Wakuu, heshima kwenu! Nina mtoto wa mdogo wangu anasoma hapo UDSM mwaka wa kwanza. Alibahatika kupata mkopo, lakini namlipia malazi.
Kinachonishangaza ni kwamba tangu semister hii ianze mpaka leo anadai hawajaingiziwa pesa kwa hiyo inabidi nimpe pesa ya kula kila siku. Nimeona semister inaishia mwezi ujao sasa ninajiuliza kama mpaka saa hizi hawajaingiziwa fedha, wataingiziwa lini sasa.
Lakini kabla sijafikiria sana, nimeona niwashirikishe mlioko UDSM hasa mwaka wa kwanza, pengine mnaweza kunisaidia maana watoto wetu wanaotoka vijijini wakifika mijini wengine wanabadilika, wanaanza kujiingiza kwenye starehe. je, ni kweli kwamba mwaka wa kwanza hawajaingiziwa fedha?