Msaada: Mfumo wa vyoo vya kisasa ukoje na una changamoto gani?

mwaega

Senior Member
Sep 22, 2013
189
254
Wanajamvi tuchangiane mawazo tafadhali kwa wale ambao wamekutana na kazi hizi mbili;

1. Mfumo wa choo cha kizamani, namaanisha unamuita fundi anachimba shimo anajengea vizuri kama tunavyofanya siku zote.

2. Mfumo wanaoita wakisasa, wakiutangaza sana kuwa vyoo havijai n.k, wanaita wenyewe vyoo vya kisasa.

Swali langu ni kuwa, changamoto gani inapatikana kwa vyoo wanavyoita vya kisasa ambavyo wanatangaza kila siku kuwa havijai n.k?

Je, ni mfumo mzuri au bora mtu aendelee na mfumo tuliozoea wakila siku (mfumo wa zamani)?

Msaada wa maoni na mawazo.

Screenshot_20230620-102847.jpg
 
Nimeweka kwangu ila Sasa situmii sio kwamba haujai ila majimaji yanapotelea ardhini ,changamoto IPO wakati wa mvua ardhi inakuwa na maji maji hivyo kama huna chemba za kutosha tegemea harufu, vitu vigumu kama vitambaa,baby wipes au peds ni hatari hivyo lazima uweke mazingira ya kuvipokea ila sio chooni na uweke matangazo vyooni kwani vikiingia kiasi kinaziba
 
Kabla ujajenga shimo la choo ni lazima ujue ardhi yako ikoje? Kama aedhi ni ya maji maji maana yake hivyo vya kisasa ni hatari.. Sifa ya shimo la choo ni kuwa na sehemu kuu tatu shimo la kwanza lime sakafiwa chini lina kuwa na sehemu kuu mbili muhimu sehemu ya kwanza kupokea uchafu na maji sehemu ya pili kuruhusu maji kwenda shimo la pili ambalo ndio sehemu ya tatu hili ali sakafiwi kazi yake kupokea maji tu kwa mtililiko huu shimo aliwezi kujaa..

Kutokana na ukosefu wa hela ufinyu wa ardhi wengi uchimba shimo moja tu lile la duara ambalo ndio kila kitu..
 
Shimo la duara (soak way pit) ni kwa ajili ya kuhifadhi maji maji tu na hili la mstatili (septic tank) ni kwa ajili ya kuhifadhi uchafu. Kama mtu hana uwezo wa kujenga yote mawili, anatakiwa ajenge hilo la mstatili na sio shimo la duara

Ukihitaji ramani zilizochorwa kitaalam kabisa kwa kuzingatia aspects za usanifu majengo tuwasiliane
 
Back
Top Bottom