Msaada maumivu tumboni na pande zote kulia na kushoto kupelekea ganzi mikononi na miguuni

G1992

New Member
Jul 30, 2019
2
10
Habari ya muda huu ndugu wana jamii forum, mimi ni kijana wa kiume umri ni miaka 30. Nina shida ndugu zanguni naomba msaada wenu hata wa kimawazo maana sijui nianzie wapi.

Ni hivi, kwa muda sasa yapata miezi 3 nimekuwa niki sumbuliwa na tatizo la kupatwa na maumivu maeneo ya tumboni japo sijui ni misuli ya tumbo au ndani ya tumbo, japo niliwahi fanya kile kipimo cha kumeza mpira tumboni kuangallia hali ya vidonda vya tumbo nika ambiwa nina shida ya GASTRITIS, nikapewa dawa aina omeprazole kwa ajili ya kupunguza acid tumboni nika tumia kwa mwezi 1.

Ila shida inakuja siwezi lalia tumbo,au kitu chochote nikiweka juu ya tumbo mfano nime lala nika egemezea latpop tumboni hata kwa dakika 10 tuu basi nitahisi maumivu kwenye misuli ya tumbo na muda si mrefu ganzi ina anza mkononi au miguuni, pia niki lalia tumbo, ubavu wa kushoto au kulia basi nikia amka asubuhi au usiku nikishtuka nina patwa na maumivu maeneo ya tumbo (misuli ya tumbo) na pande zote za ubavu yaani kulia na kushoto, hali haiishii hapo, bali nitahisi ganzi mikono yote 2 na miguu yote miwili, kuchoka sanaaa, kichefu chefu na kuhisi kutapika japo sitapiki.

Sasa nashindwa elewa shida iko wapi au niki enda hospital nipime kipimo gani tena maana mara ya mwisho nilienda hospital fulani hapa dar vipimo vilikuwa gharama kweli kweli, sasa hapa nawaza kuhusu gharama ya vipimo na kipimo gani hasa nikapime, nina pata shida sanaaa ya hii ganzi ka kushindwa lala kwa kutumia tumbo kwani nilisha zoea hivyo.

Kama kuna mtu aliwahi umwa hivi naomba aniambie shida ilikuwa nini, kipimo gani alifanya na dawa gani alitumia mpaka akapona.

Nina tanguliza shukrani zangu kwenu, samahanini kwa maelezo marefu.
 
Habari,
Pole na kuumwa.
Inahitaji uchukuaji mzuri wa historia yako. Kufanya examination/ uangaliaji wa mwili ili kuja na wazo la nini linasumbua. Kwa kifupi wazo linalikuja ni:

1: Shida kwenye njia ya chakula/gastritis/ H. Pylori

2: Shida inayohusisha viungo vya mwili kama ini.

NB: Fika kito cha afya jieleze vyema kwa mtoa huduma, usione uvivu au kuchoka kujieleza. Pia atakuangalia na kuona jinsi ya kukusaidia kwa kadri ya ufahamu atakaoupata juu ya afya yako.
 
Back
Top Bottom