Upendo kwenye Mahusiano unaupimaje?

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
642
554
Wanajamvi,

Umofia kwenu!

Mimi ni mwanaume mtu mzima kidogo, yaani miaka 44 hv.nimeoa na nna watoto. Mwaka 2015 hapa nyumbani kwangu nilipata shida ya msichana wa kazi za nyumbani, yule aliyekuwepo alipata mchumba akaolewa.

Kutokana na majukumu tuliyonayo me na mke wangu, ilitulazimu kufanya juhudi kutafuta binti mwingine wa kutusaidia! Siku moja nikiwa ofisini kwangu alikuja binti mmoja kuniomba kazi ya kufanya hapo ofisini kwangu.

Nilimwambia hapo napaweza mwenyewe ila nahitaji msichana wa kazi za nyumbani. Binti akaonekana km vile anadharau hiyo kazi, tukaongea Sana na mwisho akakubali kuja kufanya kwa makubaliano ya elf 90 kwa mwezi lkn asiseme kwa mke wangu, kwa mke wangu aseme elf 50. Msichana alikuwa mzuri wa wastani tu lkn alikuwa anavaa kwa staha Sana na alikuwa na rangi ile ya chocolate!

Baada ya kukubali kufanya ile kazi akaniambia anaishi na mwanaume, hivyo inabidi akaongee naye kwanza halafu kesho yake aniletee jibu. Niliheshimu maelezo yake na akaondoka! Ukweli yule binti alinivutia Sana hasa jinsi alivyokuwa anaonekana mstaarabu, mtu wa dini uvaaji wa kujisitiri hata kichwa huwezi kuona nywele zake!

Kesho yake mapema Sana akaja kuleta mrejesho. Akaniambia bwanaake ameridhia lkn awe anafanyakazi na usiku anaenda kulala kwake. Tukakubaliana kweli siku iliyofuata akaja kuanza majukumu yake! Binti alikuwa mzuri kila idara hapo nyumbani. Anajua kupika, msafi kwa kila kitu, nidhamu ya hali ya juu kabisaa, upendo kwa watoto wangu na kuwafundisha maadili mema. Tofauti yetu ilikuwa dini tu, yeye ni Islamic na sisi familia nzima ni christian.

Maisha yakaendelea na akawa kipenzi cha familia, mke akampenda Sana na mm nilikuwa nampenda mpaka na ule upendo mwingine lkn utamuanzaje sasa, umri wetu ulikuwa unaonekana tofauti Sana na alikuwa ananiita baba. Baadae akawa amenizoea Sana, akawa ananieleza Maisha yake na yule mwanaume, yaani kifupi alikuwa anatamani kuwa na familia yake lkn mwanaume haeleweki, hata kulipa kodi ya nyumba tu ilikuwa shida!

Siku moja baada ya kumaliza kazi zake na kurudi kwake, alienda kugombana Sana na huyo mwanaume. Mpaka mwanaume akampiga, alivyopigwa usiku uleule akampigia simu mke wangu na ikabidi twende huko. Tumejaribu kuwaweka sawa lkn dada alikataa kabisaa kuendelea kuwa pale na hivyo akang'ang'ania tuondoke naye. Na sisi kwa vile tulikuwa tunampenda ikabidi tuondoke naye. Hiyo ilikuwa January mwaka 2016.

Kesho yake akaenda kubeba vitu vyake akaja navyo pale nyumbani. Siku 2 baadae akaniomba mshahara wake kabla ya muda ili akalipie chumba sehemu nyingine. Kwa vile alishakuwa mtoto wa nyumbani nikawa nimempa. Akaenda kulipia na akahamia..akaendelea na ratiba zake za kuja na kulala kwake. Baadae tena akaingia kwenye uhusiano na mwalimu mmoja hivi ambaye anaishi kibaha.

Yule mwalimu akataka kumchumbia ili amuoe kabisaa! Hivyo binti kwa niaba ya wazazi wake akaomba hiyo barua iletwe kwangu halafu kwao wataenda kuoana tu. Me nikaruhusu hilo jambo jema lifanyike na kweli barua teacher akaleta na kwa vile nilikuwa nawasiliana na ndugu wa binti tukaijibu ile barua.

Kwakweli siwezi kuficha yule binti pamoja na yote hayo..lkn nilikuwa nimevutiwa naye sana! Kuna siku ilibidi nimwambie km utani tu. Ujue wewe(nikamtaja jina lake) we ni binti mzuri sana, ulifaa kabisaa kuwa mke wangu! Binti akatabasamu na kile kimwanya chake sasa, Acha kabisaa!!

Wakati anaendelea na mipango yake na yule mwalimu, mm pia niliendelea kumsisitiza kuwa itakuwa ni kosa kuwa mbali naye. Binti akasema haina jinsi baba, maana we ni mkristu na hamruhusiwi kuwa na wake wengi. Me km ungekuwa huna mke ningejiona nna bahati kuolewa na ww. Lkn kwa sasa acha tu na Mimi nikatengeneze Maisha yangu. Yule mwalimu wakati anamchumbia tayari alikuwa na mtoto mmoja, aliwahi kuishi na mtu bila ndoa lkn baadae wakashindwana na yule mama akamuachia mtoto.

Baada ya kuwa amechumbiwa, akawa analazimika sasa kila ijumaa jioni anaondoka kwenda kibaha,anarudi jpili jioni. Na kuna wakati akienda huko, jpili akirudi anakuja na kale ka binti katoto ka mumewe mtarajiwa. Mwezi wa 5 mwaka 2016 mke wangu alisafiri. Kuna siku nikawa nachart naye usiku Saa 5 hivi..tulichat sana..lkn ghafla akawa amebadilika akawa hajibu sms zangu..!!

Kesho yake asbh hakufika kwangu yaani kazini kwake. Simu akawa amezima, nikatuma mtu kwake hakuwepo tukaambiwa aliondoka alfajiri Saa 10. Nimekaa mpaka Saa 11 jioni ndo akapiga simu analia..ananiambia nimtumie nauli yupo kibaha. Mengine atanisimulia akirudi! Ikabidi nimtumie nauli..baadae majira ya Saa 3 usiku akaniambia yupo kwake lkn hajisikii vizuri.. nikamwambia basi nakuja hapo akasema sawa.

Nikatoka na mke nikampigia simu nikamwambia. Maana hata yaliyotokea asbh ilibidi nimwambie. Kwa hiyo alikuwa anajua kila kitu kinachoendelea hapa nyumbani. Jambo pekee ambalo alikuwa hajui ni lile la mm kumtamani huyo binti.

Nimefika pale kwake nimemkuta mnyonge Sana analia tu. Nikamtuliza nikamwambia anieleze shida nini! Binti ikabidi afunguke, kumbe wakati anachat na mm usiku, alikuwa anachat pia na mchumbaake, wakiwa wanachat kuna mazingira akawa hayaelewi. Akituma sms haijibiwi kwa wakati na ikijibiwa inajibiwa kwa ufupi tu. Akaamua kupiga simu haikupokelewa na alipojaribu tena akakuta simu imezimwa kabisaa! Hapo ndo kichwa kikazima naye akaacha kunijibu mm. Alfajiri Saa 10 akaamua kwenda kibaha kimyaa kimyaa. Amefika bado wamelala akagonga na kufunguliwa na kale ka binti. Kuingia ndani akanyoosha chumbani baada ya kuambiwa na binti baba yupo ndani na mama.

Mlango wao wa kitasa hawakuwa wameufunga alipojaribu kuufungua ukakubali..kwa bahati mbaya akamkuta jamaa ndo anapiga show ya asbh..akiwa na mzazi mwenzake yaani mama wa kale ka binti. Binti alishangaa tu macho yanaona giza na kuanguka. Hakujua tena kilichoendelea mpaka alipozinduka Saa 10 jioni akiwa hospital.

Alipozinduka akaulizia simu yake, na kumbukukumbu zikarejea na akajua kwa nn alikuwa pale. Nikamhurumia Sana binti na kumpa pole kwa kilichotokea na kumpa ushauri. Nilikaa naye sana, nikaenda kumnunulia chips, maana hata kula alikuwa hajala. Baadae usiku uleule akawa km Amani inarudi..na kwa vile usiku ulikuwa mwingi..chumbani tupo pekee yetu..binti hakuwa na hiyana..akanitunuku tunda la katikati, tunda la mema na mabaya. Na kuanzia siku hiyo uchumba kule ikawa ndo basi tena, na me na yeye ndo tukaingia rasmi kwenye kuvunja Amri ya 6 ya Mungu.

Story ni ndefu..kifupi tangu wakati huo nikawa na uhusiano na huyo binti. Pale ikabidi nimuhamishe na akanitafutia binti mwingine wa kazi yeye akaacha kazi. Tumepitia mengi na huyu mrembo, ameolewa kwa ndoa mara 2 kwa miaka hii 5 na kuachika! Lkn me na yeye kuchepuka hatuachi. Uhusiano wetu hata mke wangu alikuja kuungundua na ikawa kesi kubwa tu kidogo familia yangu isambaratike lkn hatukuachana.

Kinachonipa shida kwa sasa, huyu binti bado nipo naye, lkn simuonei tena wivu hata kidogo. Yeye pia hanionei wivu hata kidogo..kuna kipindi mwaka Jana nilikuwa mkoani nafanya shughuli zangu za kibiashara..nikamuita aje huko. Kweli akawa amekuja..lkn mm huko mkoani nilikuwa na dem mmoja Mhaya huyu alipofika ikabidi nimwambie me nna demu wangu hapa, kwa hiyo nitamwambia ww ni mdogo wangu..kweli kesho yake nikamtambulisha..na jioni ya siku hiyo yule Mhaya akaja tukalala chumbani huyu binti akalala sebuleni. Alfajiri akaondoka Mhaya binti akaja chumbani tena ana Genye za kufa mtu wala hakujali km nilikuwa na mtu.

Mpaka ameondoka akarudi Dar yule Mhaya akijua ni mdogo wangu. Yaani hatuoneani wivu kabisaa! Baadae mm nimerudi Dar..tumeendeleza libeneke km kawaida ingawa ameshaniambia kuna jamaa anaishi naye tena lkn ni mariooo!

Wiki 2 zilizopita nilimuita aje sehemu. Nikamuelekeza maana hakuwa akipajua ile sehemu. Alipokaribia na mm nikawa naenda hapo. Wakati nakaribia, me nilitokea kinjia cha uchochoro nikatokea barabarani..ile natokea na yy huyu hapa akiwa ameambatana na jamaa mmoja. Akanionyesha kwa kidole nisimsemeshe...

Me nikakausha wao wakapitiliza baadae kidogo akanipigia akiomba maelekezo akawa amekuja. Amefika akaniambia lili ni danga lake lilienda kumfanyia shopping..akanionyesha nguo alizonunuliwa, chupi na shanga..!! Basi sisi tukaendelea kula Maisha hakuna wivu.

Yule danga alidanganywa kuwa dem yupo single..juzi Kati hapa ikabidi afuatlie usiku mpaka pale kwenye chumba cha dem si ndo wakakutana na yule jamaa anayeishi naye, bahati nzuri police jamii walikuwa eneo lile wakawa wamewachukua hadi serikali za mitaa! Kwa sasa mm ndo natumiwa na dem km msuluhishi wa mgogoro wao na huyo marioo..jamaa naye ananiheshimu bila kujua me mwizi wa huyo dada wa kudumu. Hebu turejee kwenye swali langu..huyu msichana nampenda Sana, lkn mbona sina wivu naye Wala yeye hana wivu na Mimi!?? Yaani hii kiufundi inaitwaje!?. Nawasilisha.

Poleni kwa andiko refu na kwenye makosa ya kiuandishi mtavumilia maana siwezi kurejea kuanza kuhariri.
 
Upendo kati yenu ushaisha. Mnatumiana kimwili tu kwa kuwa kwako ni rahisi kumpata na kujiridhisha kingono na pia anakuheshimu wewe na familia yako na michepuko yako.

Na pia yeye anajitimizia haja zake kwa kuwa unam save hela na kumpa penzi bila wivu wala kero.

Kilichobaki mnatumiana tu.

Wewe ngono yeye hela.

All in all UKIMWI upo na unaua.
 
Nyie mapenzi ya wivu yameisha yamebaki matamanio ya kudumu kingono.. Yaani kuna mahali mnakifikishana mkiwa pamoja.. Mmekuwa sex partners... Ni ngumu kuachana kwa huo muunganiko wa kiroho mliotengeneza.

Tatizo liko kwako zaidi uliye na ndoa.. Huyu yuko huru hana cha kupoteza na hana maumivu ya kutendwa tena, amebaki kudanga.. Hisia za ule upendo wa kweli tena kwake zimekufa.

Shida kwako ni hii hapa, huwezi kumuacha na in fact huwezi kutumia condom kwake pengine, asipokuletea magonjwa ya kimwili kama hepatitis B na ukimwi basi atakuja kukuletea magonjwa ya kiroho kama nuksi au mapepo ya ngono....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom