Msaada: Fursa za kiuchumi Katoro Geita

Msaada: Fursa za kiuchumi Katoro Geita

Mkuu Mushi92 , habari ndugu.

Tangu zamani huwa nipo interested sana kutafuta riziki kupitia sector ya madini. Ni uhaba wa mtaji ndiyo umekuwa ukinikwamisha, ila pia kutokuyafahamu vizuri madini ni changamoto nyingine.

Mie nataka kufanya 'ukota' kwenye dhahabu tu! Naplan kuja Katoro, na kwenda kujikita pale Msasa kwaajili ya kufanya ukota. Najua ukota hauna limitation ya mtaji... hata mtaji wa gram 3 naweza anza.

Niwe muwazi na mkweli, SIIJUWI dhahabu. Dhahabu siifahamu kabisa!
  • Ombi... kama inawezekana upande wako mkuu, je waweza kuwa mwalimu wangu kunifundisha na kunipa uzoefu wa kuijua vizuri dhahabu ilivyo?
  • Ukota unaweza fanyika informally kienyeji? ama kuna taratibu za kisheria ambazo ni lazima kuzitimiza kwanza?
  • Ni vifaa (vitendea kazi) vipi vya lazima kuwa navyo ili kufanya ukota?
Natarajia kuja Katoro/Msasa siku ya Jmosi week hii kufanya kasurvey kuhusu suala hili.

Mambo yamekuwa taiti sana huku jijini, tunan'gang'ania kukaa mijini huku mifuko imetoboka haswa. Hatuna kitu. Kama kijana, nimeona sasa ni wakati kwenda popote kusaka maisha. Popote kambi.

Natanguliza shukrani.
niaje brooo???bado upo Katoro???
 
Ndo ninataka kwenda, kati ya maeneo ya misungwi, buseresere, katoro, au mpanda ,

Katoro imenivutia zaidi.
Katoro ni sehemu yenye watu wengi na pia mzunguko was biashara ni mkubwa.wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali huleta bidhaa zao katoro kutoka na miundo mbinu mizuri yaani barabara nk. Pia wajasiriamali kutoka Uganda huleta bidhaa zao hapo ambapo wateja kutoka sehemu mbalimbali hukutana na kufanya exchange zao.
 
Uko bado kunamapori ya kutosha. Choma mkaa bro. Uwe unapakia kwenye malori yanayotoka Rwanda, DRC, burundi au Ug kwenda dar. Gunia la elfu 10,000 unafikisha dar unauza 50,000 had 70,000
 
Wakuu,

Naomba kufahamu kwa undani mji wa Katoro.

Fursa zake za kiuchumi, kilimo, ufugaji, biashara, miundombinu, makazi n.k.

Je ni sehemu salama pia?

Asanteni.

Mie naishi Katoro hapa mjini nafanya shughuli ya tofali za kuchoma zinalipa sana nitafute pm nikupe michongo zaidi
 
Utachoma fedha kwa biashara hiyo. Pande za Geita na Katoro ni miongoni mwa sehemu ambazo wananchi wanaamini sana Waganga wa kienyeji sasa ukija na biashara ya duka la dawa ni kweli utapata fedha lakini sio kwa kiwango unacho fikiria
Hata mazao na mifugo inayohitaji madawa wanatumia waganga wa kienyeji?
 
Back
Top Bottom