Msaada hii movie ya Suniel Shetty inaitwaje?

Bonge moja la story, songi lake ni la

Kuna baadhi ya movie wahindi wametuliza kichwa, shida huwa ni kwenye action tu

Nimecheki movie nyingi za kihindi uchawi majina siyajui.
 
DARR,
hii muvi amecheza sharukhan na sunny deol..
katika muvi zenye songs kali basi darr haitakosekana..

storyline..
sharukhan alikuwa anampenda mwanamke(juhi chwala)ile kufa.
hadi ikampelekea tatizo akawa(socialpath au chizi mapenzi)ajabu toka chuoni wakisoma jamaa alikuwa domo zege kumtokea demu na kumwambia anampenda.

maisha yakaenda jamaa akizidi kuteseka huku yule demu alikuwa tayari na mchumba(sunny deol)ambae alikuwa mwanajeshi wa majini.baada ya kuwa mwanamke kamaliza chuo mikakati ya uchumba na kufunga ndoa ikawa imeshika kasi.

huku sharukhan akiteseka na kuwafanyia vituko ambavyo sio vya binadam mwenye akili timamu..
alidhamiria kuua mtu yoyote atakaemsogelea yule manzi.
hapo akakutana na mbabe sunny deol.
ingawa aliteswa sana lakini mwishoni aliweza kumuua sharukhan.

ni muvi tamu sana.ingine KOYLA.
muvi za zamani zilikuwa na stori nzuri sana halafu zinaeleweka hata km hujui kigabachori
 
ROWDY RATHORE..
akshay kumar akiwa ni askari jasiri na shupavu aliweza kumaliza tatizo la ujambazi katika eneo alilopewa majukumu...
sifa zake zilitamalaki katika ngazi zote za jeshi.
hii ilipelekea ahamishwe sehemu nyingine ambapo alienda kukutana na mambo hakuyategemea!
siku amefika katika kituo cha kazi akiwa na mwanae wa kike aliposhuka kwenye tren tuu wakora wakamfata wakitaka pesa bila kujua ni mtu gani.
aliwatandika na miwa hadi wakajinyea kisha akachukua pesa zao na kuwarudishia raia walioporwa!!
akiwa amepokelewa na askari walio chini walitambua kwamba akshay alikuwa amefiwa na mke wake...

katika wale askari wake mmoja aliulizwa na akshay wee mkeo yuko wapi naona unaishi tuu na watoto..!
akaogopa kusema hadi watoto wakasema kwamba mama ametekwa!

yule askari akamwelezea kwamba kuna DON hapo kijijini amemteka mke wake na kila akienda kumdai anaambiwa arudi baada ya siku 3...yaani kibabe unamuona mke wako analiwa halafu unaambiwa njoo baada ya mda umchukue..jamaa kinyonge anaondoka..

hapo ndio visa na mikasa inaanza!
ni muvi nzuri sana.
 
Kuna muv moja inaitwa QAYAMAT umo ndan kacheza AJAY DEVGAN na SUNIL SHETTY muv balaaa sana hii Ajay alifungwa gereza ambalo miaka 1000 hajawah kiumbe yyt kutoroka kaenda yy kakaa miez3 katoroka akawafata walomsababishia kesi akawaua then akapelekwa tena jela baadae Sunil atahitaj msaada wake kuna manyamela wanasuka mipango ya kurusha nuclear kutoka katika hilo gereza asee mziki wake co wa kitoto kuna song moja Matata sana Ajay anakumbuka wakat anapelekwa uko kuwasaidia polis linaitwa Diljual Lia(sina hakika kama ni sahih)
 
usipomtaja amrish puri utakuwa hujaitendea tasnia haki kabisa...
zamani wadogo ukikataa kula tuu unaambiwa amrish puri anakuja mbona msosi utaisha huo..hahaha
Koyla. Makaa ya motoooooo.
hii dada alitupwa kwenye mto wa mamba anaitwa REKHA na muvi inaitwa KHOON BARI MAANG..
jamaa aliamua kumuua mke ili ale bata vizuri na mchepuko.huku akitumia mali na ukwasi wa mke wake.
Kuna movie inaitwa Chandni ..
Ya zamani ..sridevi ..

Halafu kuna Amar ..akabar .. Antony..amitabh bachan..

Halafu kuna movie ya Hema malini alitupwa kwenye mto wenye mamba ..nimesahau jina..

Disco dancer ..

Na kuna movie moja ya Ajay na Salman Khan
Nimeisahau jina Ila story inahusu
Ajay alimuoa dada nafikiri ni Aishwarya..kumbe Aishwarya Yuko in love na kijamaa mwanamuziki underground..ndo Salman..

Ajay baada ya kuona mwanamke alie muoa full kisirani akaona Bora ampeleke kwa hiko kijamaa..wakaenda hadi Italy wanamtafuta huyo jamaa...Ile journey ndo ikawafanya wazoeane ..wakaanza kupendana..
By the time wanakkipata kijamaa... mwanamke hamtaki tena anamtaka mumewe..

Wahindi wanajua kuandika
 
usipomtaja amrish puri utakuwa hujaitendea tasnia haki kabisa...
zamani wadogo ukikataa kula tuu unaambiwa amrish puri anakuja mbona msosi utaisha huo..hahaha

hii dada alitupwa kwenye mto wa mamba anaitwa REKHA na muvi inaitwa KHOON BARI MAANG..
jamaa aliamua kumuua mke ili ale bata vizuri na mchepuko.huku akitumia mali na ukwasi wa mke wake.
Shahrukh hiiii mkuu. Shahrukh alilishwa makaa ya mawe ili asiseme mauaji ya wazazi wake maana aliona wakiwa wanauliwa
 
Shahrukh hiiii mkuu. Shahrukh alilishwa makaa ya mawe ili asiseme mauaji ya wazazi wake maana aliona wakiwa wanauliwa
aliemlisha hayo makaa ndio amrish puri..
baba ake na sharukhan alipata madini ya thamani akamuonesha ndugu yake ambae ni amrish.kwa tamaa amrish ndio akamuua kisha kumlisha makaa ya mawe mtoto wa kakaake ambae ndio sharukhan!
kisha akawa anamtumikisha km mbwa wake!
amrish akiwa hapati msisimko kwa mke wake hivyo mganga wake wa mitishamba akamshauri atafute binti mwingine mdogo mbichi amuoe ndio hamu yake itarudi.
katika pitapita zake ndio akamuona yule binti maskini(madhuri).akatumia ushawishi wake wa pesa kisha akamuoa kwa nguvu!!
baada ya sharukhan kugundua jinsi yule binti anapitia mateso ndio akaamua kutoroka nae!kumbuka binti wakati anachumbiwa alionyeshwa picha ya sharukhan sio amrish hivyo akakubali!!

hapo ndipo shughuli pevu ikaanza hadi kufikia bubu kuongea...
 
Yea hii muvi kazi. Kinachoniuma ni muvi ambayo niliiangalia enzi za Lufufu kibandani Big M na sijawahi itafuta sasa hivi ili niielewe.

Disco Dancer nilishindwa vumilia nikaitafuta. Vishwatma haipo online, Sholar aur shabnam haipo online pia ila ilitakiwa nizipige review
Hizo movie Star Gold hua wanaonesha sanaaa!Haswaa Sholay!naielewa sana hii movie
 
Rufufu mungu anamuona aisee.. Sunil Shet yeye alikua anamuita Shurusheti.

Kuna muvi inaitwa Tere naam ya Akshay bonge moja la muvi. Napenda sana Bollywood movies sema sina pa kuzipata mpaka nikiwa na muda niangalie B4U movies. Nina nyimbo za kihindi 500 zote video usiku napenda kulala nazisikiliza
Teree naam ya Salmaan Khan Bwana!Bhaijaan anakuwa chizi
 
Yeah
tere naam ya SALMAN KHAN mpk anakuwa chizi 7bu ya demu

AKSHAY KUMAR na RAVEENA TANDON
hawa ndo walonifanya niwe mpenzi wa MOVIE za KIHINDI tangu miaka ya 94 95 hivi TV zilipoanza kuwa nyingi BONGO

katika MOVIE za miaka ya 2000 ninayokubari ya AKSHAY kuna KHAKEE humo kaupiga mwingi na AMITABH BATCHAN pamoja na AJAY DEVGAN kama kawaida Kupenda MADEM ndiko kulimponza katika MOVIEE hii
bila kusahau AJNABEE humo anacheza na BOB DEO ni baadhi ya MOVIE chache za miaka ya 2000 ambazo ndio walikuwa wanamaliziamalizia ule ubora wao
Enzi hizoView attachment 1838232View attachment 1838234

Now demu hazeeki aiseeView attachment 1838236View attachment 1838237
Khakee first time nilivoiangalia nililia aseehh!!!Mimi bwana kwa wahindi nalia kama mtoto Niko too emotional!!! Halafu nampenda Devgan ndo kawa adui daahh!Aishwarya Rai mule ameact vzr sana
 
usipomtaja amrish puri utakuwa hujaitendea tasnia haki kabisa...
zamani wadogo ukikataa kula tuu unaambiwa amrish puri anakuja mbona msosi utaisha huo..hahahah
Sisi Daslama tulikua tunamuita mzee Ashanti daah huyu baba acha kabisaa
 
Baaazigar
Shahrukh Khan
Baba yake shahrukh ana kampuni na Mali. Ameajiri watu wengi tu. Kuna jamaa alikuwa maskini ana watoto wawili wa kike. Hapo shahrukh bado mtoto kama miaka 6 hivi. Anamuajiri huyo maskini baba wa wasichana wawili (Dalip tahil). Baada ya jamaa kuajirriwa anafanya kazi anakuwa maarufu na anaaminiwa na boss (baba yake SRK). Boss anapata safari anaenda nje ya nchi anamuachia kampuni Dalip tahil. Jamaa na tamaa zake anabadili hati miliki ya kampuni na jina anabadilisha. Boss kurud Hana chake. Anabaki mtu anafilisika anakuwa maskini wa kutupwa. Katika majanga ya njaa na stress baba yake shahrukh anakufa na mdogo wake shahrukh anakufa. Anabaki mama na shahrukh mwenyewe. Alooooo, hapo bado mtoto kama 8 years. Maisha yanaenda miaka inaenda, jamaa anakulia kijijini anakuwa mkubwa 28-35 years. Anaamua kuondoka kijijini kwenda kutafuta life mjini. Anamuaga mama. Alooooo, jamaaa ana machungu. Alooo, anaomba lift kuja mjini. Anafika anachunguza adui yake. Anajua adui yake aliyemuibia baba yake kampuni anapenda michezo ya kushindana ya magari. Alooooo, jamaa anajitosa kwenye mashindano ya magari. Siku ya competition, adui yupo naye yupo. Wanashindana jamaa anaongozaa mwanzo mpaka Karibia na mwisho. Anashika brake, anamuachia adui wa baba yake ashinde. Maksuuuuudi. Adui anafurah anasheherekea na Binti yake mkubwa. Alooo, wanamfata mtaalam kuja kumpingeza. Imetick. Binti wa adui anampenda msela. Alooooo, .........msela anamtafuta Binti wa pili wa adui wanakuwa wapenzi. Alooooo, jamaa anatembea na ndugu wawili kwa wakati mmoja......interval....bonge ya movie. Unfortunately msela alikufa. Aloooooo
Kuna movie ya Hollywood nafkiri walichkua hio story.

Zamani movie nyingi za kihindi walikuwa wanachkua story za kizungu. Sema wao huongeza na manjonjo na nyimbo zao zile basi story huzidi kuwa tamu
 
Kuna movie inaitwa Chandni ..
Ya zamani ..sridevi ..

Halafu kuna Amar ..akabar .. Antony..amitabh bachan..

Halafu kuna movie ya Hema malini alitupwa kwenye mto wenye mamba ..nimesahau jina..

Disco dancer ..

Na kuna movie moja ya Ajay na Salman Khan
Nimeisahau jina Ila story inahusu
Ajay alimuoa dada nafikiri ni Aishwarya..kumbe Aishwarya Yuko in love na kijamaa mwanamuziki underground..ndo Salman..

Ajay baada ya kuona mwanamke alie muoa full kisirani akaona Bora ampeleke kwa hiko kijamaa..wakaenda hadi Italy wanamtafuta huyo jamaa...Ile journey ndo ikawafanya wazoeane ..wakaanza kupendana..
By the time wanakkipata kijamaa... mwanamke hamtaki tena anamtaka mumewe..

Wahindi wanajua kuandika
Mie nikiangalia movies za wahindi huwa nalia tu.

Huo disco dancer niliangalia mara nyingi lkn kila nikiangalia nilikuwa nalia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom