Msaada: Mifuko ya simenti mingapi hutumika katika matofali ya kulaza?

nzalendo

JF-Expert Member
May 26, 2009
11,742
12,035
Salaam watu wa JF,

Naomba msaada ili niweze kusuluhisha kesi kati ya fundi na jamaa yangu.
Ningependa kufahamu ni mifuko mingapi ya Cement yatumika kwenye tofali za kulala.Wastani wa tofali (950.+ -)

Natanguliza shukurani.
 
Salaam watu wa jf
Naomba msaada ili niweze kusuluhisha kesi kati ya fundi na jamaa yangu.
Ningependa kufahamu ni mifuko mingapi ya Cement yatumika kwenye tofali za kulala.Wastani wa tofali (950.+ -)
Natanguliza kumshukuruni.

Wastani mfuko mmoja ni tofali 40-45
Hivo 950/45~ mifuko 22
ila simamia wakichanganya maana wanaeza kukuekea mfuko mmoja tofali 60, ukawa umepigwa mifuko 7)
 
Unajua inategea mfuko mmoja ni tofari 35-40. Tukichukulia maximum tofari 40 tunaweza sema mifuko 24.
 
Tofali aina gani, block brick; je matofali ya udongo au sement;...ukitoa majibu ya maswali haya utapata majibu sahihi kabisa...na huo ugomvi utauamua bila upendeleo.
Maswali yangu yanalenga kwa kufundi anayejenga ukuta. kama ni fundi wa kufyatua matofali kipengele cha swali la je matofali ya udongo ama sement hakina maana. jibu kipengele kingine.
 
Hizi ni tofali za kulaza au za kusimamisha?
 
Wastani mfuko mmoja ni tofali 40-45
Hivo 950/45~ mifuko 22
ila simamia wakichanganya maana wanaeza kukuekea mfuko mmoja tofali 60, ukawa umepigwa mifuko 7)
Shukran sana
Hapan shaka ni tofali za kulaza
 
Tofali aina gani, block brick; je matofali ya udongo au sement;...ukitoa majibu ya maswali haya utapata majibu sahihi kabisa...na huo ugomvi utauamua bila upendeleo.
Maswali yangu yanalenga kwa kufundi anayejenga ukuta. kama ni fundi wa kufyatua matofali kipengele cha swali la je matofali ya udongo ama sement hakina maana. jibu kipengele kingine.
NI matofali haya ya kawaida ya mchanga na sementi yanayouzwa mitaani mwetu...
Lakini yamejengwa kwa kulala msingi.
 
Salaam watu wa jf
Naomba msaada ili niweze kusuluhisha kesi kati ya fundi na jamaa yangu.
Ningependa kufahamu ni mifuko mingapi ya Cement yatumika kwenye tofali za kulala.Wastani wa tofali (950.+ -)
Natanguliza kumshukuruni.
Kwa shule niliyofundishwa mimi na uzoefu wa miaka 22 kazini, tofali za kulala huwa ni 6o kwa mfuko na tofali za kusimamisha huwa ni 70. hiyo ndio standard nzuri zaidi ya hapo majanga!
 
Unajua inategea mfuko mmoja ni tofari 35-40. Tukichukulia maximum tofari 40 tunaweza sema mifuko 24.
Mkuu ni kujengea
yaani tofali tayari lipo
halafu
unalijenga kwa kulilaza je:
mifuko mingapi itagharimu?
 
Kwa shule niliyofundishwa mimi na uzoefu wa miaka 22 kazini, tofali za kulala huwa ni 6o kwa mfuko na tofali za kusimamisha huwa ni 70. hiyo ndio standard nzuri zaidi ya hapo majanga!
Duh. Labda mimi sijaelewa anaongelea nini. Lakini kama hizi tofari zetu za cement na mchanga matofari 60 kwa mfuko ni mengi sana.
 
NI matofali haya ya kawaida ya mchanga na sementi yanayouzwa mitaani mwetu...
Lakini yamejengwa kwa kulala msingi.
Kama ni nchi sita ni matofali 50 kwa mfuko mmoja, kwa hiyo kwa idadi ya 950+ ni karibu mifuko 19 ya sementi
 
Huyu mtu tayari ana matofali yake, anachotaka kujua ni mfuko mmoja atajengea tofali ngapi za msingi.

Hivyo hapo ni ile ratio ya mfuko mmoja kwa ndoo ngapi za mchanga? na hiyo idadi ya ndoo za mchanga je atatumia mifuko mingapi ya Cement kujengea msingi wake ambao utakula kama tofali 950.

ndio nilivyomuelewa.
 
Mada zako huwa ni za ki -maendeleo sana bigup.... watu wakikaa kujadili wanaongeza ufahamu wa maendeleo
 
Back
Top Bottom