msaada kuhusu hii error "unknown filesystem"..

Skillseeker

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
225
34
habari zenu wakuu. Naombeni mnisaidie..kuna mtu amenipa laptop yake nimsaidie mpya ya lenovo nimsaidie kuweka baadhi ya programs na kumake sure everything kiko sawa then nimrudishie..ile laptop wakati naiwasha ilionekana kuwa na OS mbili (windows7 & linux).Hii version ya linus sijui ni ipi lakini nilihisi ni fedora. Sikuhangaika na linux sababu huyo mtu ni mtumiaji wa windows tu sema alipewa hii laptop ikiwa na linux. nilimuwekea antivirus,browser,vlc,video converter,burner na software nyingine muhimu ambazo ni zakawaida kwa matumizi ya kila siku.

baada ya hapo nilifungua my computer nikaona partition tatu lakini moja ilikuwa inakataa kufunguka kabisa na nilipojaribu kuiformat kwa kuright click then format ikakataa. basi nikaamua niende kwenye diskmanagement nikaiformat ikakubali. niliporudi kwenye my computer nikakuta ile partition iliyokuwa inakataa bado inaonekana na kuna hii nyingine ambayo ndo mpya nimeformat(inatotal space ya kwenye previous partition iliyokataa). nilivyozima laptop baadaye na kuiwasha tena nikakuta error inasema "unknown filesystem" alafu baada ya hapo ikaandika "grub rescue>".
baada ya kutafakari kuhusu hii error nikakugundua nitakuwa nimeformat partition ya linux so nimefuta bootloader. hii imenishangaza kidogo kwa sababu nilishawahi kutumia ubuntu na windows pamoja lakini kila nilipoingia kwenye windows sijawahi kuona partition ya ubuntu na ndiyo maana hata sikudhani kuwa ile partition iliyokuwa inakataa ni ya linux.

sasa naombeni msaada jinsi gani ya kusolve hiyo error ili niweze kuaccess windows7 na kuitumia kama kawaida.
 
hiyo laptop kama ni mpya inawezekana ikawa na ile internal recovery partition, jaribu kuizima then press f8 mara nyingi wakati inawaka (hapa ittegemeana na model ya pc...jaribu ku press key mbalimbali kama f8 haitakubali) ukifanikiwa kuingia kwenye repair unafanya factory recovery tu...kama hamna hii partition then itabidi uanze kufanya makeke ya kupata cd ya win7 ufanye repair tu mkuu kwa uhakika zaidi...
 
Back
Top Bottom