Msaada: Mgogoro best yangu na mke wake

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
Kuna best angu kaniomba ushauri nimeshindwa kumsaidia. Ipo hivi leo mida ya mchana alimchukua wife wake kutoka home akamshusha kituo cha mwendo kasi. akampatia tsh 90,000 kwamba aende kariakoo yy na watoto wake wawili akawafanyie shopping ya sikukuu.

Masaa kadhaa yakapita. Jamaa akasema ngoja ampigie kuona kama alifanikiwa. Simu ikawa haipatikani. Akajaribu baada ya few hours bado tena haipatikani akahisi kuna kitu hakipo sawa. Baada alivyorudi home akamkuta wife wake yupo home. Kumuuliza akamjibu very simple kuwa kaibiwa vitu vyote kariakoo simu pamoja na hela.

Jamaa alivyoanza kuhoji zaidi akaishia kuambiwa kama kupotea vimeshapotea kwa saut isiyoonyesha kuhudhunika wala nn. Ikumbukwe hela pamoja na hiyo simu vyote alipewa na huyu jamaa yangu.

Sasa jamaa yangu kamaindi kwamba haonyeshi kujutia vile hajanunua yy na hela zile ni za kupewa tu. Jamaa kakasirika sana na kaniomba ushauri. Wakuu hii imekaaje? Ni hatua gani anaweza kuchukua?
 
akae kimya asimuulize tena chochote kuhusu hayo....
navyoona hapo hata mke pia amekua frustrated pengine kuliko yeye mwenyew anavyojiona kawa frustrated sema asichukulie hasira amuache tu Kwanza ....then akicool down watayaongea Kwa uzuri...

ashughulikie suala la ubwabwa na mengineyo muda umeisha ni wiki ijayo tu hapa mkuu..
 
Jamaa yako ni aina ya jon alcohol

Aina ya wanaume ambao mpaka mwanamke atoe chozi la damu ndo ajue kaumia

Alafu elfu 90,000 ?? Kariakoo, msimu huu wa sikukuuu ??

Mie naona dem katumia akili tu, ili jamaa ampe hela ingine ,arudi sasa akaongezee ya awali anunue.
 
Ushauri:
Ampe pole mke wake huku akimshukuru MUNGU kuwa yupo salama, asiache kumuuliza mara mbili mbili kama hajadhurika.

Akaripoti polisi kuwa kaibiwa na achukue loss report.

Aangalie utaratibu gani mbadala wa mawasiliano maana mama anayetunza watoto hana simu na mawasiliano baina yao ni muhimu.
 
Ninavyojua mimi ukiishi na mwenza wako kwa muda unakuwa na uwezo wa kumsoma kama kitabu na kumuelewa unless uwe siyo mdadisi. Ukishamzoea mtu una uwezo wa kusoma body language na vitu kama sauti kujua hisia zake na mambo mengine mengi tu. Je, kilichomfanya aseme hivyo ni kuwa ameji-behave tofauti na anavyofanya siku nyingine anapokuwa amepatwa na jambo baya kama kuibiwa?

Ushauri: njia ya mwongo ni fupi. Ajipe muda. Aendelee na maisha na kuna siku atakuja kujua ukweli. Siku zote kwenye ndoa unapohisi mwenzako anafanya mambo ya siri wala usiwe na haraka. Jifanye kama wewe ni mjinga na hujui kinachoendelea lakini kwa siri uwe unamfuatilia.
 
Kuna best angu kaniomba ushauri nimeshindwa kumsaidia. Ipo hivi leo mida ya mchana alimchukua wife wake kutoka home akamshusha kituo cha mwendo kasi. akampatia tsh 90,000 kwamba aende kariakoo yy na watoto wake wawili akawafanyie shopping ya sikukuu. Masaa kadhaa yakapita. Jamaa akasema ngoja ampigie kuona kama alifanikiwa. Simu ikawa haipatikani. Akajaribu baada ya few hours bado tena haipatikani akahisi kuna kitu hakipo sawa. Baada alivyorudi home akamkuta wife wake yupo home. Kumuuliza akamjibu very simple kuwa kaibiwa vitu vyote kariakoo simu pamoja na hela. Jamaa alivyoanza kuhoji zaidi akaishia kuambiwa kama kupotea vimeshapotea kwa saut isiyoonyesha kuhudhunika wala nn. Ikumbukwe hela pamoja na hiyo simu vyote alipewa na huyu jamaa yangu. Sasa jamaa yangu kamaindi kwamba haonyeshi kujutia vile hajanunua yy na hela zile ni za kupewa tu. Jamaa kakasirika sana na kaniomba ushauri. Wakuu hii imekaaje? Ni hatua gani anaweza kuchukua?
Hivi 90,000 shopping ya mke na watoto wawili ananunua nini? Maana suti tu zile za bei chee ni 75,000, gauni la bei chee la mtoto ni 55,000 na nguo ya mke nadhani nguo ya maana si chini ya 80,000

Wanaume tujitahidi tusiwatie hasira hawa wake zetu, kama hali hairuhusu basi mzungumze muelewane kwanza lakini kwa hali halisi 90,000 kwa msimu huu wa sikukuu haiwezi nunua kitu
 
Jamaa yako ni aina ya jon alcohol

Aina ya wanaume ambao mpaka mwanamke atoe chozi la damu ndo ajue kaumia

Alafu elfu 90,000 ?? Kariakoo, msimu huu wa sikukuuu ??

Mie naona dem katumia akili tu, ili jamaa ampe hela ingine ,arudi sasa akaongezee ya awali anunue.
Hapa naungana na wee kabisaa
 
Back
Top Bottom