Msaada jamani! Yamenifika

Msaada jamani! Yamenifika

Watu mna roho mbaya.Mpeni kijana moyo.Ukichunwa siku ukija kupewa ndio itakuwa tamu hasa because you deserve it baada ya kuhangaika sana.Usimsikilize Preta.
 
pole sana kjana mwenzetu, kwa uelewa nilio nao kwa hao mabinti wa saluni ni waongo vibaya sana kwanza ni wapiga mizinga hatari so achana nae anakutia umaskini
 
Hilo nilimuuliza akajibu simple kua asingekua ananitafuta mara kwa mara

Basi sawa,next time akipiga shampoo imeisha mwambie akuvumilie mambo hayako sawa,ukichomoa Mara tatu tu na namba yako atafuta!
Usiogope kulia kwake bwana,alilia hospital ndio maana mama yake akapewa alipozaliwa.
 
Kweli Mapenzi hayana adabu,,,,,kwamba shy na mikoa jirani hawajamuona huyo mdada mpaka uje umkute wewe wa dar???

hahahaha mkuu umenichekesha san, ila ni kweli maneno yako yana mashiko sana mana shinyanga napo kuna mijembe ya hatar wameshiba haooooo
 
hahahaha mkuu umenichekesha san, ila ni kweli maneno yako yana mashiko sana mana shinyanga napo kuna mijembe ya hatar wameshiba haooooo
Ndio ushangae sasa,,,, shy wale wachunga ng'ombe wameshiba vile ndiyo aje amkute yeye wa dar
mla chips na mayai yasiyo na jogoo?,,,,
 
Asanteni sana, kweli nimewaelewa kwa ushauri wenu.....huyo "J" basi tena.
 
Nawasalim wana MMU,

Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa MMU na nimepata kujifunza mambo mengi sana lakini kuna jambo limenitokea naombeni ushauri wenu.

Kwa sasa ninaishi Dar nimetokea kumpenda mdada mmoja yuko Shinyanga (ndiko anakoishi), kwa sasa yapata miezi saba tokea tujuane (tulikutana Shinyanga nilienda kusalimia ndugu); mimi ninafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi (temporary) na huyu dada anayo saloon ya kike hapo shinyanga mjini.

Tatizo langu linakuja kwenye suala la pesa; kwani kila mara nikipokea simu yake baada ya kujuliana hali anaomba pesa mara shampuu na mafuta mengine zimeisha za saloon mara nimtumie pesa za matumizi mara wateja wamepungua sana anadaiwa kodi la nyuma (saloon).

Yote hayo yaweza kua sahihi lakini linapokuja suala la mafuta na shampuu huwa nashindwa kuelewa make haviwezi kuisha bila kuingiza pesa kwani zinatumika kwa wateja, pili kwa nini anapiga simu akiwa na shida la pesa tu? yungali tuko wachumba?

Mimi nilishamweleza hali halisi ya kipato changu na msaada ambayo twaweza kusaidiana, lakini niliona kama hajaelewa make alikua akipiga simu analalamika mithili ya mtu anaelia kitu ambacho sipendezwinayo. Kutokana na hiyo hali nilipanga safari adi Shinyanga wiki mbili zilizopita wala sikuona hali mbaya sana kwenye saloon yake, kurudi Dar baada ya wiki moja ameanza tena mara anataka kuleta mfanyakazi anejua kusuka vizuri kwa hiyo nimsaidie kulipa mara amepata chuo uku Dar kuna kozi anataka kuja kusoma nimchangie,,jamani!

Naombeni ushahuri huyu mdada anayo nia nzuri na mahusiano YETU? au anataka kula PESA na kusepa?
MUHIMU: SIJAWAI KUFANYA NAE MAPENZI

yaani hapa pamenimaliza nguvu nlichotaka kushauri kimeyeyuka
 
Unakuta jamaa kapenda kweli kweli!

Sometimes mi naona udwanzi kujiachia kwa mtu simply because ukipenda unatendwa!
 
Unalisha mbuzi ya jirani.


Hahahahahahahaahah,

Hivi ina maana vijana wa dotcom na ujanja wote hawawezi kushtukia deals ambazo ni magumashi?

Na uzee huu, bado naamini wachumba wa kweli huwa ni waangalifu kwenye kuomba omba fweza!

Huyo anatakiwa kufungua account Mkombozi Bank...lol!!
 
Hapo hamna mapenzi....
Kama una uwezo wewe hudumia tu , si papuchi yake anakupa ila usitarajie makubwa kivile kutoka kwenye hayo mahusiano.

Kasema mwenyewe hawajawai kubanjuka.hyo papuchi anapewaje tena?
 
Niwajuavo mim wadada kama kwel hujawah kufanyanae mapenz, kwake ni tatizo kubwa sana, anahisi una mwingine unayemthamin zaid mpaka kumvulia nguo zako! Anachokifanya sasa ni kukupiga mizinga ya adabu walau naye aambulie japo pesa tu dushe si unambaniaa!
 
Niwajuavo mim wadada kama kwel hujawah kufanyanae mapenz, kwake ni tatizo kubwa sana, anahisi una mwingine unayemthamin zaid mpaka kumvulia nguo zako! Anachokifanya sasa ni kukupiga mizinga ya adabu walau naye aambulie japo pesa tu dushe si unambaniaa!

Duuh! ya kweli haya?
 
Mtoto mjini huyo ashapata ATM yake ya muda, kimbia mtu kabla hujafulia maana atatumia mbinu nyingi za kupata pesa kutoka kwako lakini ujue wanaoombwa pesa ni wengi na pia walaji au watumiaji wa papuchi pia atakuwa nao wengi.
 
Back
Top Bottom