Msaada: Kaka yangu anaombwa rushwa ili kusainiwa cheki ya mafao yake NSSF

Siku hizi JF ukitaka upate msaada labda uulize jinsi ya kumfikisha mwanamke kileleni......au jinsi ya kusugua papuchi kwa muda mrefu.....lakini si katika mambo ya msingi kama haya.......

Maana yake ni kwamba wajinga na wapumbavu wameongezeka....hivyo watu wenye busara wameona si vyema kujiweka karibu na wajinga na kujiweka pembeni.....

Zamani JF ilikuwa kisima cha maarifa sasa hivi nj kisima cha ujinga.....

Taarifa hizi ziwafikie mods....jf irudi katika misingi yake

Malalamiko ya mtoa mada yanaweza kumkuta mtu yeyote yule...hivyo mchango wa uzi huu ungeleta manufaa makubwa sana.,,,
Ushauri wako je?
 
Ushauri wako je?

Ushauri wangu ni kwamba watu waache kuchangia kama vitu hawana ufahamu navyo.....

Mtoa mada amwambie kaka yake kama amekereka na jambo hilo aende sehemu husika zinazoshughulikia kero hizo.....achukue hatua sahihi......

Yeye awe mfano wa kupambana na kile ambacho ni kero kwa watu wengi.....anaweza akaibuka shujaa na kuwa fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia mbaya kama hizo.....
 
Awagawie wenzie kidogo hayo Mafao wenzie wakalipe Ada za Watoto wao,,
Mshauri ndg yko aache Uchoyo Ajue Mungu anamuona.
 
Hundi za NSSF kwa Uzoefu wangu huwa zinasainiwa kwa Mkupuo then ndio zinakuja kugawiwa Dirishani sasa jaribu kumuuliza vizuri ujiridhishe Kama tatizo ni kweli kusainiwa Hundi au labda kakutana na Matapeli wakamwambia kuwa wanaweza kumsaidia kupata Malipo yake ya fao la kujitoa
 
Daah hizi issue za mafao zinanikera sana ni bora iwekwe hiyari kujiunga na hii mifuko maana imepoteza dira na kubaki kusupport wanasiasa na serikali kwa pesa zetu, mwenyewe akiaangaika na nenda rudi nenda rudi.
 
Habari wana jf,
Natumai mko salama.

Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu.
Kaka yangu anasumbuliwa sana kulipwa haki yake na hawa watu wa nssf, baadhi ya maofisa wanamlazimisha atoe rushwa ilicheki yake iweze kusainiwa, kitu ambacho amegoma.

Hivyo, kwa makusudi kabisa wanamsumbua na kumuhangaisha kwa muda mrefu sana.

Najua humu kuna watu wa aina mbali mbali na ninaamini mnaweza kumsaidia kaka yangu kupata 'haki yake'.

Tafadhali, nawasihi naombeni ambao mnayo nafasi kwenye eneo husika mumsaidie kaka yangu.
Natanguliza shukrani
Jamani watzanania jifunzeni kusimamia haki yako haki yako! hayo mafao ya NSSF ni haki yako ni siyo fadhila. hata unaponda kuyadai uyadai kama haki yako na sio fadhila. Mi nimekwishapata mara 3 baada ya kufanya kazi sehemu 3 mbalimbali na sikutoa senti tanoooooooo! dai with authority. Kuna uongozi wa juu. Omba kuuona huo ili upate hakli yako. kuna vyombo vingi , TAKUKURU, Pilisi nk. Ukweli sikuelewi kabisa tena wakati huuu!
 
Habari wana jf,
Natumai mko salama.

Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo juu.
Kaka yangu anasumbuliwa sana kulipwa haki yake na hawa watu wa nssf, baadhi ya maofisa wanamlazimisha atoe rushwa ilicheki yake iweze kusainiwa, kitu ambacho amegoma.

Hivyo, kwa makusudi kabisa wanamsumbua na kumuhangaisha kwa muda mrefu sana.

Najua humu kuna watu wa aina mbali mbali na ninaamini mnaweza kumsaidia kaka yangu kupata 'haki yake'.

Tafadhali, nawasihi naombeni ambao mnayo nafasi kwenye eneo husika mumsaidie kaka yangu.
Natanguliza shukrani
Mwambie apige simu na. 113 ajieleze watampa maelekezo ya kuwakamata hao mafisi na yy atasaidiwa bila kutoa chochote, hiyo ni haki yake, hayo mafisi yanalipwa mshahara
 
asaidiwe nini wakati ni haki yake na huyo mfanyakazi ni wajibu wake kushughulikia swala la mafao.
najua ni haki yake na huyo mfanyakazi ni wajibu wake,lakini ndio hivyo anasumbuliwa. kama hataki kusumbuliwa atoe pesa,,ukitaka kula na wewe lazima uliwe kidogo.
 
najua ni haki yake na huyo mfanyakazi ni wajibu wake,lakini ndio hivyo anasumbuliwa. kama hataki kusumbuliwa atoe pesa,,ukitaka kula na wewe lazima uliwe kidogo.
ifike mahali kila mtu afanye wajibu wake.........kaajiliwa kwasababu hiyo, kama anaona shida aache akafanye vitu vingine, pesa yangu si kwamba nataka mkopo afu nikupe hela kisa usumbufu. sikupi ng'ooo

huyo ni kumpelekea TAKUKURU basi.
 
Siku hizi JF ukitaka upate msaada labda uulize jinsi ya kumfikisha mwanamke kileleni......au jinsi ya kusugua papuchi kwa muda mrefu.....lakini si katika mambo ya msingi kama haya.......

Maana yake ni kwamba wajinga na wapumbavu wameongezeka....hivyo watu wenye busara wameona si vyema kujiweka karibu na wajinga na kujiweka pembeni.....

Zamani JF ilikuwa kisima cha maarifa sasa hivi nj kisima cha ujinga.....

Taarifa hizi ziwafikie mods....jf irudi katika misingi yake

Malalamiko ya mtoa mada yanaweza kumkuta mtu yeyote yule...hivyo mchango wa uzi huu ungeleta manufaa makubwa sana.,,,
Hapana kaka watu wamekuwa na upeo mdogo sana yaani mtu anadaiwa rushwa haujui achukue hatua gani?? maana yake hajui chochote kuhusiana na takukuru wala police.

Watu wamebweteka sana, kuna vitu general tunatakiwa tuvijue ili vitusaidie katika maisha yetu ya kila siku
 
ifike mahali kila mtu afanye wajibu wake.........kaajiliwa kwasababu hiyo, kama anaona shida aache akafanye vitu vingine, pesa yangu si kwamba nataka mkopo afu nikupe hela kisa usumbufu. sikupi ng'ooo

huyo ni kumpelekea TAKUKURU basi.
TAKUKURU si hadi awe na ushahidi, kama hana atasumbuliwa napo...
 
Back
Top Bottom