Msaada kwa anae fahamu hapa shida itakua nini

Peter_John

Member
Sep 12, 2022
50
86
Habari Wana JF , Kuna mtoto hapa wa ndugu yangu umri wake ni miezi kama kumi hivi au zaid ila hajafikisha mwaka mmoja , ni mtoto wa kiume ila anatatizo sehemu zake za Siri muda mwingine zina sinyaa na kua ndogo ndogo yaani ndogo sana na Hadi wakati mwingine zinapotea kabisa yani huoni kitu , kwa ane fahamu shida hapo itakua ni nini na tunaanzia wapi, kitu ambacho nahisi labda ni kwa sababu alitahiriwa akiwa mdogo sana , alitahiriwa akiwa na siku 40 tangu azaliwe , hatujui tuanzie wapi kwa anae fahamu tiba yake atusaidie jamani
 
Sasa na nyinyi mliona wapi mtoto ana siku 40 akatahiriwa?
Mlikua mnawahi wapi kwani?
 
Sasa na nyinyi mliona wapi mtoto ana siku 40 akatahiriwa?
Mlikua mnawahi wapi kwani?
Daah ni kweli, ila mama yake na huyo mtoto alikwendwa kujifungulia kwao Kisha akaa huko kwa muda baada ya kurudi watu ndo tunagundua ingawa alimjulisha baba wa mtoto na baba wa mtoto alitoa idhini bila kuhusisha Mtu mwingine, aisee kama ningeli fahamu hili kabla angalau ningetoa mawazo yangu ingawa yasinge sikilizwa, maana hii famalia naijua mwenyewe,
 
Habari Wana JF , Kuna mtoto hapa wa ndugu yangu umri wake ni miezi kama kumi hivi au zaid ila hajafikisha mwaka mmoja , ni mtoto wa kiume ila anatatizo sehemu zake za Siri muda mwingine zina sinyaa na kua ndogo ndogo yaani ndogo sana na Hadi wakati mwingine zinapotea kabisa yani huoni kitu , kwa ane fahamu shida hapo itakua ni nini na tunaanzia wapi, kitu ambacho nahisi labda ni kwa sababu alitahiriwa akiwa mdogo sana , alitahiriwa akiwa na siku 40 tangu azaliwe , hatujui tuanzie wapi kwa anae fahamu tiba yake atusaidie jamani

Hii ni hali inaitwa penile hiddening/kujificha kwa uume. Huweza kutokana na tatizo la ligaments za uume au unene wa mtoto, mafuta sehemu ya kinena. Pia unaweza kuchangiwa na kiasi cha ngozi ilivyovutwa wakati wa kutahiriwa.

Haya huwa ai matatizo ya kudumu, ingawa ni muhimu kumfikisha mtoto kwa mtaalamu wa afya kwaajili ya ukaguzi zaidi.
Haina uhusiano wa moja kwa moja na kufanyiwa tohara mapema.
 
Poleni
Wamchunguze Isijekuwa Ngiri/Henia
japo Mambo Ya Tohara Mapema Ni Shida Kuna Mkoa Walikata Uume Wote
 
Back
Top Bottom