Msaada: Kuna mtu amehack simu yangu

Msaada: Kuna mtu amehack simu yangu

Kasheshe hilo, huyo mtu hawezi kukuambia yeye ni nani lakini siku ukimjua utashangaa sana maana ni mtu wa karibu yako kabisa kama si mpenzi wako ama mkeo/mumeo au ni rafiki tu wa karibu sana lengo ni kuku spy mawasiliano yako. Kumbuka vizuri mtu ambaye anauwezo wa kutumia simu yako ni nani maana atakua amefanya hivi, kachukua simu yako kadownload app yoyote ya spy then akaisajili kwa email yake then aka hide hiyo app kwenye simu yako sasa yeye akienda ku login kule kwenye web basi kila kitu kinachoendelea kwenye simu yako anakipata, kuna spy app zingine zina spy mpaka whatsapp ila kama hiyo app haina uwezo wa kuona whatsapp basi upande wa whatsapp alichokifanya yeye amefungua whatsapp web kwenye computer yake inakuja barcode fulani hivi akachukua simu yako akaingia whatsapp akafungua camera akalengeshea kwenye ile barcode ya kwenye laptop yake basi whatsapp yako inafunguka kule pia. Akarudisha cm yako, sasa kila unapokua online na kule unasomeka online yaane yeye pia anauwezo wa kumjibu mtu pia. Kwenye upande wa sms za kawaida wewe angalia app yoyote kwenye simu yako kama inahusiana na spyng itoe
Mkuu umeelezea vizuri sana. Niongeze tu kuwa kuna apps zingine za kuspay si lazima ziwe installed kwenye sim ya muhusika isipokuwa unapozikofigure basi unazikofigure na number za mtu unaetaka kumspay. Kwa apps ya namuna hii ili usiweze kuwa spayed kwenye watsap basi badilisha number ya watsap kwenye watsap setting yako.
 
Habari zenu wapendwa.
Mwenye uelewa wa nini chakufanya anisaidie jamani
Napiga simu nayeye anapata taarifa yote
Msg zangu anauwezo wa kuzisoma na kujibu yeye zote za kawaida na whatsapp pia
Hata location yangu anaijua kila ninaposogea.
Nenda setting kisha security alaf device administrator kisha tuambie unakuta applications gan ndani ya device administrators
 
Factory reset baasss..au angalia kama kuna ki application kinaitwa spy... kama hamna factory resert af endelea kutumia email hyohyo.akiendelea ndo utajua kuwa anatumia email kuiingilia cm yako

Sawa mkuu. Asante
 
Mkuu umeelezea vizuri sana. Niongeze tu kuwa kuna apps zingine za kuspay si lazima ziwe installed kwenye sim ya muhusika isipokuwa unapozikofigure basi unazikofigure na number za mtu unaetaka kumspay. Kwa apps ya namuna hii ili usiweze kuwa spayed kwenye watsap basi badilisha number ya watsap kwenye watsap setting yako.
Mkuu ni pm aina ya hizi app ambazo haziitaji kuinstall katika simu ya muhusika, msaada tafadhali kuna kitu nahisi nimefanyiwa na mimi pia
 
Nenda setting kisha security alaf device administrator kisha tuambie unakuta applications gan ndani ya device administrators

Android Device Manager
Smart AppLock
CM Security

Nakutana na hizo application
 
Mkuu umeelezea vizuri sana. Niongeze tu kuwa kuna apps zingine za kuspay si lazima ziwe installed kwenye sim ya muhusika isipokuwa unapozikofigure basi unazikofigure na number za mtu unaetaka kumspay. Kwa apps ya namuna hii ili usiweze kuwa spayed kwenye watsap basi badilisha number ya watsap kwenye watsap setting yako.

Mmmmh.! Sasa mkuu kama ni mtu wa karibu kwangu nikabadili namba ya whatsapp akaipata si bado ataendelea na upuuzi wake anaoufanya sasa??
 
Pole sana. Huyo kiumbe Hana ustaarabu kabisa. Ukishamjua na kujua namna ya kutatua tatizo, usisahau kumpeleka police
 
Pole sana. Huyo kiumbe Hana ustaarabu kabisa. Ukishamjua na kujua namna ya kutatua tatizo, usisahau kumpeleka police

Asante mpendwa.
Yaani sijui ananitafuta nini au ametumwa na nani na ana mpango gani namimi maana si jambo la kawaida.
 
Asante mpendwa.
Yaani sijui ananitafuta nini au ametumwa na nani na ana mpango gani namimi maana si jambo la kawaida.
Akishakuwa nyuma ya nondo yote hayo ataelezea vizuri tu na utajua kwanini alifanya maamuzi ya kipuuzi kiasi hicho
 
Uyo ameweka application ambayo ina uwezo wa kufanya aya
Kutambua location
Kuona na kusoma chats zako za watsapp sms za kawaida na hata messenger za Facebook
Kuoona missed calls received calls na dialed calls
Yote ayo ameweza baada ya ku install app kama MAXXSPY so chakufanya nenda settings kisha fanya factory resetting utakua umetatua tatzo. cc rubii
 
Hili Janga liiliwahi nitokea na nililipoti hapa JF,

kwangu mm issue ilikuwa mdogo mtu(kike) anataka niachane na dada ake,

so alikuwa anapata each and everything ninavyo fanya kwa sim,yaaini mail,whatsapp,viber,yahoo na msg plus voice..

Kuna siku nilibadili pass ya Gmail baada ya kushauriwa na wana JF,nilivyo badili to Pass alinitumia sms ilisema hivi(hahhahahaha umebadili pass,chezea it ww),nilitamani nimuuwe.

alikuwa nafanyaye?
Kwanza alikuwa anashirikiana na jamaa wa usalama ambaye alikuwa ubakozi wa Misri Tz

Huyo jamaa anakifaa mfano wa sim,kimetengenezwa japani, lengo la hicho kifaa ni for security issues,maani kinaweza kusensi kama mtu anasilaa akiwa umbali flani,pia kwa ajili ya upelelezi,hicho kifaa ukimpa namba ya mtu yeyote kina vuta inf zote kwa hiyo sim pamoja contact zote sms calender issue nk,hata uwe na sim ya kitochi,

Baada yakuwa na inf zako zote kinakuwa kinasave each and every thing unacho fanya kwa sim,pia sim yako inakuwa ipo kiganjani kwake anweza mcall mtu yeyote amtakae,hata amtukane itaonekan ni ww ndio umefanya hivyo.

Nilijuaje?

Nilihangaika sana na apps za kwa mitandao, hata kuna apps unalipia kama laki 250,kwa mwezi niliitumia,

Hi apps nimeisahau jina ila naweza kukutafutia,ina act kama untvirus,inakutell how inf zako zinavyo populated..

basi tangia hapo jamaa akajua kuwa kunasomething wrong.so nahisi kwa heshima ya kazi yake akaachana na namba zangu.

Akanipa na mbinu kuwa nikitaka nikikomeshi hicho kishem changu ninunue HUWEI P8,hii sim ni baala,

Yule jamaa na shem wangu now nimarafiki sana tu..

So mkuu kama anatumia mbinu hii ww nenda kanunue huawei.
 
Turn of data sync

Turn off location.
hii ni kwa ajili ya kuzima gps tracker kama imehifadhiwa kwenye simu yako

Turn off background application.
ni zile ambazo zina ji-run pale tu simu yako unapoiwasha.
Hivyo app zinazo track mawasiliano ya watu huwa zipo katika mfumo wa kuji- run automatic.

Nenda kwenye manage app, kisha tizama app in process Hapo utaona app zote zinazofanya kazi kwa wakati huo. kama kuna app inayotrack mawasiliano yako hapo ndipo utakapoiona.
 
Ndio maana siku zote nitaendelea kutumia Blackberry. Huo upuuzi huwez kufanyia simu hizi.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Ndio maana siku zote nitaendelea kutumia Blackberry. Huo upuuzi huwez kufanyia simu hizi.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Spying apps hata kweny brackbery zipo... Mtu akitaka ku kuspy anaweza tu akiamua.
 
Uyo ameweka application ambayo ina uwezo wa kufanya aya
Kutambua location
Kuona na kusoma chats zako za watsapp sms za kawaida na hata messenger za Facebook
Kuoona missed calls received calls na dialed calls
Yote ayo ameweza baada ya ku install app kama MAXXSPY so chakufanya nenda settings kisha fanya factory resetting utakua umetatua tatzo. cc rubii
Unistall apps ambazo huzielewi, change password ya gmail, na fata ushaur wa wengine huko juu
 
Spying apps hata kweny brackbery zipo... Mtu akitaka ku kuspy anaweza tu akiamua.
Nakubaliana na wewe lakin sio rahis kama kwenye android. Huko kuna application nyingi na zinapatikana kirahis sana. Kwa mfano ili udownload app kama hizo blackberry utatumia mda mrefu na nyingi ni za kulipia tofaut na android au Os.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom