Msaada: Mke wangu amekuwa chizi baada ya kutumia PEP

Msaada: Mke wangu amekuwa chizi baada ya kutumia PEP

Habari za asubuhi ndugu zanguni? leo siku ya pili sijalala ni purukushani mtindo mmoja.
Hipo hivi wife ni muhudumu wa afya sasa juzi kwa bahati mbaya akaji choma na sindano ya mtu alipata maambukizo ya virusi vya HIV.Ikabidi apewe dawa PEP kuzuia maambukiza kwake, alianza jioni kutumia hizi dawa' baada ya masaa 4 balaa likaanza nikapigiwa simu kuwa wife ameweuka anakimbia ovyo barabarani anaropoka kila kitu hadi siri zetu za ndani..ikabidi wamkamate wampeleke hospital wakamchoma valium , nilivyotoka job nikapitia hospital moja kwa moja mpka kwa daktari nimeongea bna daktari amesema hiyo ni kawaida kwa ARV hizo ni side effects zake akiamka atakuwa yupo poa.Baadae akaamka yaani ndio balaa likapamba moto fujo, matusi anaropoka vya ndani hadi aibu.
leo siku ya pili bado hali yake ipo hivyo hivyo hakuna mabadiliko yoyote...kibaya zaidi ana mtoto wa miezi 5
NB:kwao hakuna history ya magonjwa ya akili.
Naombeni msaada kwa ili maana nimechanganyikiwa hapa
@skyeclat Deception Suriya na wengineo
Pole, inaelekea nawe umechanganyikiwa kiasi hata unashindwa kutueleza yuko hosipitali gani ili tuweze kujua kama anapatiwa huduma stahiki au la.
Unaposema anakimbia mitaani napata picha yupo zahanati za mitaani ambapo anafanyia kazi, mpeleke hosipitali JF siyo hosipitali sahihi kwa kwenye matatizo ya akili kwani nako kumelemewa wenye matatizo hayo.
 
huu ni ujinga,badala ya kushauri walau atafutiwe psychologist unashauri apelekwe kwa matapeli wenzio,umeona hayo ni mapepo au ni psychological case??acha uzwazwa,
Mkuu.

Tuheshimiane katika kutoa mawazo, simply nimesema hii case naijua na zimetokea nyingi.

Iko hivi, sio kila mtu akienda kwenye maombi anaombewa mapepo wengine wanaombewa Rehema na Neema. Baada ya kuomba Rehema kwa Mungu basi Ushauri kwa huyu mtu inakua rahisi.

Wa kristu tunaamini kuwa Giza havichangamani na Nuru, hivyo basi, kama tunataka asaidiwe tunaomba Rehema na Neema kisha ushauri unafuata.

Natamani niseme zaidi lakini kwa uchache ni hayo.
 
Kwanza maambukizi hajapata kwa kuwa aliwahi kuchomwa hiyo sindano ya PEP.


PILI, Jaribu kumbadilishia Daktari .


Tatu omba ruhusa KAZINI au Likizo ushughurike naye kiukamilifu.Wewe ndiye mwenye KUJUA umuhimu wake kwako na kwa Watoto wako hasa huyo mdogo kabisa .


MBADILISHIE HOSPITAL/ DAKTARI. AU UMPELEKE CLINIC YA MAGONJWA YA AKILI KWA MSAADA ZAIDI NA VIPIMO ZAIDI.

POLE SANA MUNGU AKUIMARISHE
 
Wambadilishie dawa mbona simple tu
Habari za asubuhi ndugu zanguni? leo siku ya pili sijalala ni purukushani mtindo mmoja.
Hipo hivi wife ni muhudumu wa afya sasa juzi kwa bahati mbaya akaji choma na sindano ya mtu alipata maambukizo ya virusi vya HIV.Ikabidi apewe dawa PEP kuzuia maambukiza kwake, alianza jioni kutumia hizi dawa' baada ya masaa 4 balaa likaanza nikapigiwa simu kuwa wife ameweuka anakimbia ovyo barabarani anaropoka kila kitu hadi siri zetu za ndani..ikabidi wamkamate wampeleke hospital wakamchoma valium , nilivyotoka job nikapitia hospital moja kwa moja mpka kwa daktari nimeongea bna daktari amesema hiyo ni kawaida kwa ARV hizo ni side effects zake akiamka atakuwa yupo poa.Baadae akaamka yaani ndio balaa likapamba moto fujo, matusi anaropoka vya ndani hadi aibu.
leo siku ya pili bado hali yake ipo hivyo hivyo hakuna mabadiliko yoyote...kibaya zaidi ana mtoto wa miezi 5
NB:kwao hakuna history ya magonjwa ya akili.
Naombeni msaada kwa ili maana nimechanganyikiwa hapa
@skyeclat Deception Suriya na wengineo
 
Pole sana. PEP inafanyakazi. Hatapata virusi akiitumia vizuri. Hapo kwenye mambo ya ndani naona umekazia sana. Kwani huko ndani huwa mnafanya nini? Epuka kufanya mambo yasiyo ya kawaida uwapo ndani...
 
kama walimpa PEP ya 1g wajaribu kumbadilishia wampe 1r huenda efavirenz ndo inaleta madudu hayo?
Ni kweli kuna baadhi ya watu hawapatani na Efavirenz na ndiyo sababu kuu ya mauzauza.

Una maana gani unapotaja dawa ya 1r? Tumia majina halisi au vifupisho watu waelewe.

Kama alikuwa anapewa TLE inatakiwa abadilishiwe apewe dawa gani? Duovir N? Mwongozo wa PEP unasemaje?
 
Back
Top Bottom