Msaada: Mke wangu amekuwa chizi baada ya kutumia PEP

Msaada: Mke wangu amekuwa chizi baada ya kutumia PEP

Huyo amepata shock kutokana na hofu aliyonayo juu ya HIV.Unajua jinsi uwazavyo ikitokea ukapata tension or stress kidogo kiuhalisia lazima ufyetuke.Halafu huyo ni nurse lakini inaonyesha akili,upeo uelewa wake kuhusu huu ugonjwa jinsi ulivyokuwa.Pengine alikuwa anawanyanyapaa hata hao wagonjwa kwa mawazo tu,Sasa kuja kuwaza naye anaupata ndio amepata mshtuko.Atakaa sawa.Hata humu jukwaani utaona comments nyingi zitolewazo kuhusu waathirika ni za kinyanyapaa(ukisoma uzi za huu ugonjwa utathibitisha Hilo).Mtu mwenye mentality hiyo ikitokea kivyovyote apate ama ahisi Ana huu ugonjwa,nakuhakikishia lazima achizi.
You stole my thoughts. Tatizo watu wanawaza sana kuhusu maisha ya UKIMWI. Take it simple na utaishi kwa raha. Mbona watu tunajipima kila siku bila woga.
 
Habari za asubuhi ndugu zanguni? leo siku ya pili sijalala ni purukushani mtindo mmoja.
Hipo hivi wife ni muhudumu wa afya sasa juzi kwa bahati mbaya akaji choma na sindano ya mtu alipata maambukizo ya virusi vya HIV.Ikabidi apewe dawa PEP kuzuia maambukiza kwake, alianza jioni kutumia hizi dawa' baada ya masaa 4 balaa likaanza nikapigiwa simu kuwa wife ameweuka anakimbia ovyo barabarani anaropoka kila kitu hadi siri zetu za ndani..ikabidi wamkamate wampeleke hospital wakamchoma valium , nilivyotoka job nikapitia hospital moja kwa moja mpka kwa daktari nimeongea bna daktari amesema hiyo ni kawaida kwa ARV hizo ni side effects zake akiamka atakuwa yupo poa.Baadae akaamka yaani ndio balaa likapamba moto fujo, matusi anaropoka vya ndani hadi aibu.
leo siku ya pili bado hali yake ipo hivyo hivyo hakuna mabadiliko yoyote...kibaya zaidi ana mtoto wa miezi 5
NB:kwao hakuna history ya magonjwa ya akili.
Naombeni msaada kwa ili maana nimechanganyikiwa hapa
@skyeclat Deception Suriya na wengineo
Daah eh bana ee pole sana mkuu hzo dawa ni shida sio wote wanaotumia huwa zinawakubali
 
Pole sana...

Mawazo ya kwamba alijidunga sindano yenye Virusi kwa bahati mbaya ndiyo yanayompelekea huo uchizi, hakuna kingine...

Pale atakapogundua hajaathiriwa na chochote atarudi kawaida...


Cc: mahondaw
 
You stole my thoughts. Tatizo watu wanawaza sana kuhusu maisha ya UKIMWI. Take it simple na utaishi kwa raha. Mbona watu tunajipima kila siku bila woga.
Hili ndilo lililomkumba,ampeleke hospital private,apewe bedrest,apumzike vya kutosha,baada ya wiki atakuwa mzima wa afya .
 
Kwakweli hawa wauguzi wana kazi ngumu serikali iendelee kuwajali kwa kuwapa maslahi mazuri story hii ukitafakari inaumiza sana
 
Sijui nicoment nini!!pole mkuu😢😢.ila nmeona umemtag Deception,nahis 75% anaweza kukusaidia!
 
Pole sana aisee. side effect ya efavirenz hyo.abadilishiwe regimen
 
Duuh nnkakupa pole sana mkuu, hizo dawa kwa story zake ni hatari zinaleta mawenge balaa, cha msingi amalize dozi kwanza
 
Hapo suala la Mwanae ndo limemfanya awaze mpaka afike levele ya juu kabisa akili zikawa kama zimemruka anawaza sanaa...!! Japo hayo madawa pia yanashida sanaa
Broo kwenye ule uzi wa Deception si ulisema hizi dawa muhimu kwa mtu affected mbona sasa hivi unasema yanashida tena ! !
 
Mkuu kama una amini katika maombi fanya haraka kumpeleka huko huku unasubiri msaada wa pili wa madaktari.

Hiyo kesi naielewa sana, practice maombi kwanza.
Asitumie PEP aende kuombewa na nabii gwaji boy si ndio , halafu atapona sieti eh Mtoto mzuri
 
Usije ikakuta huko ndani unaruka ukuta mkuu hahaha nataniatu mkuu
Pole sana. PEP inafanyakazi. Hatapata virusi akiitumia vizuri. Hapo kwenye mambo ya ndani naona umekazia sana. Kwani huko ndani huwa mnafanya nini? Epuka kufanya mambo yasiyo ya kawaida uwapo ndani...
 
Back
Top Bottom