PROF NDUMILAKUWILI
JF-Expert Member
- Mar 25, 2016
- 10,516
- 13,269
Ndugu usipotoshe watu,eti "hakuna HIV"Hakuna HIV,Ukimwi si ugonjwa,ukimwi,hauui bali kinachoua ni ugonjwa unaoingia baada ya kuwa na ukimwi,ukimwi hautishi kama ulivyoaminishwa bali ukimwi huja na kuondoka mwilini kulingana na aina ya maisha unayoishi,ukimwi hausababishwi na HIV kwakua hakuna kijidudu chochote chenye uwezo wa kusababisha ukimwi duniani.
Hitimisho:
Aachane na hizo sumu anazokula atapona tatizo lake.
Mimi sio mtaalumu wa afya lakini kwa macho yangu nimeshuhudia watu wengi katika jamii nayo kaa nayo pamoja na kuwa wako vizuri kiuchumi na kuishi mtindo mzuri wa maisha lakini kuna kipindi afya zao zilipolomoka vibaya sana tena sana wamepelekwa katika vituo vya afya na wakagundulika wana HIV, kwa miaka ya nyuma nimeshuhudi watu wenye hili tatizo walikuwa hawana la kufanya japo wana hari nzuri kimaisha lakini walikuwa wanapigwa na magonjwa ya hapa na pale wanapata dawa zinazohusiana na hilo tatizo lakini wapi afya inadidimia hadi wanakufa.Miaka ya sasa hivi wote tunaona watu wa afya hawalali wanapigania hili na hauweni tunaiona jamii kubwa ambayo ni wahanga wa hili tatizo tunaona afya zao zinaimalika vizuri kwa matumizi ya arvs na wanaendelea na kazi zao.
Usipotoshe watu kwa jambo linaloonekana wazi.