Msaada: Kuondoa utelezi maji ya mvua

Wakuu,kutokana na maji ya bomba ya dawasa kutoka kwa muda wa lisaa limoja tu kwa kila miezi 3,nimeona nihifadhi maji ya mvua
Tatizo yana utelezi fulani mwilini,minapooga,je njia rahisi ya kuondoa huo utelezi ni ipi?,msaada tafadhali.
Tia Chumvi kiasi fulani yanafanya kuondoa utelezi na yaweza kukaa muda mrefu bila kuzalisha wadudu
 
Wabongo bhana. Siyo utelezi. Hayo kitaalamu yanaitwa maji laini. Ni maji yasiyokuwa na chumvi, ndo maana ukitumia sabuni povu linakuwa jingi, maji mengine laini ni ya mitoni. Maji magumu yanakuwa na chumvi ndo maana sabuni hazitoi povu mfano maji ya Dodoma au ya visima vifupi.
Sasa unapoweka chumvi maana yake unayafanya kuwa magumu.
Maji laini yana umuhimu wa kwanib husaidia kutumia sabuni kidogo na kuto kuuchakaza nguo.
 
Siyo wabongo bos ni hatujui, mi ndo nimejua leo kuna maji laini na kuna kuweka chumvi.
Nina swali mfano maji lita 3000 chumvi naweka kiasi gani?
 
Wakuu, kutokana na maji ya bomba ya dawasa kutoka kwa muda wa lisaa limoja tu kwa kila miezi 3, nimeona nihifadhi maji ya mvua

Tatizo yana utelezi fulani mwilini mimi napooga, je njia rahisi ya kuondoa huo utelezi ni ipi? Msaada tafadhali.
Labda mazoea.

Mi natumia maji ya mvua zaidi ya miaka 12, sioni shida.

Navuna kwenye kisima na kupandisha juu kwenye tenki kisha hushuka chini kwenye mabomba.

Familia haijawahi pata magonjwa yoyote

Nakunywa lakini nachemsha, na kufanyia kila kila kitu.

Yakija ya bomba wakati wa kiangazi, huwa naona kama yana chumvi....magumu, huwa siyapendi.

Mara chache huweka water guard kwenye kisima.
 
kuna ukame na uhaba wa maji kwye mito ndo maana Dawasco hawana maji.
Mvua inanyesha kwenye majaruba na maji yanatitia

Hii nchi imelaaniwa kwa kuwa na viongozi wasio na upeo
Vipi wananchi nao, wana upeo? Viongozi wanatokana na wananchi, wananchi kama wana upeo, wangeweza kuwashawishi viongozi wasio na upeo wafanye mambo kwa mantiki.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom