Rugaijamu
JF-Expert Member
- Jul 10, 2010
- 2,942
- 1,294
Asante Mjomba, umeiweka vema sana hii kitu. Hawa watoto hawajawahi kujenga.Watu mnabwabwaja tu ili muonekane wazee wa viwango, ni aidha mnaishi kwa shemeji hamjui kitu au lengo lenu ni kukatisha tamaa wenzenu!
Mfuko tofali 19!!!!
Mara tofali 25!!!
We unafikiri hiyo tofali ungeuziwa 1000-1200? Mpigaji angefanya biashara kichaa namna hiyo!
Tofali zote unazoona zinauzwa mtaani huko ni wastani wa zaidi ya 40, na kila siku unaona zinaondoka na maghorofa yanainuka... jipe muda kuwauliza wapigaji japo wanaweza wasikwambie ukweli.
Huu mjadala wa ujenzi upo juu ya uwezo wenu hivyo mlipaswa kuuamkia na kukaa kwa kutulia.
Mfuko wa simenti kwa tofali za ujenzi wa nyumba, 32.5R au 42.5R inatoa tofali 40-50 tena ni zenye ubora wa kiwango cha juu.
Na huyu ni mpigaji wa mikono, kwa mashine zinaweza kuzidi hapo na zikafaa tu.
Acheni ubishani na mizaha, hii ni moja ya sababu mnaogopa kujenga.
Kwenye uimara wa Tofali mbali ya ratio ya mchanga na simenti, pia utaalamu wa Fundi kwenye uchanganyaji una nafasi kubwa pia.