Msaada: Kununua nyumba Tanzania kwa hela zilizo benki iliyo Marekani.

Nadhani tuache kudanganyana hapa; kama fedha umezipata kwa halali na unataka kuzitumia kwa uhalali unaweza kuzihamisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine bila tatizo. Unachotakiwa kufanya ni ku prove kwamba umezipata kwa halali na utazitumia kwa uhalali.
 
Mkuu hapo tupo pamoja, halafu hujamwambia kuhusu hizo bei zenu zisizo na kichwa wala mguu
Nyumba mbavu za mbwa kiwanya lease hold bei ni ya kufa mtu
Nilikuwa na tudola 100,000 nikaonyenshwa nyumba ya milioni 200 ambayo hamna maji, umeme wala barabara, nighbourhood mshikemshike mtaa mmoja baa tatu, ikabidi nishindwe mimi, lakini kwa budget hiyo hiyo nimeweza kununua nyumba Johannesburg na appartment Dubai na chenji ikabaki

Kamanda hili ni la ukweli kabisa. Sielewi tatizo limeanzia wapi haswa.

Kuna thread ilianzishwa humu kwamba soko la mambo ya nyumba halipo regulated. Watu wanauza vitu kwa bei ya ajabu sawa na bei za US kwenye prime areas. It is crazy out there mazee.

Huenda waizi wa mali ya umma wanasababisha haya maana wao ndo wanunuzi wa kumwaga hayo mahela, maana hawakuyatolea jasho.
 
Back
Top Bottom