Msaada, Mgao Wa Mali Endapo Wanandoa Wametalakiana?

Langu

Member
Nov 20, 2011
37
0
Habari za asubuhi ndugu wana JF, Nawasalimu katika jina la bwana mungu wetu.

Nimekua nikisikia kuwa kisheria wanandoa wakitalikiana, wanaweza wakagawana mali walizovuna wakiwa pamoja, sijui hii maana ni sahii au nakosea naomba nirekebishwe.

Maswali yangu yanakuja hivi;


  • Je, ni mali gani mahakama inaweza kusema hii imevunwa kwa pamoja?
  • Mfano, mimi endapo ni mama wa nyumbani tu sina kazi, naweza kupata chochote kwa hicho kigezo cha kuvunwa kwa pamoja?
  • Je,mali nilizokuta tayari anazo mme au mke, zinaweza zikawa sehemu ya mgawanyo, na kwa misingi hipi ikawa hivyo?

Nitashukuru kwa michango yenu wapendwa.

Be blessed.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Anaeweza kusema ni huyo atakae kurithi. Si anajuwa zipi walichuma pamoja, zipi alimkuta nazo mwenza wake.
 

tama

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
603
195
Mama wa nyumbani pliz ebu acha hiyo kauli kwani wew ulivyokuwa unabika nyumbani ulikuwa hupiki?hufui nguo?na n.k,zile malizo zote mlizochuma nae kipindi cha ndoa yenu mnagawana nusu kwa nusu.
 

Langu

Member
Nov 20, 2011
37
0
Anaeweza kusema ni huyo atakae kurithi. Si anajuwa zipi walichuma pamoja, zipi alimkuta nazo mwenza wake.

Inakuja swala kwamba kila mmoja anabisha kuwa ni mali yake, ndo tatizo linaanzia hapo

Mama wa nyumbani pliz ebu acha hiyo kauli kwani wew ulivyokuwa unabika nyumbani ulikuwa hupiki?hufui nguo?na n.k,zile malizo zote mlizochuma nae kipindi cha ndoa yenu mnagawana nusu kwa nusu.

Kumbe na kazi za nyumbani inaweza ikaamount mwanamke apate mgao?
 

nameless girl

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
4,150
2,000
Kuhusu mgao wa mali wa wanandoa, mahakama itaangalia zile ambazo mlianza kuzipata mara tu mlipokuwa pamoja. Mfano ulimkuta mumeo amepanga, mkaanza kujenga pamoja, haijalishi kama ulikua mama wa nyumbani tu, kila ulichokifanya, kilimsupport yeye kufanya kazi na kujenga, hivyo mlijenga wote. Ila kama ulimkuta na hiyo nyumba, hupaswi kuihesabia...
 

Langu

Member
Nov 20, 2011
37
0
Vipi kama mali mlinunua wote wawili, then jina la hiyo mali imeandikwa jina la mmoja wapo,

Na huyo mwenye jina kwenye mali anakatalia kuwa ni yake tu, hapo mambo yanakaaje?


cc: nameless girl, cc: tama
 
Last edited by a moderator:

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,711
2,000
Mama wa nyumbani pliz ebu acha hiyo kauli kwani wew ulivyokuwa unabika nyumbani ulikuwa hupiki?hufui nguo?na n.k,zile malizo zote mlizochuma nae kipindi cha ndoa yenu mnagawana nusu kwa nusu.

Hembu twende kisheria basi, hayo mambo ya nusu kwa nusu mi sijayasikia popote.
 

Asnam

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
4,258
1,225
Hembu twende kisheria basi, hayo mambo ya nusu kwa nusu mi sijayasikia popote.

suala la nusu kwa nusu huja endapo mmechuma mali pamoja,haijalishi mlichangia pesa,nguvu au mawazo ktk kuzipata Mali hizo.Yawezekana hujasikia kwa sababu hufuatilii sheria za ndoa zinasemaje maana hapa nchini kila mmoja anadhaniwa anaijua sheria,hivyo una wajibu wa kuzitafuta na kuzisoma
 

Langu

Member
Nov 20, 2011
37
0
cc: Mphamvu

Umeona eeh ndugu yangu, inapendeza kidogo ukiargue kisheria.

cc: Asnam

Your welcome mkuu
 
Last edited by a moderator:

Asnam

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
4,258
1,225
jina sio kipimo cha umiliki wa mali ktk ndoa,labda kama jina ni la mtoto/ watoto lakini kama jina ni la mke/ mume na hiyo mali mmeipata wakati wa ndoa basi mtagawanywa nusu kwa nusu.Ingawa kuna vigezo na masharti ya kuzingatia kabla ya mgawanyo
 

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,711
2,000
suala la nusu kwa nusu huja endapo mmechuma mali pamoja,haijalishi mlichangia pesa,nguvu au mawazo ktk kuzipata Mali hizo.Yawezekana hujasikia kwa sababu hufuatilii sheria za ndoa zinasemaje maana hapa nchini kila mmoja anadhaniwa anaijua sheria,hivyo una wajibu wa kuzitafuta na kuzisoma

Sheria sijaipitia, lakini nimepata kusikia kesi kadhaa za ndoa mahakamani. Ambazo nadhani hukumu zake ziliegama kwenye sheria, sio?
 

Asnam

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
4,258
1,225
Sheria sijaipitia, lakini nimepata kusikia kesi kadhaa za ndoa mahakamani. Ambazo nadhani hukumu zake ziliegama kwenye sheria, sio?

uko sahihi,mnapofika mahakamani sheria ndo muamuzi wenu.
 

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,711
2,000
uko sahihi,mnapofika mahakamani sheria ndo muamuzi wenu.

Kuna kesi moja maarufu sana ya miaka ya themanini (hata wanafunzi wa sheria huwa wanairejelea) ilikuwa ya talaka. Huyo mama mdai na mwanasheria wake wakaja na hoja kuwa kuchuma mali si lazima iwe wote mfanye kazi au biashara, hata mchango wa mama katika kulea watoto, kupika, na kulitunza jitu zima pia unahesabika ingawa hauhitimishi mgao wa nusu kwa nusu.
Ile kesi ilikatiwa rufaa hadi mahakama kuu, na ndio ikawa chanzo cha marekebisho ya sasa kwenye sheria ambayo yanatambua mchango wa mama wa nyumbani katika kuchuma mtonyo.
Maelezo yangu hayana data mahususi kwa kuwa nilisimuliwa na jamaa wangu anayesomea sheria.
 

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,711
2,000
Kama sijakosea ni kesi ya Bi Hawa mdau

cc: Mphamvu


BI. HAWA MOHAMED v. ALLY SEIF [1983] TLR 32

Ni hukumu muhimu na maarufu kuliko zote pale linapokuja suala la migogoro ya wana-ndoa wanaotaka kutalikiana na pia suala zima la ugawanaji mali pale mahakama inaporidha talaka itolewe na ndoa hiyo ihesabike kwamba imeshindwa kuhimi mikikimikiki ya kutoelewana. nazungumzia hapo tamu inayogeuka kuwa shubiri baadaye.

Hukumu huu ilitolewa mwaka 1983 na Jopo la Majaji Watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania (Jaji Mkuu Nyalali, kama alivyokuwa wakati ule, Jaji Lewis Makame na Jaji Robert Kisanga). Mengi yalizungumzwa humo na kinachoskikitisha hata baadhi ya wanasheria wameilewa vibaya hukumu hii kwa kutoisoma kwa umakini neno kwa neno, aya kwa aya.

Inatosha tu kusema kuwa kikubwa kilichoelekezwa hapo ni kwamba mama wa nyumbani anastahili kupata mgawo katika mali iliyochumwa na wanandoa hata kama kazi alizofanya ni za nyumbani tu na mumewe haijalishi alikuwa akikesha akirusha ndege, katika vikao vya mawaziri, kwenye dili kubwa ama safari za ki-biashara ana kazi nyinginezo, iweza kitaalam ama za suluba. Nikumbushe tena, jambo hili lisieleweke kijumla jumla tu hivyo, mahakama ilitoa ufafanuzi zaidi katika hili na sitaweza kutazungumza yote hapa.

Kesi hii ni muhimu kwa vile Mahakama hii ikiwa ni ya Juu zaidi Kikatiba na ambayo hukumu zake zapaswa kufuatwa na mahakame zote chini yake (katika tafsiri ya sheria husika). Ndiyo kusema,Jaji wa Mahakama Kuu, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya au Ilala na wengineo wanatarajiwa kuzingatia msingi uliwekwa hapo.
 

nyamlega

Member
Jan 16, 2014
38
0
Vipi Kama hamjafunga ndo a ila mmeishi miaka mingi
Na kuchuma Mali pamoja na sasa mnataka kuachana?

Mkuu,mkishakaa miaka 2 ndani ya paa moja,kisheria ninyi ni mke na mume.japokuwa mkikaa miezi 6 watu wanaizungumzia kuwa mshakuwa wanandoa ni sawa,ila mkiachana hamuwezi kwenda sheriani,maana huko wanasikiliza waliokaa pamoja kuanzia miaka 2 na kuendelea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom