha wahoji namkudadisi,hizi ndio taratibu nzuri zitakazofanya watu wapate maarifa ambayo pengine yatawasaidia sana katika maisha yao;

Sustiva kwa mfano,ambayo ndani yake kuna efavirenz,huwa inasababisha matatizo ya akili kwa watumiaji wengi sana,lakini watu wakipata matatizo ya akili basi inachukuliwa kama ni dalili au matokeo ya HIV,wanamsingizia bure HIV.

Huko Afrika kusini mateja wanatumia hizi ARVs kama street drugs kama ilivyo cocaine au heroin na wanapata ladha/effect kama ile wanayoipata watumiapo heroin au cocaine....sasa unganisha dots hapo;

Someni hizi link hapo chini;

madhara ya efavirenz;

watu wasije kusema hawajaambiwa.
Deception is Beck
 
Back
Top Bottom