Msaada kuna vibali vya upigaji picha maeneo ya mijini?

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
Habari wakuu. Kama kisomekavyo kichwa cha habari, binafsi nimeanzisha shughuli ya kutangaza utamaduni na maisha ya Tanzania nikitia ndani vivutio vyote, watu na kila kitu.

Kwa sasa nimekumbana na changamoto nyingi ikiwemo kuzuiwa kupata picha za mnato kwenye baadhi ya maeneo ambapo kwa macho yangu sioni kama ni kosa kupiga picha maeneo hayo.

Hivyo wakuu, kama kuna vibali maalumu vya ruhusa ya kufanya hivyo tafadhali naomba nijuzwe hapa.

Ahsante.
 
Wewe siyo mzima kichwani, huwezi kulazimisha kupiga Picha sehemu wenyewe hawataki.

Ikulu ya Marekani kupiga Picha ruksa, ikulu ya Tanzania Picha hawaruhusu, kambi za Jeshi hawaruhusu na sehemu zingine utaona Salama maalum au tangazo la kukataza.

Kama Kwa sababu zako tunahitaji Picha za maeneo hayo kibali utapewa na hao wenyewe wahusika wa maeneo hayo.

Kama ni ikulu waone wenyewe ikulu, kama ni Jeshi ni waone wenyewe na sehemu zote utaratibu ndio huohuo.
 
Ahsante mkuu kwa ushauri wako, lakini kuna sehemu niliambiwa nikatafute Kibali ngazi ya juu, sehemu nyingine mbili zaidi niliambiwa hivyo na wenyewe hawakusema niende wapi kupata ruhusa hiyo.
 
Ahsante mkuu kwa ushauri wako, lakini kuna sehemu niliambiwa nikatafute Kibali ngazi ya juu, sehemu nyingine mbili zaidi niliambiwa hivyo na wenyewe hawakusema niende wapi kupata ruhusa hiyo.

Vibali vya picha jongevi na mnato vinatolewa Bodi ya filamu Tanzania. Ofisi zake zipo UTUMISHI HOUSE barabara ya Kivukoni.
 
Back
Top Bottom