Anko Elly
Member
- Feb 22, 2017
- 69
- 70
Habari za asubuhi The Great Thinker wa jukwaa hili adhimu la Teknolojia. Matumaini yangu kuwa hamjambo na mnaendelea vizuri katika suala zima la upambanaji.
Kilichonileta leo kwenye hili jukwaa ni mambo mawili, Mosi ni kuhitaji msaada wa kueleweshwa kuhusiana na Sony Home Theatre System na kingine ni Ram ya Laptop yangu.
Nikianzia kwenye suala hili la HTS(Home Theatre System) za Sony nimejaribu kufanya Research kuona ni ipi yenye nguvu na bora zaidi.
Katika Research yangu ndogo nikagundua kuwa zipo za madaraja mbalimbali kuanzia 350, 650, 950 hapa nazungumzia nguvu ya mziki. Mfano hizi za 350 huwa na Speaker ndogo jumla 5 wakati hii ya 650 huwa ni zile speaker ndefu 4 na ndogo moja halikadhalika na 950.
Sasa swali langu ni kwamba nimetokea kuipenda hii yenye nguvu ya 950 sema zipo za aina mbili, moja ni ile yenye wireless speaker na nyingine Speaker zake unatumia wire kawaida.
Msaada naohitaji hapa kuweza kufahamishwa juu ya hizi Speaker za Wireless, kwa wale walioweza kutumia hasa katika ubora wake na Je, huwa zinakuwa na changamoto gani? Maana nimekaa nikaona kabla sijanunua nije huku kuomba msaada.
Mwisho kabisa nahitaji kujua bei ya RAM ya Dell Latitude E6410 8GB ni kiasi gani? au kama kuna mdau anauza ambayo ni mpya na sio Used anijuze hapa jukwaani kwa manufaa ya wengine na tukiafikiana bei tuweze kufanya biashara.
Nawasilisha wakuu