Msaada aliyewahi kupata mafao yake ya NSSF kabla ya kustaafu, baada ya kuachishwa/kuacha kazi

KABAKA28

Senior Member
Jun 18, 2014
197
188
Habari wana Jf, mimi ni member since 2016 nimekua nikichangia mada mbali mbali na nimekua nikisoma pia nyuzi za watu.

Leo naomba kuleta kwenu swala la mafao ya NSSF kwa vijana wanao amua kuacha kazi ya kuajiriwa na kutaka kuishi maisha mengine wanawezaje kupata mafao yao? Ngoja niende kwenye point.

Mimi nimefanya kazi kwenye shirika linalo jihusisha na miradi ya utafiti hapa Dsm kwa muda wa miaka 4, miradi imeisha na shirika limefungwa,

Kwa muda nimekua nikijipanga kustaafu baada tu ya shirika hili kufungwa, nina biashara yangu ndogo ninafanya,

Nilitamani nipate hela yangu ya NSSF ili niweze kuongeza mtaji maisha yaende, sasa mara kadhaa nimekua nikienda ofisini kwao naishia kupata statement tu.

Waliniagiza nikachukue certificate of service na barua inayo onesha kua sina mkataba na shirika hilo, nimefatilia sana kupata hiyo barua ila imeshindikana ( nimekua nikipewa majibu ya kesho kesho kesho....)

Jamani ukinyimwa barua ya namna hiyo na mwajiri wako unapaswa uende wapi kushtaki?

Na je haiwezekani kupata haki yangu mpaka niwe na hiyo barua?

Kwa yeyote ambae anaweza kunisaidia, kama ni wakili au mtu mwenye uzoefu, nitatoa details zote na nitampa compassation pindi nikifanikiwa kuipata hela yangu.

Asante
 
Kwa uzoefu nilionao siku hizi kuna mafao ya aina tatu kwa wale wanaokoma ajira kwa kuachishwa au kustaafu kama ifuatavyo:-

1: Kustaafu kwa lazima ni miaka 60.

Kwa yule ambae amechangia miezi 180 na kuendelea mfuko wa NSSF atalipwa pensheni mkupuo na kila mwezi.
Kwa yule ambae amechangia chini ya miezi 180 atalipwa kwa formula nyingine ya mkupuo. (Sio Pensheni).

2: Kustaafu kwa hiari Miaka 55 -59 (Wanawake 54 - 59): Hawa watalipwa kama wastaafu kwa lazima kulingana na uchangiaji kwenye mfuko isipokuwa kuna asilimia kama sikosei 3.6% itakatwa katika kukokotoa mafao yake.

3: Kwa anaeachishwa kazi kuna makundi mawili nayo ni:-
3A: Wale wasio na taaluma (Unskilled): Watalipwa michango yao yote (Fao la Kujitoa)
3B: Wale wenye taaluma (Skilled): Watalipwa fao la kukosa ajira asilimia fulani kila mwezi kwa muda kama sikosei miezi sita.

Katika hatua zote tatu hapo juu uthibitisho wa barua ya mwajiri ni lazima.

Kwa wale ambao wameacha kazi wenyewe na hawajatimiza umri wa kustaafu (iwe kwa lazima au hari) taarifa nilizonazo ni kwamba NSSF haitawajibika kuwalipa.

Nimewasilisha kwa uzoefu nilionao wachangiaji wenye taarifa sahihi nakaribisha marekebisho iwapo nimekosea.
 
Asante mkuu, nimekuelewa, mimi kazi niliyo kua nafanya imeisha....

Na sihitaji kuajiriwa tena, sijafikisha miaka 55 wala 60.

Nipo kwenye category ipi? Mchakato huwa unakadiriwa kuwa wa muda gani mpaka upate mafao? (Kama una kila kitu kinacjohitajika)

Na je atakiwa kufanyaje endapo mwajiri wako anakucheleweshea barua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana Jf, mimi ni member since 2016 nimekua nikichangia mada mbali mbali na nimekua nikisoma pia nyuzi za watu.

Leo naomba kuleta kwenu swala la mafao ya NSSF kwa vijana wanao amua kuacha kazi ya kuajiriwa na kutaka kuishi maisha mengine wanawezaje kupata mafao yao? Ngoja niende kwenye point.

Mimi nimefanya kazi kwenye shirika linalo jihusisha na miradi ya utafiti hapa Dsm kwa muda wa miaka 4, miradi imeisha na shirika limefungwa,

Kwa muda nimekua nikijipanga kustaafu baada tu ya shirika hili kufungwa, nina biashara yangu ndogo ninafanya,

Nilitamani nipate hela yangu ya NSSF ili niweze kuongeza mtaji maisha yaende, sasa mara kadhaa nimekua nikienda ofisini kwao naishia kupata statement tu.

Waliniagiza nikachukue certificate of service na barua inayo onesha kua sina mkataba na shirika hilo, nimefatilia sana kupata hiyo barua ila imeshindikana ( nimekua nikipewa majibu ya kesho kesho kesho....)

Jamani ukinyimwa barua ya namna hiyo na mwajiri wako unapaswa uende wapi kushtaki?

Na je haiwezekani kupata haki yangu mpaka niwe na hiyo barua?

Kwa yeyote ambae anaweza kunisaidia, kama ni wakili au mtu mwenye uzoefu, nitatoa details zote na nitampa compassation pindi nikifanikiwa kuipata hela yangu.

Asante
mkuu vip ulipata hela yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina ujuzi sana ila nachokijua ni kua kama si profesheno ela yako unapata yote inategemea na cheo, ujazaji form......

Kama ni profesheno ukidai ela yako utapewa asilia 33 ya mshara wako kwa miezi 6...
Na baada ya miezi 6 NSSF watasubiri miezi 18 kuona kama umeajiriwa tena kwa maana kuanza kupokea michango mipya ya uko uliko ajiriwa

Kama awatoona basi utapewa mpunga wako wote....
 
Nilipata, wakawa wanahitaji certificate of service, hapo mwajiri ndo alipo nitoa baru, eti hua zinatolewa kwa muda maalum (Baada ya miaka mitano) wanaitwa watumishi walio staafu na walio acha kazi wanapewa kama zawadi na kunakua na hafla
 
kama ulikuwa mshahara wako ulikuwa 1m kwahyo utapewa 333000? na vip wanaa calculate kwenye gross salary au take home?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
form zote ulisha kamilisha kwa bado hela kuingia kwenye ac tuu? au umekwama kwenye process

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani sikujaza fomu yotote. Nilienda NSSF kuuliza utaratibu wakaniambia nahitaji barua ya termination of contract na certificate of service, hapo ndo nilipo kwamia, maana mwajiri wangu hajanipatia hivyo vitu, sijui wapi pa kushtaki
 
Nilipata, wakawa wanahitaji certificate of service, hapo mwajiri ndo alipo nitoa baru, eti hua zinatolewa kwa muda maalum (Baada ya miaka mitano) wanaitwa watumishi walio staafu na walio acha kazi wanapewa kama zawadi na kunakua na hafla
kama huna hiyo unapeleka mkataba wa kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkataba wa kazi niliwapelekea wakagoma kaka, labda kama kuna mtu humu ndani anaweza kunisaidia nikapata haki yangu, hata pa kushtaki tu, ili nipewe stahiki zangu, nitashukuru sana
 
Yaani sikujaza fomu yotote. Nilienda NSSF kuuliza utaratibu wakaniambia nahitaji barua ya termination of contract na certificate of service, hapo ndo nilipo kwamia, maana mwajiri wangu hajanipatia hivyo vitu, sijui wapi pa kushtaki
nenda idara ya kazi ya mkoa ilipo hiyo kampuni ukawashtaki watakupa vitu vyako vyote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taasisi yenyewe nikikutajia hapa utanaki mdomo wazi, ni kubwa na adirifu kinoma, ila ina madudu ya kufa mtu. Ni hapa Dar es Salaam, ofisi zao ziko wapi?
 
Back
Top Bottom