Niaamini unamaanisha hupati free traffic kutoka search engine
Nimefanya reverse DNS lookup ya hiyo top level domain na kuona inamilikiwa na kampuni kubwa tuu na ilianzishwa tarehe 04 ya machi mwaka 1995 ikimaanisha kuwa hii domain webs.com ni 'very old' kwahiyo indexing siyo tatizo.
Pia nimeangalia hiyo subdomain yako bongoland.webs.com kwenye google nakukuta ipo indexed lakini only two pages.
Sasa hii inamaanisha nini?
Ni kwamba tatizo siyo kwamba domain ni mpya (yaani haina relationship na google) bali tatizo ni links. Kuwa na relationship na google ni kuwa google inaamini kwamba website yako ina authority online. Google wanakitu kinaitwa trustrank yaani wakikuamini kwamba unatoa taarifa sahihi (relevence) watataka kuijua website yako zaidi (spidering your pages more) na baadae kukuorodhesha kwenye indexing yao. Na hapo ndipo watu wakitafuta "
Usher, Rihanna waacha maswali" kwenye google lile bandiko lako litatokea na wao watabonyeza na kujakwenye blog yako.
Sasa kama mtazamaji alivyokuambia hapo juu ni lazima ujiulize dhumuni lako ni kulenga akinanani (target audience)? kwasababu hata kama utatumia paid traffic (mf google adwords) kama shabaha yako haieleweki basi utakuwa unacheza makidamakida.
Ukienda u-turn.co.tz utaona wao wanalengaa mambo ya ulimbwende na mahusiano na wanaume weupe.Sasa hiyo ni shabaha ya uhakika (well defined target) na mlengwa akiona tuu hiyo blog anasema, 'this is it!"
Kwahiyo nakushauri uangalie upya nini unataka kufanya kwakurudia kusoma bandiko la mtazamaji. Pia kama unaweza andikisha domain yako mwenyewe ni $2 tuu kwa mwaka na ni kama $30 kwa mwaka kwa shared hosting. kam hiyo iatakushinda naweza kukupa free hosting kwenye reseller account yangu.
Ukisha maliza hayo nitakusaidia kutengeneza links, unajua, wakati Larry Page na Sergei Brin (google guys) wanafanya paper yao ya backrub pale Stanford university walitengeneza algorithm ya ku-analise links (the more the links the the page has higher the ranking), hayo mambo yalibadilika baada ya akina sisi kuabuse google system. Hata hivyo , japokuwa mambo yamebadilika sana lakini bado kama una-links nyingi kwenye page yako basi google wata kurank higher katika search engine result pages (serp).
Sasa utapataje link?
Unaweza kuomba mtu mwenye blog (yenye walengwa kwama wako) kulink kwako mfano unaweza kumuomba kaka michuzi, dada chemi au dada mage n.k. Tatizo la njia hii ni kwamba inachukua muda mferu sana na hakuna uhakika wa kupata 'linkback'.
Sasa utafanyaje?
Welcome to the world of blackhat seo my friend
Unalazimisha kutengeneza links kwa kutumia software. Kuna platform zinazo ruhusu kuweka links kwenye blogs zake, mfano wordpress blogs. Nimeona katika blog yako kunawatu wanne wame-comment kwenye hii post:
Usher Raymond Wa Bongo, Is this man lookin like Usher?? Toa Maoni yako!!
Sasa kama hiyo blog ingekuwa ni wordpress na hao jamaa wange kuwa 'badass' like me ((LOL)) wangeweka 'anchor keyword' ya website badala ya majina jao. Na hapo watakuwa wame-optimise page with an anchored link. Ieleweke hii inafanyika kwa kutumia software/script na wala siyo eti mtu nakaa na kufanya hivyo manually.
Nitaishia hapa kwa leo ili usijeogopa bure.