Msaada kwa ndugu yetu huyu

Nimepitia huu uzi mwanzo hadi mwisho kuna baadhi ya matukio nimeyakumbuka kupitia huu uzi. Lakini zaidi ni vile binadamu alivyobadilika sasa hivi au kuwa na sera mbaya ambazo haziangalii ubinadamu kwanza bali usalama kwanza. Si jambo baya sana kuwaza usalama, lakini pia tuchukue mjda kidogo wa kuwa na benefit of doubt kwa baadhi ya vitu/taarifa na kunyoosha mkono pale tunapoweza kusaidia baada ya kupima hasara na faida. Kwenye hili kuna faida nyingi ya kusaidia kuliko hasara ingawa kuna baadhi ya maswali ukijiuliza unapata ukakasi kidogo kama utakua ile roho ya utu imekutoka kidogo. Niliwahi kuhusika kumsaidia Msauzi mmoja ambaye alikua anaumwa na tuchakanga pesa za kumpeleka hospitali kwa kweli kitendo kile kilimtoa machozi akakiri kuwa hata kama angekua kwao ndugu zake wasingekuwepo angeweza kufa. Inanipa wasiwasi kwa binadamu kuwa na sera nyingi ngumu au kuweka uzito tuuu kwenye mambo ambayo hayapaswi kuwekewa uzito. Mtu ukiwa mtaalamu eneo fulani ukiongea na mtu tuuu kwa utaalamu wako utajua kuwa huyu ni sawa au si sawa. Naomba kuwasilisha na nasimama kukosolewa.
 
Lakini amesema kbs yuko mbali!
Yap yeye yuko mbali bt mjini hapo ana wadau wa kutosha tu ambao angemlengesha jamaa chap tu wangempa tag...
Jf ni last refuge labda sababu kuubiwe bkoz kamjulia jf basi wadau wa jf ndo wahusike.. Ila naamini msaada ushapatikana by now
 
Wakenya ni wajuaji sana,kuna dogo mkenya tunaishi nae amekuja kusoma sasa kawa MTU Wa makundi ya vijana Wa mtaani wavuta bangi, walevi na wacheza kamari,sasa wenyeji walimtahadharisha asiwe na marafiki wasioeleweka lakini hakusikia.

Sasa kilichomkuta anajuta alienda kuweka bond tablet ya Samsung kwa muhuni mmoja Wa mtaani ile muda Wa kurudisha pesa umefika akaja kuitwa anaambiwa wezi wamekata dirisha wameiba tablet,simu 2 na sh.laki2,mpango ulipangwa kifamilia mama Wa muhuni akawa anatetea wameibiwa kweli, ukicheki sehemu iliyokatwa ni ndogo ukilinganisha na ile tab,mkenya akawa ametapeliwa kihivyo.

Unakuta wakiwa wakenya wawili wanajifanya wajuaji kuliko wenyeji wao wanajipangia mambo yao wakishafikwa na matatizo ndio wanakuja kutia huruma kwa wenyeji wao, inabidi wabadilike kabisa la sivyo ndio yanakuja kutokea kama haya.
Pole sana mkenya na mshana jr.
 
Hii ishu ni ya tangu jumamosi na mimi nimeiweka hapa jana... Kwahiyo hizo siku nne zote zilizopita kuna wadau wangu wameshatoa support sana
Yap yeye yuko mbali bt mjini hapo ana wadau wa kutosha tu ambao angemlengesha jamaa chap tu wangempa tag...
Jf ni last refuge labda sababu kuubiwe bkoz kamjulia jf basi wadau wa jf ndo wahusike.. Ila naamini msaada ushapatikana by now
 
Kwanini uende mbali kabla hujatatua matatizo ya mgeni wako?
Umemkimbia? Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
 
thanks,will do
 
Hahaha kweli Wengi ni rejected Katika Jamii inayowazunguka
Humu Ndio faraja yao
 
Mbona umepanic chifu

Huwezi jua coments yangu moja imeokoa watu wangapi wasipigwe hahaha

Kwahiyo Endelea kujifunza sisi haya Mambo tunayaelewa
Jitahidi kutumia ujinga wako vizuri kama unakupa faida.
 
Shukrani kwa wenzetu wa JF waliojitolea kwa hali na mali kumsaidia.... Mbarikiwe mno... Changamoto iliyopo saivi ni wadhamini ili apate dhamana mpaka tar 19 January kesi yake itakapotajwa tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…