Msaada: Kununua nyumba Tanzania kwa hela zilizo benki iliyo Marekani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Kununua nyumba Tanzania kwa hela zilizo benki iliyo Marekani.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Al-Watan, Mar 17, 2010.

 1. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,563
  Likes Received: 13,327
  Trophy Points: 280
  Wakubwa heshima zenu.

  Mie kijana nimezichanga ughaibuni kwa kiasi (si kama Bligate hahaha), tatizo ilmu ya mambo ya fwedha haijakomaa.

  Tatizo linakuja, nikitaka kuja kununua kitu cha gharama kubwa nyumbani, mfano kibanda cha kuotea Tanzania kwa pesa iliyoko benki ya Kimarekani, malipo nitafanyaje?

  Maana ndugu zetu wengine huwezi kuwalipa kwa credit card, na Mmarekani haruhusu kutoa zaidi ya $ 10,000 bila maelezo marefu, Wamexico wanaotewa kila kukicha, kuna mmoja alifanya kazi kuosha vyombo miaka 10 na kuzichanga $ 60,000, wakamuotea na kumpukutisha $ 50,000. Isitoshe kutembea na mihela mingi ni ulimbukeni.

  Sasa nikikutana na Mzee asiyejua hili wala lile, anauza nyumba kwa cash Dar, na mimi nina hela benki ya Kimarekani, nitafanyaje.

  Natanguliza shukurani.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...swali zuri.
  Vipi ukinunua kitu/vitu vya thamani hiyo halafu ukaja viuza nyumbani?

  No, am not talking about 'Money laundering' here, msinikodolee macho :(
   
 3. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  usumbufu wa ushuru na rushwa unaweza ukaona nusu ya pesa uliyopiga box miaka kibao inaishia kwenye kuhonga, Bongo watu hawakuachi ukatishe hivi hivi.
   
 4. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  acha woga,still hiyo pesa ni yako andikisha hayo maelezo utapewa pesa yako kiasi chochote utachohitaji,nashangaa kwanza kama mpaka hapo ulipo huna acc kwenye benki ya nyumbani pole.
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...swali la nyongeza;
  afungue account kwenye bank gani Tanzania ambayo anaweza kufanya Online transfer?
   
 6. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ushauri wangu;
  Kama ulivyosema si rahisi kwa Wamarekani kukuruhusu kuchukua kitita cha zaidi ya USD 10K. Na pia si rahisi kukuruhusu utume kwenye akaunti ya mtu binafsi pesa nyingi maana wanaweza kudhani unafadhili Alqaeda na hata wakikurusu ndugu yangu ni risk, maana waweza kumwekea mtu mamilioni hayo kwenye akaunti yake na nyumba usiipate. Kwahiyo nakushauri ufanye mpango wa kununua nyumba kenye mashirika yanayoeleweka kwa mfano NHC wana nyumba wanauza kule Mbweni (from TShs 72M to 142M) au NSSF wana nyumba wanauza sehemu mbalimbali ikiwemo kule Tuangoma (Kigamboni). Unaweza kuwasiliana nao wakakutumia proforma invoice utakayoitumia kwenye benki yako huko Marekani kutuma pesa kwa njia ya TT.
   
 7. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mbu,
  Benki yoyote kwa TZ anaweza kufanya online transfer kutokea nje. Mimi huwa nafanya online transfer kwenda CRDB na Exim Bank. Kama anataka kufungua akunti ya dola (USD), Exim Bank ni wazuri zaidi maana charges zao ziko chini sana kuliko benki yeyote Tanzania kwa forex akaunti.
   
 8. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,563
  Likes Received: 13,327
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe unataka niandikishe halafu nisafiri na $ 50,000 au zaidi in cash kwenye ndege?

  Nafikiri hili la online transfer linahusika zaidi.

  Ingawa nasikia kuna wakuu wanazikamata katikati hapo bongo, benki za kibongo hazina mawaa?

  Kuna mtu kashawahi kutumia Citigroup ya Dar na ya North America katika kuhamisha michune kwa style hii?
   
 9. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  ok hapa umeongea mkuu,hata mimi kikubwa nnachohitaji kujua ni hiki maana nimechoka kutapelewa kwa kuwatumia ndugu na jamaa,ila pia hii ya online naona nayo ni risk kweli da.
   
 10. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Babukijana risk gani iliyoko kwenye online transfer? Maana inabidi uwe na akaunti TZ tthen unahamisha pesa zako kutoka uliko kwenda kwenye akaunti yako ya TZ kwa internet (online transfer). Kukiwa na tatizo benki yako (huko unakotoa pesa) watakujulisha. Nimekuwa nikifanya hivi kwa zaidi ya mwaka sasa na sijawahi kupata tatizo lolote, pesa zinaingia kama kawaida baada ya siku 5 au ukitaka express zinaingia siku hiyohiyo ila charges zake ni kubwa.
   
 11. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu, nijuavyo mimi ni kuwa CitiBank Tanzania ni kwa ajili ya makampuni tu na si kwa individuals sijui kama wamebadili utaratibu huu kwa sasa.
   
 12. Naumia

  Naumia Member

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 13
  Ningekushauri ufungue Tanzanite account through Tanzanian Embassy in DC (if you are in USA). Process Inachukua mda kidogo...but its worth it. Then kabla ujaondoka kwenda Dar fanya International wire transfer to your Tanzanite account. I believe the fee is $45 for most USA banks.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sheikh wataka kurudi bongo ili iweje?

  We bana hukohuko ulipo, huku bongo watakukera tu na mwisho utajuuuta kufikiria hata ni shetani gani alikushawishi kurudi. Huku bana tuachie akina sisi, kwanza umeskia umeme hamna, sasa shauri yako, kama hujakamata jimama la makaratasi unajipalia makaa ya moto kichwani..ohoooo.
   
 14. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha.......hahahhahahahahahahahahaha.....hahahahaha...

  We jamaa wewe yani mbavu zinaniuma kwa kucheka.

  Hivi mbona nakuona wewe ndo yule nlo soma nae?!
  Yaani jamaa alikua na vituko kama vyako. My instincts tell me its u! Tena jamaa anakaa zenji, utakua wewe aluu. Kama sio wewe pacha wako basi.

  Dah! Naenda ospitali kutibiwa mbavu.
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sasa wacheka, wachekani sasa hapo ami?

  Mi nlikua namshauri mdau ajiepushe na dhahma zinazoepukika kaa hizo anazotaka kujiingiza kichwakichwa.

  Ni hayo tu mkuu. . .
   
 16. M

  Mkora JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapo tupo pamoja, halafu hujamwambia kuhusu hizo bei zenu zisizo na kichwa wala mguu
  Nyumba mbavu za mbwa kiwanya lease hold bei ni ya kufa mtu
  Nilikuwa na tudola 100,000 nikaonyenshwa nyumba ya milioni 200 ambayo hamna maji, umeme wala barabara, nighbourhood mshikemshike mtaa mmoja baa tatu, ikabidi nishindwe mimi, lakini kwa budget hiyo hiyo nimeweza kununua nyumba Johannesburg na appartment Dubai na chenji ikabaki
   
 17. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Real estate business bongo bado haijatulia; lakini kwa kukwepa ushauri mdau naomba wasiliane na GIMCO Africa hawa ni real estate makini wanayo website for further contacts anaweza akawalipa na wakampa nyumba ya maana kama wanayo.
   
 18. M

  Mkora JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu hata ukiwasiliana na hao jamaa haitasaidia bora kusubiri hizo pesa za wizi ziishe na bei ita promoka saana na watu watajuta kununua kwa bei hiyo
  Just imajine nyumba ipo kwenye kiwanja cha lease ya miaka 33 unalipa sh 200milion
  sasa baada ya hiyo miaka 33 serikali ikigoma kurenew lease ut hama na nyunba yako ?
   
 19. MtuSomeone

  MtuSomeone Member

  #19
  Mar 19, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili si suala la kuleta kwenye JF, ni issue ndogo sana!
  1. Kama una akaunti yako bongo tuma hela zako kwa international wire transfer, then ukiwa huku unaweza kuchukua...easy
  2. Kama huwezi hilo huyo anayeuza kwa cash akupe akaunti yake, tuma fedha kulingana na that day's exchange....hakikisha unapoweka atleast zizidi hata elfu 10 ili huyo mzee anayekuuzia afurahi maana nimeshawahi kumtumia mtu hela exchange rtae ikawa tofauti kukapungua elfu 3 ikawa ishu!
  3. Kama zote hizo unaona haziwezekani mtumie unayemuamini...wazazi etc, wao watafanya malipo cash....easy
  4. Kam ahuwaamini wote kaka kwa pesa ya marekani $50,000 au hata $100,000 si mzigo mkubwa at all, tumeshawahi kuzibeba zaidi ya hizo (japo haikuwa zetu), weka kwenye kibegi chako unachoingi anacho kwenye ndege, kile cha kufungia kiunoni ni bora zaidi.....KAMA UNAMSUKUMA MLEVI
  Kila la kheri
   
 20. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna mambo muhimu lazima uangalie kabla hujaamua kubeba kitita cha noti kwenye ndege.

  Mfano kama unatoka UK siku hizi huruhusiwi kubeba zaidi ya £1000.00 tasilimu kama utabeba ni lazima uonyeshe kwamba umezipata kihalali - yaani una bank statement zako, na vile vile uonyeshe kwamba umezilipia kodi muafaka. i.e. PAYE or corporate tax etc.

  Hata kama ukiamua kutuma fweza bongo kwa TT lazima uwe makini kwa sababu mfano kutoka marekani any transaction of more than $5000.00 kwenda popote pale duniani huwa inafanyiwa kitu kinachoitwa monitoring kutokana na urahisi sana wa kutumia computer technology hata baada ya miaka miwili hata mitano wanaweza kuja kukuuliza uhalali wa fweza ambazo umezituma etc.

  Njia rahisi na nzuri kwa wengi japo sio wote ni kuwa na off shore account kama ya Mwizi wetu Vijisenti huko huwa hakuna maswali unaweza kutuma any amount anywhere bila mkwaruzo wowote. Ongea na bankers wako watakuambia nini unahitaji kufanya na wanaweza wakakupa advise nzuri sana. Lakini usisahau usibebe furushi la fweza kwenye ndege siku hizi za matatizo ya kujilipua. Vile vile usisahau unaweza kutuma foreign cheque Tanzania ambayo kama sikosei inachukua kama wiki mbili kuwa cleared bankers Tanzania wanaweza wakakupa definitive time. ALL THE BEST.
   
Loading...