Msaada kwa anae fahamu hili swali, an appraisal of handling of exhibits in law enforcement agencies practice: Tanzania police force

Timotheo Kija

Member
Aug 31, 2015
44
95
Habari za mda huu,

Ikiwa kama kuna regulations, laws au Act zozote zinazoweza kutoa majibu ya hilo swali naomba mnisaidie.
 

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
1,972
2,000
si uendepe pale police station/post iliyo karibu na wewe.au unaogopa kukamatwa na kubambikiwa kitu?
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,917
2,000
Dogo, cheza na sheria tatu, usiumize kichwa na Sheria Nyingine;

1) The Criminal Procedure Act CAP 20 RE 2019.
2) The Evidence Act CAP 6 RE 2019.
3) The Cyber Crime Act 2015.
4) The National Prosecution Service Act na Establishment Of The Office Of DPP as per Section 89 of CPC. - Hii kama swala lako linakwenda kuhusiana na Makosa ambayo DPP ana mamlaka fulani alizopewa kama Kuzipa nguvu Mahakama Za Hakimu Mkazi Kusikiliza Baadhi Ya Kesi na Makosa Ya Uhujumu Uchumi.
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,917
2,000
Nashukuru,unaweza lifafanua linataka nn hasa
Tathmini ya jinsi vyombo vya utekelezaji wa sheria nchini Tanzania unavyo shughulikia maswala ya vidhibiti (Handling Of Exhibits).

Swali ni pana sana, kuelezea nini hasa kitu kinacho tambulika kama kidhibiti kisheria, kuna maswala ya kuchomekeana vidhibiti (Hapa umekamatwa huna kosa ila askari anakuchomekea stiki za bangi mfukoni), upungufu wa vifaa vya kisasa vya kuhifadhi vidhibiti vinavyo haribika kutokana na muda (Mfano mtuhumiwa akikamatwa na Nyanya au Nyama za wizi, vituo vya polisi hawana vifaa vya kuhifadhi mpaka kesi ianze vidhibiti zimesha haribika n.k), madhaifu ya sheria kwenye kutambua na upokelewaji wa baadhi ya vidhibiti mbele ya mahakama (Mfano vidhibiti vya kielektroniki mpaka kiapo ndio vipokelewe mahakamani) na mengine mengi.

I hope hautaisahau ile kesi maarufu ya magufuli (The Magufuli Case) ya wavuvi waliokamatwa na samaki katika bahari ya tanzania wakiwa hawana vibali na wakiwa wana samaki wengi sana, magufuli akatoa amri samaki wagaiwe kwenye mashule ya bweni kuhofia wasiharibike. Mwisho wa kesi walishinda wale wavuvi na hawakukutwa na hatia yoyote kwasababu ya kukosekana vidhibiti, na wakashitaki kudai fidia. Magufuli kukurupuka kwake akaitia hasara serikali mabilioni.

Hapo nimekupa njia ya muelekeo tu.
 

Timotheo Kija

Member
Aug 31, 2015
44
95
Tathmini ya jinsi vyombo vya utekelezaji wa sheria nchini Tanzania unavyo shughulikia maswala ya vidhibiti (Handling Of Exhibits).

Swali ni pana sana, kuelezea nini hasa kitu kinacho tambulika kama kidhibiti kisheria, kuna maswala ya kuchomekeana vidhibiti (Hapa umekamatwa huna kosa ila askari anakuchomekea stiki za bangi mfukoni), upungufu wa vifaa vya kisasa vya kuhifadhi vidhibiti vinavyo haribika kutokana na muda (Mfano mtuhumiwa akikamatwa na Nyanya au Nyama za wizi...
Nashukuru sana mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom