Wanafunzi wa UDSM, tumezuiliwa kufanya mitihani kwa kushindwa kukamilisha Ada

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
431
1,101

Lecturer anayefundisha kozi ya Research Methodologies akifukuza Wanafunzi ambao hawajakamilisha Ada.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tumezuiwa kufanya mitihani ya Test One kwa kukosa vitambulisho vilivyo hai (Valid ID) kwa sababu ya kushindwa kumalizia Ada ya Semister ya Pili.

Hii inachagizwa na Wanafunzi wengi kuwa na kawaida ya kutumia fedha za kujikimu (Boom) tunazopata kutoka Bodi ya Mkopo kwa ajili ya kulipa ada, pia mpaka sasa wengi wetu hatujapata Boom la pili na hivyo kushindwa kumalizia ada tunayaotakiwa kuilipa.

Changamoto hii imetokea kwenye Vitivo mbalimbali hasa Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza na Wapili mbao walilipwa kiasi kidogo.

Wanafunzi tulituma barua ya maombi kwa Mkuu wa Chuo kuomba turuhusiwe kufanya mitihani kwa kuwa malipo ya Bodi yanatarajiwa kutolewa wiki ijayo lakini majibu tuliyopata ni kuwa hilo halitawezekana.

Uongozi wa Chuo umesisitiza Wanafunzi wote wanatakiwa kulipa Ada kwa maelezo kuwa wapo ambao hawategemei Boom kulipa ada ambao hawajapata mkopo na kuwa idadi ya ambao hawajalipa ada ni kubwa, hivyo chuo kina ukwasi.

Majibu ya Bodi ya Mikopo - HESLB: Fedha za kujikimu (Chakula na Malazi), Wanafunzi kuanza kupokea kuanzia Jumatatu, Mei 20, 2024
 
Back
Top Bottom