Msaada: Dada yangu anapatwa na Ganzi Mguuni

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Ndugu zangu naombeni msaada nina dada yangu ni mgonjwa.

Anasikia maumivu kwenye mguu na baada ya kupata maumivu anasikia ganzi kwenye mguu baada ya kupata ganzi hata ukimpiga kitu gani kwenye mguu hawezi kusikia maumivu. Sijui ilo litakuwa tatizo gani.

Kwa bahati mbaya yupo kwenye kambi ya wakimbizi kule hakuna hospital za maana. Hawapimagi ugonjwa mwingine zaidi ya malaria tu.

Kama kuna mtu yeyote ambaye anajua dawa ya ugonjwa huu anaweza kutusaidia au jinsi ya kutibu kwa kutupa maelekezo.
 
Kama unaweza kumtoa hapo kambini kamtoe umpeleke hospitali. Hakunaga matibabu mazuri kama mgonjwa yeye mwenyewe kuelezea hali yake mwenyewe na akapata mtoa huduma anayejua kazi yake
 
Ndugu zangu naombeni msaada Nina dada yangu ni mgonjwa
Anasikia maumivu kwenye mguu Na baada ya kupata maumivu anasikia Gazi kwenye mguu baada ya kupata Gazi hata ukimpiga kitu gani kwenye mguu hawezi kusikia maumivu
Sijui ilo litakuwa tatizo gani

Kwa bahati mbaya Yupo kwenye kambi ya wakimbizi kule Hakuna hospital za maana
Hawapimagi ugonjwa mwingine zaidi ya maleria tu

Kama Kuna mtu yeyote ambaye anajua dawa ya ugonjwa huu anaweza kutusaidia au jinsi ya kutibu ugonjwa huu anaweza kutupa maelekezo

Pole kwa kuuguza.

Zingatia ushauri kwenye post namba 2.

Kuna mambo/shughuli ambazo zinaweza kuwa ni chanzo cha tatizo, ila mgonjwa hajui huvyo haoni tatizo kueleza mpaka akutane na wataalamu.

Mfano: kwa hapa tunawaza shida kwenye mishipa ya fahamu inayopeleka na kupokea mwasiliano toka mguuni.

1: Je ganzi inaishia wapi, ina muda gani, ilianzaje, ilianzia wapi, shughuli zake kuhusisha mgongo?

2: Historia ya ajali yoyote?

3: Umri wa mhusika?

4: Kazi zake?

5: Pia uhitaji wa vipimo zaidi?
 
Pole kwa kuuguza.

Zingatia ushauri kwenye post namba 2.

Kuna mambo/shughuli ambazo zinaweza kuwa ni chanzo cha tatizo, ila mgonjwa hajui huvyo haoni tatizo kueleza mpaka akutane na wataalamu.

Mfano: kwa hapa tunawaza shida kwenye mishipa ya fahamu inayopeleka na kupokea mwasiliano toka mguuni.

1: Je ganzi inaishia wapi, ina muda gani, ilianzaje, ilianzia wapi, shughuli zake kuhusisha mgongo?

2: Historia ya ajali yoyote?

3: Umri wa mhusika?

4: Kazi zake?

5: Pia uhitaji wa vipimo zaidi?
hizo point ni muhimu sana. ukienda kwa neurologist atakuuliza maswali kama hayo. Muone Dr Linjenje wa PCMC

most likely ni matatizo ya nerves
 
Back
Top Bottom