Mkuu
Mushi92 , habari ndugu.
Tangu zamani huwa nipo interested sana kutafuta riziki kupitia sector ya madini. Ni uhaba wa mtaji ndiyo umekuwa ukinikwamisha, ila pia kutokuyafahamu vizuri madini ni changamoto nyingine.
Mie nataka kufanya 'ukota' kwenye dhahabu tu! Naplan kuja Katoro, na kwenda kujikita pale Msasa kwaajili ya kufanya ukota. Najua ukota hauna limitation ya mtaji... hata mtaji wa gram 3 naweza anza.
Niwe muwazi na mkweli, SIIJUWI dhahabu. Dhahabu siifahamu kabisa!
- Ombi... kama inawezekana upande wako mkuu, je waweza kuwa mwalimu wangu kunifundisha na kunipa uzoefu wa kuijua vizuri dhahabu ilivyo?
- Ukota unaweza fanyika informally kienyeji? ama kuna taratibu za kisheria ambazo ni lazima kuzitimiza kwanza?
- Ni vifaa (vitendea kazi) vipi vya lazima kuwa navyo ili kufanya ukota?
Natarajia kuja Katoro/Msasa siku ya Jmosi week hii kufanya kasurvey kuhusu suala hili.
Mambo yamekuwa taiti sana huku jijini, tunan'gang'ania kukaa mijini huku mifuko imetoboka haswa. Hatuna kitu. Kama kijana, nimeona sasa ni wakati kwenda popote kusaka maisha. Popote kambi.
Natanguliza shukrani.