Msaada kuhusu elimu na Vyeo Jeshini

Msaada kuhusu elimu na Vyeo Jeshini

Labda kama taratibu zibadilishwe sasa... ila wote naowafahamu wameingia na Degree zao moja... wametoka na nyota moja moja... zikatoka kozi wameenda sasa wana nyota mbili mbili...

Cc: mahondaw
Ilikuwa kabla ya Jiwe kuingia yani Jamaa JK aliwapa shavu snaaa ila jiwe lilipokuja ooho Mambo sio kabisaa
 
😀 😀 😀 Nakumbuka cuz tulibebwa kilazima af siku ile watu hatukulala, ni kukabidhiana mabunduki na kulinda usiibiwe
sasa kuna kitu inaitwa Heavy heart na kaza viungo siku ukikutana nazo utajuta kupafahamu jeshini
 
Duuh hii hatari ninachojua mimi Unaenda na basic education labda ya Form six ulisoma PCM then unaenda kusomeshwa uingeneer wa Mitambo ya vita hapo sawa lakini sio Form four eti uruke uende mpaka Eng duuh... Ndo maana wanafunzi wa vyuo na form six wanakuwa na chance kubwa zaidi maana kumuendeleza form four au la saba akasomee uingeneer ni balaaa.. hana msingi mzuri kuhusu hayo masomo so ni ishu sanaa
Hata kwa yule ambaye uraiani amesomea degree ya uhandisi ila jeshini akataka akasomee urubani pia inawezekana?
 
Kwahiyo wote ambao ni wanajeshi hawajawahi kuulizia mishahara jeshini?
wanaulizia ila sio swali namba 1...siku zote mwanajeshi kweli hawazi mshahara anaulizia na kuwaza Kilichomfanya atamani kuwa mwanajeshi kisha ndio ktk story za kupoteza time Atauliza kuhusu mshahara.
 
Huyo mdogo wangu yeye jeshi analipenda na wala hauliziagi mshahara ila mimi ndo nimeona nimsaidie kuuliza humu na kama umesoma uzi wangu vizuri nimesema ningependa kujua mishahara pia kama ikiwezekana

Yaani hilo swali lilikuwa la nyongeza tu ila muhimu ilikuwa ni kujua kuhusu elimu na vyeo kama kichwa cha habari kinavyojieleza na ofcourse mimi siyo mwanajeshi na aliyeuliza hilo swali ni mimi na si yeye na kama umesoma vizuri sijaliweka swali namba moja
wanaulizia ila sio swali namba 1...siku zote mwanajeshi kweli hawazi mshahara anaulizia na kuwaza Kilichomfanya atamani kuwa mwanajeshi kisha ndio ktk story za kupoteza time Atauliza kuhusu mshahara.
 
Labda kama taratibu zibadilishwe sasa... ila wote naowafahamu wameingia na Degree zao moja... wametoka na nyota moja moja... zikatoka kozi wameenda sasa wana nyota mbili mbili...

Cc: mahondaw
Ndicho kilichopo na nimekisema mwanzo kabisa sasa hivi degree sio inshu jeshini na zilikuwa zinapigwa vita kwa sababu hiyo.
.
Sasa hivi ukiingia jeshini na degree yako sijui ya sheria sijui education utajiona huna tofauti na darasa la saba walioingia jeshini zamani utaanza na ukoplo au sajini
 
Yeah hilo sawa ila nilikuwa nauliza kwa mfano mtu hajawahi kabisa kusomea uhandisi yaani tuseme uraiani kasomea unesi halafu akaenda jeshini je inawezekana akasomea uhandisi huko jeshini kitu ambacho hajawahi kusomea hapo kabla?
Ndio inawezekana kabisa anafata tu utaratibu, unaotakiwa kama anachokwenda kusomea kipo ndani ya mpango wa jeshi anapewa na ruhusa kabisa nilikuwa na rafiki yangu mjeda tulisoma nae chuo safi kabisa no shida.
 
Ndicho kilichopo na nimekisema mwanzo kabisa sasa hivi degree sio inshu jeshini na zilikuwa zinapigwa vita kwa sababu hiyo.
.
Sasa hivi ukiingia jeshini na degree yako sijui ya sheria sijui education utajiona huna tofauti na darasa la saba walioingia jeshini zamani utaanza na ukoplo au sajini
Unajua kazi za majeshi zilikuwa zinadharaulika sana zamani baada ya mambo kubana wengi wakakimbilia huko so promotion zilikuwa za kutosha hali hii iliamsha morale ya in service kujiendeleza pia!! mwisho wa siku degree zipo kibao jeshini, swali utawapeleka wote vyeo?? Bureaucracy in kataa hapo. Kwa mana hiyo lazima upepo ubadirike. Kwa hiyo mkuu wengi hawalijui hili wanaishia kukariri tu ukiwa na degree lazim uwe officer some thing wrong!
 
Mpaka mi naondoka niliacha mambo yakiwa hivi..

Form 6 - nyota mbili (luteni) kuna mtu namjua kapata hicho cheo.

Bachelor degree - nyota tatu (captain).

Lazima apite Jkt miezi 6 ya kujitolea, baada ya hapo atapiga kozi ya TPDF yaani bakabaka kwa muda usiopungua miezi 4 hadi 6. Baada ya hapo ndio ataenda monduli kupiga kozi ya cadet officer kwa muda miezi 9. Baada ya mlolongo wote huo ndio ataweza kuwa afisa wa jeshi.

Kuhusu mshahara nakumbuka captain wetu aliyekua na nyota 3 alikua anachukua m3 kasoro hivi, kutokana na kauli mwenyewe. Na wenye nyota 2 inacheza kwenye m2 mbili kasoro point kidogo (kwa hapa am not sure).

Naongea from my experience ya miaka 5 nyuma, labda mambo yabadilike hivi sasa.

I hope nimesaidia.
Kwanza atambue degree sio kigezo cha kupata nyota,na ni elimu ya kawaida sana Jeshini,wapo wengi mno.Anaweza akapita kote, kuanzia Jkt,Tpdf na akafika kozi ya uofisa akachemka.Namshauri kama ataingia jeshini aingie tu,asijiwekee atakuwa nani huko mbeleni,hayo yanakuja tu.Hata asipokuwa afisa bado atakuwa vzr tu sio lazima awe afisa.Akienda na akili hiyo tangu awali atachemka tu.
 
Huku kwetu nmeona sanasana ambao wanaenda kwenye hizo OP ni kuanzia rank ya Major kushuka chini yaani Captain, Leutenant na kuendelea kushuka chini. Ila kuanzia Leutenant Colonel, Colonel na kuendelea kule mbele sijaonaga kama wanaenda OP
Wa huku kwetu huwa hawaendi kabisa?
 
kwa wasiojua JWTZ kuna kila taaluma kuna maproffessor na watu wa PhD wengi tu.
Mfano waligoma waongoza ndege hawa jamaa wakaingia kusaidia
.Wakagoma Ma Dr Muhimbili hawa jamaa wakaingia kusaidia.
Ninachowapendea hawa jamaa sio watu wa rushwa wao ni amri.
 
Unaanza uzalendo, ukuruta, service man/girl, bakabaka, then inakuja course ya maafisa anaenda. Ila mambou yamebadilika inaweza chukua muda kupata nyota. Kulingana na nlivyopita mujibu wa sheria, 😜 😜 😉Elimu ya kidato cha sita ni tosha kwenda officers cadett course. Zamani ilikuwa waliomaliza form six ni lazima kwenda JKT mujibu wa sheria, na ukiwa kwenye mafunzo mnapewa nafasi ya kujiunga jeshi kwa anayetaka. Hivyo baada ya miezi sita ya ukuruta unarushwa Chuo cha maafisa Monduli, kule ukimaliza unaanza na nyota moja( luteni usu)
 
Utaratibu sasa hivi umebadilia

MOJA: Askari anayetakiwa awe na nyota kwa UMRI ni chini ya miaka 23 kushuka chini,kwa experience yangu Uncle angu mda huu anapiga hiyo course ya uafsa.

MBILI: Hata kama utakuwa na Masters ni lazima uanzie chini yani nyota moja lakini kabla ya hapo utaratibu ulikuwa mwenye degree mfano ya MD atachukua nyota tatu.

TATU: course ya Uafsa ni miezi 9 na sio chini ya hapo.

Nb: Kuna uncle wangu mkubwa ana elimu ya form six lakini hakupata cheo chochote ila alivaa UKOPLO kwa Sababu ya fani yake CLINICAL OFFICER.

Jeshini usipokuwa na refa utapiga mihayo Sana utashangaa wa darasa la saba anavaa bakabaka ila mwenye Degree ya Engendering anarudi nyumbani.
Sidhani. Ukifaulu tu utapata nyota moja. Nyota ya pili hutolewa kwa bidii kazini, nyota ya tatu kitabu major bidii, lt col kitabu, col bidii ndio wanavyofanya. Baada ya hapo wanaenda chuo cha viongozi ft Ikoma
 
Utaratibu sasa hivi umebadilia

MOJA: Askari anayetakiwa awe na nyota kwa UMRI ni chini ya miaka 23 kushuka chini,kwa experience yangu Uncle angu mda huu anapiga hiyo course ya uafsa.

MBILI: Hata kama utakuwa na Masters ni lazima uanzie chini yani nyota moja lakini kabla ya hapo utaratibu ulikuwa mwenye degree mfano ya MD atachukua nyota tatu.

TATU: course ya Uafsa ni miezi 9 na sio chini ya hapo.

Nb: Kuna uncle wangu mkubwa ana elimu ya form six lakini hakupata cheo chochote ila alivaa UKOPLO kwa Sababu ya fani yake CLINICAL OFFICER.

Jeshini usipokuwa na refa utapiga mihayo Sana utashangaa wa darasa la saba anavaa bakabaka ila mwenye Degree ya Engendering anarudi nyumbani.
Kuna suala la afya na utimamu wa mwili,uvumilivu nk.
 
Back
Top Bottom